kuhusu matumizi ya kiswahili ktk shughuli rasmi za kiserikali
SERIKALI imeagiza kutumika kwa Kiswahili katika usaili kwa watu wanaoomba kazi kwenye Wizara na Idara za Serikali na pia imetaka matangazo yote ya kazi za idara za umma yatolewe kwa lugha hiyo badala ya lugha ya kigeni kama inavyofanyika sasa hivi.
Katika agizo hilo, pia serikali ambalo lilitolewa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika bungeni, imeagizwa dhifa mbalimbali za kitaifa, hotuba za viongozi, warsha, semina na mikutano ya kitaifa iendeshwe kwa Kiswahili.
Pia alisema maofisa wa serikali na mashirika ya umma watumie Kiswahili katika shughuli zote kama vikao vya Bodi na mawasiliano ya kiofisi pia yaendeshwe kwa lugha hiyo ya taifa pamoja na kuandika madokezo.
Pia aliagiza sheria zote ziandikwe kwa Kiswahili ikiwa ni pamoja na kutafsiri zile zilizoandikwa kwa lugha za kigeni. Alisema jitihada za makusudi zifanyike ili shughuli za Mahakama katika ngazi zote ziendeshwe kwa Kiswahili pia.
Katika agizo hilo, pia serikali ambalo lilitolewa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika bungeni, imeagizwa dhifa mbalimbali za kitaifa, hotuba za viongozi, warsha, semina na mikutano ya kitaifa iendeshwe kwa Kiswahili.
Pia alisema maofisa wa serikali na mashirika ya umma watumie Kiswahili katika shughuli zote kama vikao vya Bodi na mawasiliano ya kiofisi pia yaendeshwe kwa lugha hiyo ya taifa pamoja na kuandika madokezo.
Pia aliagiza sheria zote ziandikwe kwa Kiswahili ikiwa ni pamoja na kutafsiri zile zilizoandikwa kwa lugha za kigeni. Alisema jitihada za makusudi zifanyike ili shughuli za Mahakama katika ngazi zote ziendeshwe kwa Kiswahili pia.
Habari Kamili
basi na mitaala iwe kwa kimatumbi miswaada ya bunge pia maana tunaona sheria nyingi sinapitiswa sababu waheshimiwa luga gongana
ReplyDeleteHongera Mkuchika na serikali kwa uamzi huu. Uamzi huu umechelewa lakini hata hivyo bado ni muhimu. Kawia ufike. Kiswahili ni lugha na sehemu muhimu ya utamaduni wetu. Tujivunie Kiswahili na ni wajibu wetu kukiendeleza. Tumefika sehemu watu wanaona aibu kuongea Kiingereza chenye makosa lakini Kiswahili chenye makosa wanaona ni kawaida tu. Vyombo vya habari ni lazima viwe mstari wa mbele kutumia Kiswahili fasaha. Kuna Kiswahili kibaya sana katika vyombo vyetu vya habari. Hata katika vipindi rasmi kama taarifa ya habari. Ni wajibu wa kila Mtanzania kukipenda Kiswahili na kukiendeleza nje ya mipaka ya nchi yetu. Tuwe kama Wachina, Wajapan, Wakorea, Wafaransa nk ambao wameweka lugha zao namaba moja kwanza. Tujifunze lugha za kigeni pia, ila ziwe namba mbili baada ya Kiswahili.
ReplyDeleteASANTE SANA MHESHIMIWA WAZIRI KWA TAMKO LAKO LENYE MANUFAA KWA UTAMADUNI WA MTANZANIA.LUGHA YA KISWAHILI NI KIOO CHA UTAMADUNI WA MTANZANIA.HUU NI WAKATI UFAAO KWA WATANZANIA KUANZA KUWEKEZA KWENYE MAENDELEO YA KISWAHILI.
ReplyDelete"JASIRI HAACHI ASILI NA MUACHA ASILI NI HASIDI"
----------------------------------
Mdau na mtetezi wa Kiswahili.
BaruaE:mcraynjau@gmail.com
--------------------------------
MUHIMU HAPO NI KUWA KUANZIA CHEKECHEA HADI CHUO KIKUU TUSOME KWA KISWAHILI SIO KUTUCHANGANYA HAPA VITABU TUNASOMA VYA KIINGEREZA KAZI KWA KISWAHILI
ReplyDeleteMIMI NAFIKIRI KISWAHILI FASAHA KINGEANZA KWANZA KUTUMIKA HUKO HUKO BUNGENI MNAKOTUNGA SHERIA MAANA HUKO NDIO KUNA KISWANGLIS KULIKO SEHEMU YOYOTE ILE HAPA TANZANIA MAANA MNATUNGA SHERIA AMBAZO HATA NYIE HAMUWEZI KUTEKELEZA KILA SIKU MNAONGEA KIINGEREZA BUNGENI
ReplyDeleteWabunge acheni hizo english ndio lugha inayokubalika kuwa namba moja global ok tungeni sheria za kupambana na ufisadi ok
ReplyDeletehizo ni longo longo tu hata USA kuna english na spanish kila mtu ana uhuru wa kutumia lugha atakayo
ReplyDeleteKwani Tanzania si ina lugha mbili za Taifa yaani Kiswahili na Kiingereza? sasa hii lugha ya kigeni ambayo ilikua inatumika kwenye kutangaza kazi za serikali ilikua ipi tena? Kihindu, kijapani au kimandarini?
ReplyDeleteDuh Ama kweli kwahiyo Kwahiyo yes yes of course me and you hakuna tena ! Me kissing you shavuni no no!
ReplyDeleteDuh kwa hiyo wanetu nikimatumbi kwakwenda mbele sasa nchi zawatu wata compete vipi kazini?
duh Padogo, but anyway! Yote mambo.
Umombo uleeee!
Mbona tunashindwa kupangalia mambo jamani.? sasa nini maana ya mitaala kwa shule za sekondary na vyuo vikuu kuwa ya kiingereza?
ReplyDeleteUshauri,: Tanzania tujifunze kuwa tunafanya research kabla ya kutoa maamuzi yenye long time effects. tunayaona sasa hivi tu wakenya wanavyo tuzidi katika soko la ajira kwasababu ndogo tu ya wao kojua kiingereza kuliko sisi.
sikubaliani na hou uamuzi hatakidogo.
Tatizo la kuwa na wabunge vihiyo. Yaani kwa kuwa hawaelewi kiingereza kwa kukimbia umande wameona kuahalalisha uwepo wao bungeni wabadili lugha.
ReplyDeleteLugha siyo hoja, hoja ni uwezo wa kupembua mambo na kuongeza ufanisi.
Kama wanataka kuirudisha nchi zama za ujima basi wang'ang'anie kiswahili chao ambacho 70% ya maneno ni Kiarabu. Hatuwezi kuendelea kwa style hii ya wavivu wa kufikiria. Kama mtu unaelimu na umequalify why not be able to speak the literate language?.
Siasa tupu na upotezaji wa muda, mambo ya maana kama kuhakikisha maendeleo, kuondoa foleni jijini, kupunguza uhalifu kwa kuongezajira kwa vijana na kupiga vita ubadhirifu na ufisadi yanawashinda wanageukia vitu ambavyo ni nonsense.
hakuna utumwa mkubwa kama kujiona dhalili sasa hii a atua italeta maendeleo nchini zimbabwe wageni wana rush kukamikisha law ya kotoa hisa kwa wafrica huu ni mwanzo mzuri na sisi tunaweza mpoto ansema fikra sahihi uja na lugha sahihi.
ReplyDeleteKalikali inabidi ujue kiswahili kina very poor vocabulary. Ndio maana ukiwa unaongea na watu, wakati mwingine unajikuta unatumia maneno ya english. Kwa sisi tulio US, wenyeji huwa wanatuuliza tafsiri za maneno fulani fulani, hato maneno hayapo kwenye kiswahili, a clue that swahili is a very limited language. Pia hakuna utamaduni ambao ni uniform kwa wa Tanzania wote, kwa sababu Tanzania ina makabila zaidi ya 100, na kumbuka kila kabila lina utamaduni wake. Kwa mfano, utamaduni wa kimakonde, sio sawa na utamaduni wa kihaya. Kwa hiyo kusema kiswahili kinadumisha utamaduni wetu ni UONGO. Hakuna utamaduni ulio uniform kwa wa Tanzania wote. Nchi nyingi huwa zinakuwa na lugha kuu zaidi ya moja. Tanzania, english ni lugha ya pili na ni muhimu sana kuimudu. Tumeyaona huku U.S. ambapo wa Tanzania wanashindwa kuongea makazini, mpaka wana acha kazi kwa sababu english yao ni poor. Wa Tanzania wamekalia kuendekeza kiswahili kila mahali, kila wakati, kiasi kwamba english inakuwa tatizo na huku U.S. bila kuongea english kila kitu kinakuwa kigumu. Shuleni ni english, vitabu viko kwenye english, madukani ni english, kazini ni english, bank ni english, hospitali ni english. Amini usiamini, english ni muhimu sana sana. Mimi nina mtoto amezaliwa hapa U.S., waswahili wanaoishi huku wananiambia kwa nini simfundishi kiswahili. Mimi nawaambia mtoto wangu ni raia wa Marekani kwa kuzaliwa, na hicho kiswahili atakiongea na nani wakati nchi nzima inaongea english. Inabidi tuwe realistic. Kiswahili kilitusaidia kutuunganisha kujiona wote ni wa Tanzania, lakini technically speaking, unapotaka kuwa competitive globally,kiswahili hakina nafasi. Wake up folks!
ReplyDeletewewe uliyesema Tanzania ina lugaha mbili za taifa!mimi nina wasiwasi kama unauelewa au umeropoka tuu!Lugha ya Taifa ya Tanzania ni kiswahili tuu,kiingereza sio lugha ya taifa it's official language tuu!dont miss lead people please!
ReplyDeleteNdugu waziri umesahau haya yafuatayo:
ReplyDeleteMagazeti yote yatolewe kwa lugha ya Kiswahili.
Habari zote kwenye blog za kibongo na comments zake zitolewe kwa lugha ya Kiswahili.
Kuna mtu anabisha?
VIPI NABII MASHAKA?
ReplyDeleteNimeipenda sana ile hoja kwamba usaili ufanyike kwa Kiswahili. Kuna vitu adimu nilikuwa nashindwa kuwasilisha kwa sababu ya kiinglishi.
ReplyDeleteSasa nimepata nafasi ya kujieleza vizuri kwenye usaili kwa mbwembwe zote za Kiswahili.
Hoja imekuja muda muafaka.
Mwaka wa uchaguzi huu...maagizo kede kede.
ReplyDeleteSafi sana! ndio tunajiandaa kuingia ist afrika ya mashariki. unataka kazi zetu, ongea kiswahili.
ReplyDeleteumeshasikia tena anko, hapa pasiletwe tena kiingilishi!!!
ReplyDeleteumeshasikia tena anko, hapa pasiletwe tena kiingilishi!!!
ReplyDeletemdau wa Tue Apr 20, 04:17:00 PM, whats your point? au ndio unataka kujinyesha ya kuwa uko usa? unataka kutwambia kuwa huko uliko sheria zimeandikwa kwa english ya spanish? unataka kutwambia kuwa viongozi wa serikali huko wanatowa hutuba kwa kispanish?
ReplyDeletewacha kurukia mambo tu na kujifanya unajuwa kila kitu, si angalau basi ungelisoma taarifa yote kabla ya kuleta maoni yasio ya kweli hapa?
Tue Apr 20, 04:17:00 PM
ReplyDeletetehe tehe eti kuanzia leo bungeni na sehemu nyingine zianze kutumia kiswahili hehhehe kwani hapo mwanzo mlikuwa mnaongea lugha gani?naona hakuna badiliko lolote kama kiingereza hamjua kuanzia mzee mpaka chini kwa watoto,msituletee za kuleta....subiri sasa utone mkienda huko kuomba misaada kwa wakubwa nawaita wakubwa maana mtu mzima mwenyewe baba anawaita wakubwa alishawahi kusema "naenda kwa wakubwa"...tz kushnei
ReplyDeleteEXCUSES KILA SIKU BADALA YA KULETA MAMBO YA MAANA.
ReplyDeleteBASI NA MASOMO YA CGUO KIKUU YAWE KWA KISWAHILI.
SERIKALI HII INASHINDWA HATA KUSAMBAZA VITABU VYA KUTOSHA LEO WANADAI WANATAKA KISWAHILI.
baada ya kuona mheshimiwa inglisi haipandi analazimisha watu wabonge swahili, lol
ReplyDeleteMdau wa 5:33 sijawahi kusikia eti kiswahili kina very poor vocabulary. Hiyo ni kuthamini vya wenzako na kudharau vyako. Unavotaka ni kujaribu kulazimisha maneno ya kiingereza yawe na maana ya kiswahili. Kwani maneno ya kiswahili yote yana tafsiri ya kiingereza?
ReplyDeleteEti wewe unaona fahari sana kuwa mwanao amezaliwa Marekani kwa hivyo humfunzi kiswahili. Ndugu yangu hujiamini ndio maana. Kujua lugha zaidi ya moja kunampa huyo mwanao nafasi kubwa na upeo mkubwa zaidi.
MDHARAU KWAO........
Wajinga ndio waliwao!!
ReplyDeleteWatoto wa mawaziri wanasoma ng'ambo ambako hata kiswahili hakitambuliki, baba zao Bongo wako mstari wambele kuwadumaza watanzania wabaki kupata elimu kwa kiswahili. Matokeo yake wajanja wachache wanaojuwa kimombo kwa kusomeshwa nchi za nje wanapewa nafasi za juu na jukumu la kutia sahihi mikataba iliyoandikwa na wawekezaji akina YES YES MZUNGU KALA MAFENESI. Mimi na wenzangu akina Shabani Gonga na Mzee Bao wa shule ya Juma na Roza tunabaki kuambulia moshi wa Buzwagi, EPA na Richmond!!
bungeni tu kunawashinda kuongea kiswahili,sembuse ilo???jana kuna m-mama mbunge sijui alikua anatoa taarifa fulani bungeni JAMANI?!adi nilibadili channel maana uozo mtupu yaani anavochanganya lugha utafikiri kachumbari mara kiinglish mara kiswahili,,sasa sijui umma wa wabongo walio wengi ulimuelewa?nilisikitika sana,,,eti WABUNGE WAMESAHAU KISWAHILI ovyo kabisa,,,acha zenu wacha tuongee lugha yoyoote tu ilmradi ujumbe unafika
ReplyDeleteviongozi wamechanganyikiwa
@Mdau wa USA. Lugha inakuwa kwa kuongewa na si kwa kuinyanyapaa. Kuinyanyapaa ni kuidumaza. Lugha zote huazima maneno kutoka lugha nyingine pale inapobidi. Kwa wale wanaoongea lugha yoyote iliyozaliwa toka kwenye Kilatini (Kihispania, Kireno, Kiromania, Kiitaliano, Kifaransa) watakubaliana nami kuwa Kiingereza chenyewe kimeazima maneno mengi mno kutoka Kilatini. Lakini kwa vile wewe unajua Kiingereza na Kiswahili tu unafikiri maneno yote unayojua ya Kiingereza basi asili yake ni Kiingereza chenyewe! La hasha. Kwa wale waliosoma sheria na udaktari watakubaliana nami kuwa lugha inayotuma katika fani hizo kimsingi ni Kilatini (japo watu husema yanafundishwa katika Kiingereza). Kiswahili pia chaweza kuazima kutoka lugha nyingine.
ReplyDeleteHilo wazo ni zuri sana kwa upande wangu kwani asili mia kubwa ya watanzania hawaongei kiingereza kwahiyo iwapo bunge litakuwa linazungumza kiswahili itawasaidia mabibi na mababu zetu kuelewa kila linalosemwa bungeni. Kwa nyongeza ikiwa mtu ana haja ya kujua kiingereza au lugha yoyote ile ya kigeni basi ana ruhsa ya kujifundisha kwa wakati wake.
ReplyDeletesawa sawa mheshimiwa kimatumbwi juu juu zaidi.maana nchi ka japan danemark norway france sweden holland ujerumani wanaziendeleza lugha zao za taifa hicho kimombo mtoto anasoma akiwa sekondari kama lugha ya ziada.so wao ukiwa mgeni umeeenda kukaa huko kwao lazima uongeee lugha yao asili si kimombo.mh dumisha mila mgeni akija boxini tz na atakaa zaidi ya miezi sita kusoma kimatumbwi kwanza kabla hajapewa kibari cha kuishi bongo africa.
ReplyDeletemdau mbere kwa mbere
HAJASEMA KUWA KIINGEREZA KISIFUNDISHWE TENA MASHULENI, AMESEMA SHUGHULI ZA KITANZANIA ZINAZOFANYIKA TANZANIA ZIFANYIKE KWA KISWAHILI, WANAFUNZI WATAENDELEA KUJIFUNZA LUGHA NYINGINE MASHULENI KAMA SOMO IKIWEMBO NA HIYO ENGLISH, WACHINA WAJAPAN NA NCHI NYINGINE SHUGHULI ZAO HUFANYIKA KIKWAO NA ENGLISH WANAJIFUNZA KAMA SOMO MADARASANI WANAONGEA PALE WANAPOHITAJI KUIONGEA AMA WAKIENDA KWENYE NCHI ZA WATU WANAOTUMIA ENGLISH AU WAKIFANYA BIASHARA NA WATU WANAOONGEA ENGLISH. KUTUMIA KISWAHILI KATIKA SHUGHULI ZETU HAKUTATUFANYA TUSIJUWE ENGLISH. THE WAY TU-MASTER PHYSICS NI THE SAME WAY TUTA-MASTER LUGHA ZA KIGENI. ACHENI KUWAKUMBATIA WA-INGEREZA NI WASHEZI TU KWANZA HAWATUTAKI MAKWAO NI WABAGUZI SANA NA WANA DHARAU SANA
ReplyDeletecommon sense is how comes college and university graduates taught in english gonna be able to speak fluent swahili while interviewed coz its very difficult to flow in swahili to reference what you were taught at school,thats why you see people mix-up swahili and english while trying to explain something and this tells that there's a huge problem as far as communication is concerned in Tanzania.Lets our leaders be realistic,decision should be made to opt a use of one of these 2 languages in all levels of education,business and government institutions and agencies as there will always be problems somewhere in communication if we continue the use of 2 languages in academic secta.In Kenya forestance they use only english as a medium of instruction from kindergaten to university level this eliminates alot of confusions to students as we have seen on tanzanians.Theres no way a child that is taught in swahili for nine(9) yrs to be able to successfully switch to english language with no confusion.So Folks lets be realistic and thats only what we need in order to solve this communication mess we are into.
ReplyDeletemimi nipo hapa NOrth America ni kwamba jamaa wa huku wanaifagilia sana lugha ya kiswahili wanasema Tanzania ina lugha yao wenyewe tena ni ya kimataifa yaani Kiswahili!!
ReplyDeletekwa kweli ni jambo la kujivunia!!!
Badilisha na TBC inatuaibisha.
ReplyDeleteRudisha RTD & TVT hamuoni huo ndio utumwa?
Au ndio homa ya uchaguzi? Tutaonana oktoba
Heri yenu wadau mlio huko USA na kubahatika kuongea kiingereza kwa ufasaha. Lugha ukiijua utaongea tu bila hata kufikiria usemeje hakuna hata atakae kuongoza maneno yatakuja yenyewe. Sisi tuliowengi huku si kosa letu kutojua kuongea English kwa ufasaha. Hebu fikiria shule ina walimu watatu hao hao wafundishe kila somo. Mtu hata ukifanikiwa kufaulu kwa kipaji alichokupa Mungu lugha hio utajua kusoma na labda kuandika kiasi tu. Kuongea utajulia wapi wakati hukuwa unaiongea i.e. umefundishwa kusoma na kutamka. Si kwamba watu hawataki kujua. Mbona lugha za makabila watu wanazijua tena zingine ni ngumu zaidi ya hio English? Kila lugha ukikua unaitumia kwa maongezi utaimudu tu. Hapa TZ sehemu ya kwanza tuliowengi tunayoenda kukutana na English ni shule ya Msingi. Walimu hakuna hivyo ni ngumu sana kuwalazimisha watu waongee kiingereza kazini wakati huku kwenye msingi hakuna walimu wa kutosha. Ni kumnyima mtu nafasi ya kujieleza kwa kosa lisilo lake. Fikiria kama wewe ni Mfipa halafu anakuja mtu anakufanyia usaili kwa Kimasai eti umejifunza kwa kudonoadonoa tu pale shule utajieleza kitu cha maana kweli? Uamuzi mwingine hata kama unaathari zake kimataifa lakini unatokana na hali halisi. Tanzania shule ziko nyingi sana lakini walimu wa hicho kingereza kweli ni wachache mno. Kurekebisha ni kuaandaa walimu wengi wanaomudu kiingereza kama ilivyokuwa miaka ya zamani, watu watajua tu. Mbona waliobahatika kusoma hizo English Medium wanazungumza vizuri tu.
ReplyDeletewagosi wa kaya waliwahi kusema ,kiingereza chenyewe ni cha ugoko..!
ReplyDeletepamoja na kufurahia kusikia kuwa lugha ya kimatumbi inakuwa juu juu zaidi...ila pia ninafikiri wasingebana sana hii lugha ya kiingereza kwani ni lugha ya KIBIASHARA zaidi ,nafikiri wakuu mmenisoma.
tukirudi mashuleni ni balaa..
fiziksi au hesabu na kemia ukiachia baioloji kufundishwa kwa lugha ya kiswaswa hahha..kazi itakuwepo! lazima wanafunzi watoke nduki..tupo hapa.
ushauri:
KWA SERIKALI YETU:
Kabla ya kufanya uamuzi mkubwa kama huu,wangekuwa wanaihusisha jamii yenyewe kuliko kukurupuka watu watatu tu.kumbukeni kuwa wengi wa wabunge wa bunge letu vyeti vyao ni vya kughushi..ndio kusema Yes,no.. kibao zinawapiga chenga.EAC inawajia, wakenya, kati ya magrupu 3, moja linaongea kiinglishi tupu,lingine kiinglish na kiswahili,la mwisho ni kiswahili tupu.unategemea watakuwawapi kwenye mtafaruku wa kuomba kazi ..kudadeki...wabongo wote vijijini kulima,hatimaye,wakikuyu wanakaa mjini.
big losers!! mimi nashauri tungechanganya.mambo ya matangazo,mitaa na vitu vingine viwe kwa lugha zote..jamani mbona nchi nyingine ni hivyo!!? bongo kwa kukurupuka!!! wanashindwa kukurupuka kuwakamata mafisadi wanakurupuka kuharibu mambo tu!!
moody
Nasubiri marekebisho ya yafuatayo:
ReplyDelete1. TBC
2. Taifa Stars
3. Serengeti Boys
4. Ngorongoro Heros
5. Taifa Queens
6. TFF
7. Daily News & Sunday News
8. TANAPA, TRL, TANESCO, DAWASCO
Bora waliojigundulia mapema kama:
SHIMIWI,SHIMUTA, UMISETA, UMISHUMTA, MKUKUTA, MKURABITA, MKUZA, MMEM (Hapa namkumbuka Mungai) na kazalika.Ila usaili kwa kimatumbi itakuwa raha maana tutaishia kuulizana habari za nyumbani tu kwakuwa hata interviewer mwenyewe hajui aulize nini!!!
@Mdau wa USA. Hata mimi nimekaa USA (New York + Miami). Kwa sasa niko Ulaya. Marekani wenyewe wanasema lugha yao ni Kiingereza si Spanish. Kuna wanasiasa wanataka sheria ya kusema hivyo ipitishwe. Hata Kiingereza kiko tofauti. British accent(s) ni tofauti na US accent. Tofauti ni nyingi mno: USA vs Australian, Australian vs Canadan. Mjamaika akiongea Mwingereza anaweza asielewe kabisa. Nk nk
ReplyDeleteHata katika nchi moja kama Uingereza, BBC English (aka Queen's English, Received pronunciation) ni tofauti na Scottish. Hivyo hivyo na USA. Kwa hiyo hoja yako ya makabila na Kiswahili cha Pemba vs Kiswahili cha Kigoma haina nguvu yoyote.
nchi kama uingereza inatumia lugha yake kwani haimtegemei mtu yeyote kwa msaada na inajitimizia mambo yake. mjerumani anaongea kijerumani peke yake kwani haitaji msaada wa mtu . mspanishi hivo hivo. n mafaransa pia nae hana haja ya kuongea lugha ya mtu mwingine SASA NYINYI WATANZANIA MANALAZIMISHA KUONGEA KISWAHILI JE MNAJITEGEMEA NINI? JE MTALIAJE NJAA ZENU ZA MISAADA KWA WAZUNGU? AMBAYO MNAILILIA KILA SIKU? JE MTAFANYA VIPI BIASHARA ZA NJE? NAMKIUGUA WAKATI MNALETWA NJE MTAONGEAJE? AU NA NYINYI MNAJITEGEMEA KAMA NCHI ZILIZOENDELEA ? MNATENGENEZA MAGARI NA KADHALIKA WENYEWE? AAHAA JIULIZENI YOTE HAYA. ACHENI KURUDISHA NCHI NYUMA KWA UJINGA WENU WA KUSHINDWA KUONGEA KIINGEREZA. MBONA WAZUNGU MMEWAUZIA MABENKI KAMA NBC NA MENGINEYO. WATUMWA NDANI YA NCHI YENU. SOO SAD. NO WONDER WHY WAMEJAZANA BONGO. EASY TARGET COUNRTY. SOOO SILLY..na je watoto wenu mnaowapeleka international school huko bongo itakuwaje?? maana nikama fashion kupeleka shule za kiingereza. shame on u all who supportmambo ya kiswahili. human rights watu wachague lugha wanayoitaka kuongea wenyewe na watoto wao. msipumbaze wananchi.badilini kila kitu mabenki, matangazo na maongezi yenu bungeni kwanza. ndio maana viongozi wa serikali wanatia aibu wakija nchi za nje hawawezi kujielezea.
ReplyDeleteWABUNGE ACHENI HIZO, NCHI YETU TANZANIA TUNAIPENDA LAKINI MNAIPELEKA KI-BEACH BEACH, KAMA MMEZEEKA TUACHIENI NCHI YETU MPUMZIKE, EBU PAMBANENI NA UFISADI, MADA YA LUGHA MMEISHIDWA . ENGLISH NI GLOBAL LANGUAGE, YOU NEED PROPER DECISION MAKING TO ALTER THE LANGUAGE. THIS IS COMPUTER AGE NYIE NA SIO STONE AGE OK, TANZANIAN TUSEMA NO.
ReplyDeletehii ni kali, hauwezi kuniambia umefanya nondozz kwa kiingereza then uelezee kwa kiswahili nadhani hapo wamepotea hawa na kiswahili chetu.
ReplyDeletetunachojaribu kufanya ni kuiga nchi ambazo vimeendelee kwa kutumia lugha zao lakini ukweli ni kwamba hao watu kwa sasa wanahaha maana hawawezi kujitambulisha kimataifa.
chukulia nchi kama south korea kwa sasa inatumia pesa nyingi sana kujifunza kiingereza kwa sababu wanabidhaa na hawawezi kujibrand kwa lugha tofauti na kikorea. elimu yake iko juu kiasi ila international wise wachache wanao weza kusoma huku maana hadi hicho kiwe juu.
TUTUMIE HII NYENZO YA JAMII KUJUA KIINGEREZA KWA KUJILETEA MAENDELEO TUKICHANGANYA NA KISWAHILI CHETU KIAMA ILIVYO SASA.
Kiswahili oyeeeeeeeeeee. Kama hutaki hama nchi.
ReplyDelete.......Ankal mtu anaposema tuwe "competitive globally" ana maana gani? hao Globally nahitaji kushindana nao nini? wageni wengi wanaokuja Bongo wanapashida sana kufanikisha mambo yao. Maana lazima wao waseme kiswahili. Huduma zote za nje zinapaswa kuletwa Bongo wahusika wanahangaika ziwasilishwe kwa kiswahili.Nimeshuhudia Profesa yuko kwenye LECTURE ( KISWAHILI INAITWAJE...VILE?)alipoona watu hawelewi akaomba ufanyike ufafanuzi kwa kiswahili kwa wale wasio elewa! Globally yule mwenye shida atamfuata mwenzie....hivi warusi, wachina, wakorea, watasliani, waturuki, wa Iran wa Pakistan, maendeleo wamepata na wanatoa ushindani Duniani wametumia Lugha gani! tuna kasumba kama tumedhurika na madawa ya kulevya "mateja ya Kiinglish!"
ReplyDeleteYees I support Kiswahili but this is a political decision.
ReplyDeleteOK je Serikali yenyewe imeshabadilisha sheria, Kanuni, taratibu, Sera na nyaraka zake zote ikiwemo Website ya Serikali na hata Ikulu kwenda kwa kiswahili. If Yes hakuna neno. If NO namshauri Mkuchika a-keep quiet kwa sababu hakuna jipya hapo.
C.V kwa kiswahili sanifu inaitwaje?
ReplyDeleteWABUNGE NDIO NAMBA MOJA WA KUONGEA ENGLISH
ReplyDeleteNina msupport anony wa April 21, 12:26 pm. Kiswahili sio deal kabisa. Kwani ukushapanda ndege pale Dar, ujue ukitua Amsterdam au London au U.S. au popote pale duniani, sahau kiswahili chako. Wewe Kali Kali nieleze ni wapi duniani ukiacha Tanzania umekwenda ukakuta signs zimeandikwa kwa kiswahili? Kama ukiwa airport unatafuta gate lako au unachukua mzigo wako. Ni owner's manual ngapi zipo kwenye kiswahili? Kwa nini hapo hapo TZ kwenye colleges text books almost zote ziko kwenye english? Viongozi wenu wenyewe wakija kiwanja hawawezi kuongea english, wakati wanatoka kwenye english speaking nation. Hapa U.S., kuna wa Tanzania kibao wanakosa kazi au wanafukuzwa kazi kwa sababu hawawezi kuongea english. Mtu toka darasa la tatu anajifunza english lakini hayuko fluent. Sisi tuliobahatika kuwa na watoto huku U.S., kuna haja gani ya kumshindilia mtoto na kiswahili wakati hatakitumia? Akienda shule, mtoto wangu anaongea english, akicheza nje na wenzake ni english, akienda dukani ni english, vitabu vya shuleni ni english, simu ikipigwa ni english, akigombana na watoto wenzake wanagombana na kubishana kwa english. Sasa nieleze ni wapi atakiongea kiswahili? Na mtoto wangu sitampeleka Tanzania kuishi, kwa sababu sitaki afike huko apate malaria na kipindipindu, na anyanyaswe na fujo za dala dala kukataa wanafunzi, na kupigwa viboko shuleni na walimu. Hapa U.S. mwalimu mwiko kumgusa mtoto, ni child abuse. Alafu wewe Kali Kali kiswahili hakisaidii utamaduni wa ki Tanzania, kwa sababu hakuna utamaduni ambao ni UNIFORM kwa Tanzania nzima. Ndio maana nikatoa mfano wa wamakonde na wahaya. Ni makabila mawili tofauti, na kila kabila lina utamaduni wake. Kwa mantiki hiyo hiyo, makabila zaidi ya 100, hayawezi yakawa na utamaduni UNIFORM. Na kwa mantiki hiyo hiyo, hakuna utamaduni mmoja wa Tanzania. Kiswahili kimifanikiwa kutuunganisha kujiona wamoja kama taifa, lakini kubali kwamba ni lugha changa mno, with very limited vocabulary. Usijidanganye na kusikia kwamba kuna watu nchi za nje wanajifunza kiswahili, watu hao hapa U.S. tunajua kwa nini wanafanya hivyo. Ni kwa sababu ni easy credit hours. Kama mtu anaweza kupata credit hours 6 au 9 kwa kujifunza kiswahili, why not? Anaongeza credit hours zake halafu shule yake inaisha kilaini, kuliko mtu mwingine anayeng'ang'nia physics, au chemistry, au biology ambazo zinamshinda. Tatizo wa Tanzania wengi hawajagundua kwamba ili waweze ku compete globally, inabidi wawe fluent in english. Imagine umeitwa kwenye interview na kampuni kama General Electric halafu huwezi ku form sentence au kujibu maswali. Unafikiri watakupa kazi hata kama una master's ya engineering? Kalikali fungua macho brother. Hichi kiswahili unachokipenda sana hakina nafasi kama unavyofikiria. Tembea uone.
ReplyDeleteAnd then mnalalama kwamba wakenya wanawachukulia kazi zenu....SHWAINIESSSSS!
ReplyDelete@ Wed Apr 21, 04:47:00 PM:
ReplyDeleteNinapokipigia Kiswahili chepeo si kwamba siongei Kiingereza. Naongea vizuri na States nimekaa. Naongea Kisukuma pia. Naweza kuwasiliana kwa Kichina pia (siyo fluently lakini maji naweza kuomba). Kwa sasa niko Hispania. Najifunza Kihispania sasa. Hata hivyo Kiswahili bado ni namba moja kwangu. Kwa hiyo usifikiri kukaa US na Kiingereza cha US (ambacho ni "Old English" ya UK) ni deal kubwa. Nikiwa Tz naongea Kiswahili. Nikiwa US naongea Kiingereza. Nikiwa China naongea Kichina. Usukumani - Kisukuma. Kwa sasa niko Spain - hawaongei Kiingereza au Kiswahili hapa - naongea Kihispania. Tatizo lako ni kulazimisha Watanzania kuongea Kiingereza. Watanzania wanatakiwa kujifunza Kiingereza kwa ajili ya matumizi ya nje ya nchi tu. Viongozi wetu kutokuongea Kiingereza wewe unaona nooooma. Ni sawa na kushangaa Wazungu kutokuongea Kiswahili. Hu Jintao (China), Hatayama (Japan)nk nk anakwenda kwa Obama na wakalimani na hakuna kinachoharibika. Tena viongozi wetu wakitumia Kiswahili ugenini kupitia wakalimani itakiongezea Kiswahili soko nje ya nchi.
Tuache utumwa wa akili.