Ankal,
Lipo swali lililoulizwa na mdau mmoja kuhusu 'ukataji kimeo kwa watoto' (kama linavyosomeka hapo chini), nililifikisha kwa wadau wa sekta ya afya na mmoja wa wahusika, Dk. N. Mkopi aliyepo katika kitengo cha Magonjwa ya Watoto katika hospitali ya Taifa Muhimbili alilitolea ufafanuzi kama inavyosomeka hapo chini.
Subi
www.wavuti.com
-------------------------
Kimeo ni nini?
Kimeo ni sehemu ndogo ya kinywa inayoning’inia mkabala na mwisho wa ulimi. Hivyo kila mtu huzaliwa na kimeo na kimeo sio ugonjwa.

Kazi ya kimeo ni ipi?
Husaidia kinga ya mwili
Husaidia kulainisha koo
Husaidia kutoa sauti.

Je kwanini watu wengi wanakata kimeo?
Kutokana na elimu potovu juu ya kimeo; mfano: Kimeo kimevimba na kikipasuka tu mtoto ndo anakufa, Kimeo kina usaha, Kimeo ni kirefu sana. n.k.

Watu wengine hufikiri kuwa kimeo kinasababisha magonjwa kama vile:- Kukohoa muda mrefu, au Kukonda au Kutapika mara kwa mara au Mtoto kulialia bila sababu. Hii si kweli.

Je ni sahihi kukata kimeo?
HAPANA! Kimeo hakipaswikukatwa kutokana na sababu yeyote ile!

Nini madhara ya ukataji wa kimeo?
Mtoto anaweza kupoteza damu nyingi na kupoteza maisha Maambukizi ya magonjwa mbalimbali kutokana na kutumia vyombo ambavyo si salama kukatia kimeo; mfano:- Pepopunda, Homa ya mapafu, Maambukizi ya VVU, Mototo kupata maumivu makali au Kupaliwa na chakula kupitia puani.

Tufanyeje/Jitihada gani zifanyike ili kuzuia madhara haya yasitokee?
Watoto wanao kohoa muda mrefu, wasiokua vizuri, wanaotapika mara kwa mara, n.k. wapelekwe kwa daktari kwa ajili ya uchunguzi na tiba mbadala!

Dk. Namala Mkopi
MNH - Kitengo cha Watoto
2010/4/16 Subi

Linki:
http://issamichuzi.blogspot.com/2010/04/msaada-tutani_16.html

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. VITU KAMA HIVI NDIO VINATAKIWA KUWEKWA BLOGU YA JAMII HUMU WADAU WAPATE KUSOMA ILI WATOTO WAO WASIJE KUWAKATA, SIO WENGINE WANAKUJA NA TOPIC ZA SWALI LA KIZUSHI. VITU KAMA HIVI NDIO VYA KUWEKA JAMII IJIKINGE. ASANTE MDAU KWAKUWEKA HII. SEIF.

    ReplyDelete
  2. MicrobiologistApril 22, 2010

    Maelezo ya Dr ni sahihi kwa kwa sehemu na si sahihi kwa sehemu. Ni kweli kimeo kama kimeo (Uvula) hakihusiani na kukohoa wala hakihitajiki kukatwa. Lakini kimeo kiko very vulnerable kwa infection na hivyo hupelekea ku swell, kiki swell sababu ya infection huweza hata kupelekea kufanya usaha (pus) wakati mwengine kina fanya kioteo sababu ya hiyo infection, hicho kioteo ndicho kinacho pelekea kikohozi sababu kina habour virus na bacteria kama vile streptococcus pneumoniae na wengine wanaopelekea kikohozi, hichi kioteo huwa mara nyingi hakipotei kwa treatment za kawaida, hadi kikatwe (uvulectomy)! Ukataje huo wa kimeo tumezoea kuufanya kienyeji (sishauri iwe inafanyika hivyo, kwa kuzingatia mazingira hatarishi ya HIV, pia uwezekano wa kupelekea magonjwa mengine ya infectio kutokana na mazingira husika), ningeshauri wagonjwa wa vimeo wapelekwe hospital wakapate matibabu katika mazingira mazuri. Lakini mara nyingi ugonjwa wa kimeo huchanganywa na epiglotittis ambayo nayo pia treatment yake ni sugery na dalili zake ni kama hizo za kimeo, ila hii epiglotittis ni hatari zaidi kwani hu grow hadi kuzuia upumuaji wa kawaida hivyo mgonjwa kukosa hewa na hatimae kufa!

    Scientist (microbiologist)

    ReplyDelete
    Replies
    1. Naomba mawasiliano yako kaka unisaidie juu ya hili jambo

      Delete
  3. Mimi sio daktari lakini majibu ya daktari naona si sahihi kutokana na uzoefu wa mazingira ya watoto wanaopata vimeo. Watoto wanaopata vimeo wakikatwa huwa anapata nafuu na kupona kabisa ndani ya siku chache na hata mimi nilikatwa kimeo nikiwa mdogo ila tu angalizo hapo ni kwamba mazingira ya ukataji ni ya kienyeji na yanaweza kusababisha maambukizi.

    Labda Daktari pia atuambie instead of kukata kimeo kinatibiwaje endapo utaenda Hospitali maana mimi nilivyomuelewa inaonekana kimeo kama sio ugonjwa lakini mbona watoto wanateseka na kupata homa sana?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...