Marehemu Kibo Marealle alifariki jana Jumapili asubuhi nyumbani kwake Mbezi Beach (njia ya Africana karibu na Jangwani Sea Breeze hotel) jijini Dar. Habari za kifamilia zinasema Kibo alifariki ghafla na kila mtu ameshangazwa na kifo hicho, kwani habari zinasema siku moja kabla ya mauti kumkuta Marehemu alikuwa katika sherehe za mahafali na kuzaliwa kwa rafiki wa familia sehemu za JKT Mlalakuwa jijini na akiwa buheri wa afya.
Kwa sasa msiba uko nyumbani kwake wakati mipango ya kusafirisha mwili wake kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika kwao Marangu Moshi siku ya Jumamosi.
Kwa mujibu wa taarifa za kifamilia misa ya kumuombea pamoja na kuaga mwili vitafanyika siku ya Alhamisi hapo nyumbani kwake Mbezi Beach kuanzia saa nne asubuhi.
Kwa niaba ya wadau wote Globu ya Jamii inatoa pole kwa wafiwa na kumuomba Mola aiweke roho ya Marehemu Kibo Marealle mahala pema Peponi. Sisi tulimpenda lakini yeye amempenda zaidi. Jina lake na lihimidiwe - Amin
Marealle usiku kuamkia leo nyumbani kwa marehemu Mbezi Beach
waombolezaji wakitoa pole kwa wafiwa usiku wa kuamkia leo
Marehemu Kibo (mwenye fulanazzz nyekundu) akiwa na marafiki katika sherehe za mahafali ya
rafiki wa familia Mlalakuwa jijini Dar siku ya Jumamosi kabla ya mauti
Kibo akijumuika kusherehekea siku ya kuzaliwa
ya rafiki wa familia Jumamosi mchana


rafiki wa familia Mlalakuwa jijini Dar siku ya Jumamosi kabla ya mauti

ya rafiki wa familia Jumamosi mchana
poleni sana wanafamilia kweli nilishtuka sana kusikia hizi habari pole sana dada mercy kwa kuondokewa na mume wako mpendwa
ReplyDeleteR.I.P kibo
R.I.P
ReplyDeleteunajua mtu kufa gafla kunatokana na sababu nyingi tofauti. si ajabu alikuwa na matatizo ya moyo ukaamua tu kusimama gafla au ndio cholesteral imezidi, sugar, nk inatakiwa sie wote tuwe tunaenda kwa madaktari kupima kila kitu kila mwaka, mara nyingi damu huwa inaeleza mambo mengi mno. kwa huku ulaya wanajua mpaka ukiwa una dalili za heart attack nafikiri hata nyumbani pia.
vitu vya kuwa macho navyo:
-kifua kikiuma upande wa kushoto
na maumivu yanaelekea mpaka
kwenye mkono wa kushoto.
-ukosaji pumzi.
-kichefuchefu na kizunguzungu.
wadau, mjue kwamba maumivu ya kifua si mchezo na huwa yanaweza kwenda na kupotea halafu yakarudi tena baadae, na saa zingine wakati unafanya kazi nzito unaweza kuona maumivu ukadharau, lakini ujue wazi unakaribisha kifo.
nategemea mtatilia maanani maoni yangu.
dr. mtarajiwa.
Mwanga wa Milele akuangazie.
ReplyDeleteBy the way Marehemu atakufaje? Mnang'ang'ania kuongea na kuandika kiingereza fasaha wakati kiswahili mnachoandika au kuongea ni kibovu.
R.I.P KIBO
Our deal lord has called another. Our thoughts and prayers are with the family.
ReplyDeleteMay God rest his soul in eternal Peace.
MARA NYINGI NIMEKUA NIKISOMA GLOBU YA JAMII LAKINI UANDISHI WAKE UMEKUA KAMA MTU ASOKUA NA TAALUMA! NAMAANISHA YA KWAMBA,MWANDISHI ANAANDIKA KAMA VILE ANAONGEA NA MTU HAPO KWA HAPO,BILA KUWEKA NOTABILITY YA KITU,MFANO KIBO MAREALE,KWA WATU TULOKUA NJE YA NCHI TUTAMJUA NI NANI NA ANA UMUHIMU GANI?HII SI MARA YA KWANZA,KWA VILE UNAJARIBU KUELIMISHA BASI ELEZEA ALIKUA NI NANI NA UMUHIMU WAKE SIO KILA MTU ANAMJUA YEYE NI NANI.NI HAYO TU KAKA MICHUZI(MDAU UGIRIKI NURAMO)
ReplyDeleteShocking. So sudden.
ReplyDeletePoleni.
Wengi tumegutushwa sana baada ya kupata taarifa ya kifo cha Kibo. Mtu mwema, mcheshi na mpenda watu. Kweli wengi tutakukumbuka kwa urafiki uliokuwa nao kwetu; bila ya kujali umri, utajiri wala umaskini. Hata miaka mingi ikipita hatujaonana, Kibo you always remembered your friends and greeted them with great warmth.
ReplyDeleteMy heartfelt sympathy and condolences go to Mercy and the Marealle & Kida families and all friends and relatives. May the Almighty God give you eternal peaceful rest. Amen.
UK
London
R.I.P
ReplyDeleteOh My GOD...what a sad news...
Nashindwa kukubali,kama bado nipo usingizini,baada ya miaka mingi iliyopita katika ujana wetu,tukiwa pamoja karibuni kila week-end katika sherehe mbalimbali nashindwa kukubali kabisa kama Kibo hatunaye tena...
Mungu ana mipangilio yake katika maisha yetu,tumwombee amsamehe makosa yote amweke mahali pema peponi.
Nawapa pole ndugu na marafiki wote katika msiba huu wa ghafla.
Mickey Jones
Denmark
wewe anony wa 04;55pm kama wewe humjui wengine wanamjua hii ni blog ya jamii hata wewe ukifiwa unaruhusiwa kumtumia habari na bro michuzi akailusha mshamba we
ReplyDeletewewe anony wa 04;55pm; Unataka Michuzi awe anaweka taarifa za misiba ya nani na aache ku-post msiba wa nani????.... Unataka kusema ukisoma gazeti na ukakuta matangazo ya vifo yote unakuwa unayajua ni akina nani????.... Acha ushamba wewe, Mnadandia magari kwa mbele hamna nauli na haujui uendeko....
ReplyDeleteSikuwahi kumfahamu marehemu lakini Comments za huyo bwege hapo juu zimenichafua nyongo
$#&*@#@# we, msonyo......
Poleni Familia kwa msiba na wafiwa kwa ujumla.
Anony wa 08:53:00 PM acha ghadhabu kwa anony wa 04.55pm, jamaa ana jaribu kutaka kumfahamu marehemu kama alikuwa anajulikana kwa watu sana akimaanisha mtu mashukuri . sidhani kama alikuwa anamaanisha watu special ndio wanaweza kuwekwa humu.
ReplyDeleteKutoa habari ndani ya globu ya jamii inakupasa kuielezea habari kwa kina kidogo ila kila mmoja wao aweze kuelewa.
Kama ni habari ya kifo, basi japo elezea wasifu aliokuwa nao marehemu, ama shughuli alizozifanya.
tuache jazba jamani lol !
Mdau No 5 .
Mwenyezi Mungu ampe pumziko la milele. Amina.
ReplyDeleteMbigiri umesema kweli Kiswahili kinafinyangwa finyangwa na Waswahili wenyewe. Watu wanakosea mambo madogo madogo wanaona kawaida tu. Kusema marehemu alifariki, ni lugha mbovu kwani marehemu hawezi kufariki. Ili uitwe marehemu shurti uwe umefariki.Tuwe makini jamani.
Kibo Marealle!
ReplyDeleteTulisoma wote Mzumbe, Morogoro. Namkumbuka alivyokuwa mtu wa utani utani bila aibu, kusita alilosema, au namna alivyokuwa kibinadamu. Hiyo ilikuwa 1973-74.
Baadaye kama inavyojiri maisha haya; sikumwona hadi habari zilivyowaka jana. Taswira iliyobakia akilini ni ya kijana anayecheka cheka kirahisi; anayefanya masihara, kavaa kaptula ya shule na raba, anasogoa na wenzake, sote tukingojea kwenda darasani. Alikuwa bweni moja na marehemu Kapteni Cuni Zongo( aliyefariki mwaka 1997) na Profesa Chachage (aliyefariki 2006).
Shule ya Mzumbe miaka hiyo ilikuwa shule ngumu, ya shida na mambo mengi; ilijenga vijana wa kila aina. Kati ya tabia kuu zilizopiganiwa pale shuleni ilikuwa kuijali jamii yako, uzalendo na kupenda au kujali wenzako. Jamaa wengi waliosoma pale kama hawakuwa viongozi ama wataalamu kama marehemu Zongo na Chachage, hawasahauliki.
Si ajabu kifo chake Kibo kimestua wengi hasa wale waliomjua au kumsikia.
Mungu aiweke roho yake Kibo pema peponi!
Amina.
Hili ndio kosa moja Tanzania mtu akijaribu kujenga wengine wanabomoa,Kuna mambo 2: Matangazo yanawezwa kuwekwa na mtu yoyote yule lakini kwa njia tofauti na yakafahamika:Mbona juzi tu hapa kulikuwa na tangazo la kifo cha tu Canada na hakuna alielalamika: Kwa kuwa limeanza kwa kuelezwa MSIMBA CANADA! tushafahamu ndugu yetu aemtutoka na asiwe na umuhimu wowote: lakini sio Uweke tu matangazo Flani hatunae tena haya kwa nini usiweke Msiba Dar es salaam tukajua kuna msiba: Lakini aina ya tangazo lilivowekwa inaonesha ni mtu mashuhuri sana sasa tuelezwe ili tupate tumjue:Hapa commet zote sijaona Kibo alikua ni nani hadi sasa na tuna hamu kumjua kwa kuwa ni mtanzania mwenzett: Sasa watu wakielezwa haya wanapanda Jazba:Mfano mzuri Fundikira.. alikua mchezaji timu ya .... au Flani Alikua dj au Flani alikua ... sasa Kibo tu,tutamjua ninani sasa si bora aandike tu MSIBA DAR?
ReplyDeletePoleni sana wafiwa ndugu jamaa na marafiki mliomfahamu marehemu kwa karibu na hata wale mliowahi kumsikia kwa ajili ya sifa zake za ki binadamu za kujali wenzake bila kuangalia utajiri, cheo n.k. POLENI SANA.
ReplyDeleteWewe anon 11:07pm na nyie wengine wote kama huyo anon juu...wewe kama hukumfahamu marehemu basi hilo ni lako na usiweke hasira zako kwenye blog hii ya jamii kutaka kujua marehemu alikuwa na sifa zipi...alikuwa binadamu mwenye utu!Nadhani hiyo ni sifa tosha kabisa zaidi ya hizo nyingine unazozitafuta..sijui mcheza mpira..sijui nini..kuwa na utu labda na wewe siku moja ukiaga dunia utawekwa kwenye blog hii ya jamii na labda watu kama mimi na wengine wengi tusiokujua tutasikitika na kukuombea pumziko la amani...kumbuka hiki ni kipindi kigumu kwa wafiwa na badala ya kuanza kuuliza vijiswali vyako vya ki ubinafsi tafadhali onyesha utu na angalia mambo kwa undani na elewa maana yake kabla hujaanza kubwabwaja....ni hilo tu zingatia!
Pole kwa familia ya Mareare...
ReplyDeleteJamani mimi si mwandishi wa habari kwa taaluma, lakini najua ni vigumu kuandika habari katika namna ambayo utagusa hadhira yote kwa kiwango kile kile! Kwa watu walioko Bongo na wanaofuatilia habri familia ya Mareale ina kaumaarufu kiasi fulani, ni kama ilivyokua msiba wa S. Fundikira, Kwa hiyo kuna watu watamfahamu na wengine hawatamfahamu. Naomba tuahe kukosoa uwasilishaji, wewe soma pata ujumbe songa mbele!
Hili tatizo lipo sana kwa huyu Michuzi, naweka kitu akiandika kama utani au kama vile wote tunamjua, Kibaya zaidi inabidi utafute data zaidi za huyo mtu
ReplyDeleteNimemsikia sana na ku muona huyu Marehemu mara moja tena kwenye Msiba wa mama Bomani , ila hapo kwenye picha za chini nimeshindwa kumjua ni huyo mwenye tshirt nyekundu ndio KIbo Marealle?
MIchuzi najua huwezi badilika ila tafadhali unatuudhisana kutoa tarifa nusu nusu, kama mfano , hapo kwnye picha ya marehemu na hizo walizo kaa hazifanani ni vizuri ungeema Kibo Mareale mwenye nguo fulani au ungesema waliye upande fulani tungeelewa na hata kuelezawaifu wak kidoko kama ni mfanya biashara au ni ana uongozi fulani, kuliko kuema amefariki ghafla wakati wengi wange taka kujua ni nani.
Nashindwa kukuelewa ile presentantion uliandikiwa au ilikuaje kwanini vitu vidoo huwezi kuvifanya vizuri ? ole wako JK akupe ukuu wa wilaya haki nita shinda njaa mbaka wananchi wandamane kukukataa.
hata kama unasafiri ugenini ukapita sehemu ukkambiwa kuna mtu kafa na watu wasikitika kufiwa kiungwana utaungana nao nakutoa rambirambi zako ndipo uendelee na safari zako huwezi kuanza kuuliza huyo aliyefariki ni nani? na anaumuhimu gani kwenye jamii? kwani kifo kimeumbiwa nani? kwani mtu hawezi kufa bila kuwa na umuhimu wowote? na ukifa bila umuhimu hautangazwi? jamaa kaniboa mpaka basi wafiwa poleni, achaneni na jamaa kachanganyikiwa!
ReplyDeleteKibo gone too soon,
ReplyDeletegone without a word,
gone with your humbleness,
gone with your charm
gone with your kindness,
The memories left behind
will linger in our hearts forever,
May you rest in peace
Kibo!We will miss you!
From old classmate.
RIP Kibo, hivi jamani mbona watu hamna ustaarabu? hizi comments mnazoandika hazina taste nzuri!
ReplyDeleteondoeni upuuzi wenu hapa kwani mkijua marehemu alikuwa nani itawasaidia nini? umbea tuu alikuwa na makampuni yake na alikuwa mtu wa watu mkitaka zaidi hudhurieni mazishi yake ili mkasikie wasifu wa marehemu!
ReplyDeleteR.I.P kibo tulikupenda ila Mungu kakupenda zaidi
Nadhani cha Muhimu hapa ilikuwa ni kutoa taarifa na taarifa imefika, kama ilivyokuwa, Breaking News, sidhani kama kuna muda wa kutosha kutafuta maelezo zaidi ya Marehemu, ambaye alikuwa ni mtu maarufu na kwa wanaomfahamu ambao ni wengi tu duniani pote,taarifa ilisambaa kwa muda mfupi tu, sasa ndugu yangu anayekuwa na muda wa kukaa kwenye kompyuta yake na kuanza kuhoji na nani, anafanya nini badala tu kwanza kuwapa pole wafiwa na umtafute Michuzi kwa wakati wako na kero zako, unaacha maswali mengi sana juu ya wasifu wako wewe mwenyewe, Mwenyezi mungu ampumzishe marehemu Kibo Marealle mahali pema, ameen.
ReplyDeleteAnyway tatizo siku hizi jamii imekuwa kubwa sana NA WATU WAKUJA WAMEKUWA WENGI. Enzi zetu za shule na mabugi ya mjini miaka ya sabini mpaka themanini hivi, sisi wengine na Michuzi akiwemo, mjini Dar es Salaam watu wa mjini tulikuwa tunajuana.
ReplyDeleteNamkumbuka KIBO Mareale 1977 akiwa ansoma CBE alikuwa maarufu sana kwa wana vyuo mabli mbali mpaka sehemu zote za burudani. So Michuzi alivyotoa hiyo habari kawalenga watu watokea enzi hizo na umaarufu wa kijana huyo. Kama ulikuwa humjui KIBO au familia ya kina KIDA alikooa enzi hizo basi ujuwe wewe ni mtu wa kuja,kaa kimyaa
R.I.P Kibo,
ReplyDeleteNyie mnaoshoboka alikua nani, sijui ana umuhimu gani kwenye jamii mna maana gani? AU ULITAKA TU TUJUE UKO NJE YA NCHI? Kua mstarabu acha ushamba, nyoooo
May the Lord grant you eternal peace Kibo.
ReplyDeleteDada Mercy our thoughts and prayers are with you at this difficult time.
Those who knew him lost someone special.
POLENI SANA WAFIWA!!!
ReplyDelete(Mon Apr 05, 11:07:00 PM,) Nimependa point yako. tunapopenda kumfahamu mtu si kwamba lazima awe mashuhuri lakini mimi nimelazimika kuzama kwenye comments labda nitapata details za marehemu, ukiwa unamfahamu ni rahisi sana kuona hili jambo ni la kipuuzi lakini sivyo. kiufupi tuwekeeni details kidogo tupate kufahamu wasifu wa marehemu maana hata misiba yote huwa ina wasifu hata huo utakuwa na wasifu sasa kwa mtu asiyefika ni vyema akimfaamu marehemu japo kidogo.kama hupatata details basi tumia hata 'Msiba Dar' inasaidia msomaji kufahamu nu mtu wa aina gani. asante
MAREALLE ni familia ya kitajiri na wanajulikana hapo tangia enzi za mkoloni . Wanawake wanataka kuolewa na marealle na wanaume wanata kuoa marealles . Sasa hapa huyu kaka ni mjukuu wa MAREALLE . Lazima ni mfanya biashara na na mashuhuri . MAREALLE ni kama KENNEDYS watu ambao wako famous kwa jina hata kama hawana lolote . Hili ni tatito la dunia nzima kama haujulikani kijina inakuwa ngumu sana kujulikana kwenye society regardless how succesful you are . Mfano OBAMA mpaka sasa hili jina linafanya watu wajiulize kazaliwa wapi ? Angekuwa KENNEDY haaa k . HUYO NI MJUKUU WA MAREALLE . R.I.P
ReplyDelete..........Nashukuru mdau wa Tue Apr 06, 02:49:00 PM, at least Tumepata walau wasifu kidogo wa mjukuu wa MAREALLLE.
ReplyDeleteStop the bickering please he was a human being like everyone else. A life is gone thats what matters. To classify who is who does not make any sense at this time. Let his wife Mercy, and their families grieve. Poleni sana familia ya Marealle na Kida. Mungu ampumzishe Kibo kwa amani.
ReplyDeleteKwanza kabisa naanza na kuwapa pole wafiwa na kuwaombea Mwenyezi Mungu awatie nguvu hasa katika wakati mgumu kama huu wa kuondokewa na ndugu yenu mliye mpenda, pili naomba bwana Michuzi sasa afikirie kuanzisha full website ambayo inaweza kukidhi haja za wengi, kwa mfano nimeona hapo katika mabishano inaonyesha watu huingia hapa kwenye hii blog kwa interest tofauti hivyo bwana michuzi akiweka website itakuwa rahisi kuweka habari chini ya headline zilizopo, kwamfano anaweza kuwa na kipengele kama vile: BREAKING NEWS
ReplyDeleteHARUSI
MICHEZO
MATANGAZO YA VIFO
HABARI ZA KIBIASHARA
HABARI KUTOKA UGHAIBUNI
HABARI KUTOKA NYUMBANI N.K
Hebu fuatilia hii website ya Michuzi wa Kenya. www.misterseeds.com, nadhani mtapata picha ya ninacho ongelea.
Majina makubwa Tanzania ambao wako kwenye system tangia enzi hizo either walikuwa kwenye government or private companies. Ni watu wenye elimu, wafanyabiashara na wana standard. Hata uwe na millions huwezi kunock them out kwa reputation waliyotengeza tangia enzi za mababu. Tangia miaka ya 1960’s ni majina ambayo nimesikia na mpaka sasa. No matter they are now rich or not. Walitanua enzi zao na wengine mpaka sasa. Either you take it or not, u can add. Kama unabisha then jiji la Dar hulijui.
ReplyDelete1. Marealle
2. Kida
3. Mbowe
4. Mdope
5. Kahama
6. Janguo
7. Luangisa
8. Mselikari
9. Kile
10. Kusaga
11. Rweyemamu
12. Bakharesa
13. Mulokozi
14. Lwakatare
15. Mtulia
16. Rwehumbiza
17. Malima
18. Lema
19. Kazaura
20. Andrews
21. Bomani
22. Makani
23. Ngaiza
24. Mtei
25. Malecela
26. Michuzi
Kuna baadhi ya nchi ukiishi muda mrefu zinakugeuza unakuwa mtu wa kisirani full time!
ReplyDeleteUnaanza kidogo kidogo mpaka inakuwa kwenye damu.
Unaishi kwenye kiji-nyumba chako hu-associate/socialize unakuwa kama mnyama aliyefungwakwenye cage na hakuna visitors.
Unamalizia frustrationzako kwenye blogu!
Rudi nyumbani, maana na wanao watakuwa hivyo hivyo.."maddogs"
all in all,We need to focus what God needs as to be in this 3world.just love each other cause love start from God.we are all passing here is not our home.
ReplyDeletekibo marealle finish his way.so its time to think the short time remain for us to leave in this world .
GOD GIVE,GOD TAKE.BLESSING HIS NAME.AMEN.FROM JBM