http://www.listerelia.com/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mr.Lister
    Mimi nakukubali kuwa wewe ni mtaalamu au wamlimu wa ufundi wa mziki,ambaye unaweza kuwaelimisha wanamziki wengine kiufundi wa mziki.
    Lakini kibiashara ya mziki bado kidogo sikubaliani nawe ktk baadhi ya maoni yako,kuwa mwanamziki wa Tanzania hili hawe wa kimataifa lazima awe na uzoefu wa kupiga miziki tofouti kama vile Jazz nk?apo kidogo umechemsha .
    Mtazamo wangu:mwanamziki ili awe mwanamziki wa kimataifa kwanza hawe na Sifa zifutazo(a)Awe mwenye kujihamini (self confidence)
    (b) lazima akubali kukusolewa na kusoma kutoka kwa wengine pamoja na kuelewa au kujielewa washabiki wake wanataka kitu gani? au rhythm gani?
    (c)Hasiwe mwenye kuyumba yumba kimsimamo,lazima awe na msimamo wa aina gani? mziki anautangaza.
    Nakubali ana na wewe katika lugha wanamziki wetu wajaribu kujisome au kujiendeleza katika kujua lugha za kimataifa kwa ajili ya mawasilianao na kuthibiti masoko ya kimataifa.
    mkuu maoni yangu hayana nia mbaya au ukosoaji bali ujengaji,ili tuweze kusonga mbele.
    tupo pamoja.
    wako
    Bw.Kidaka Tonge

    ReplyDelete
  2. NAKUBALIANA NA KIDAKA TONGE KWA ASILIMIA ELUFU MOJA. KUNA TOFAUTI YA KUWA MWANAMUZIKI KWA MAANA YA MBURUDISHAJI NA MJUZI WA MUZIKI KWA MAANA YA KUWA UMEUSOMEA NA UNAUELEWA FIKA (HAPA NDIPO ANAANGUKIA BWANA LISTER ELIA).

    KUWA MWANAMUZIKI MBURUDISHAJI NI KIPAJI PENGINE WALA HAKIHITAJI KUSOMEA KWENDA SHULE, KWA MFANO MZURI NI FAMILIA YA AKINA MICHAEL JACKSON NI KIPAJI KILICHOWAPELEKA HAPO WALIPOFIKIA KAMA WALISOMEA BASI NI BAADAYE SANA.

    BWANA LISTER ELIA ANAFAA KUWA MWALIMU MFUNDISHAJI SI MWANAMUZIKI, NIMEENDA KWENYE TOVUTI YAKE NA KUSIKILIZA MIZIKI YAKE YOTE HAIWEZI KUPATA SOKO MAHALA POPOTE DUNIANI HATA TANZANIA, HAINA ILE HALI YA KUBURUDISHA, NI NASAHA TU AMBAZO NI KAMA KUSOMA KITABU.

    YEYE SI MWANAMUZI NA WALA SI CREATIVE.

    NAKUBALIANA NAYE TU KUWA ANAWEZA KUFUNDISHA MUSIC (TECHNICAL STUFF) LAKINI KUMTENGENEZA MBURUDISHAJI HAWEZI, ANATAKIWA KUELEWA KATI YA KUWA MWANAMUZIKI NA MJUZI WA MUZIKI, SAWA NA MWALIMU ANAWEZA KUFUNDISHA WATU WAKATOKEA KUWA MAMENEJA WAZURI LAKINI HAINA MAANA MWALIMU HUYO ANAWEZA KUWA MENEJA MZURI.

    JAMANI NENDENI KWENYE TOFUTI YAKE NA MSIKILIZE NYIMBO ZAKE, HAMNA HATA MOJA ITAINGIA KWENYE CHATI YOYOTE DUNIANI ACHA YA TANZANIA

    ReplyDelete
  3. Sasa wewe Anonym wa kwanza,Lister ameeleza sifa mbili tu kati ya sifa nyingi ambazo zinahitajiwa.Hizo sifa ulizosema wewe kama vile self confidence ni za kawaida kwani kama huna self confidence huwezi kaunza chochote.Acheni umbea jamani,kama mtu ni skilled kama Lister mpeni "Big Ups".Asante Listeryou are skilled and humble brother.God bless you.

    ReplyDelete
  4. wewe Anonym wa Tatu: Umekurupuka tu bila ya kumwelewa Anony wa kwanza! kwa mwanadamu yeyote yule ambaye anataka awepo katika uringo wa kitaifa au kimataifa,awe kwenye biashara yao hii ya mziki na sanaa,au siasa au biashara yoyote ile inayaousu washabiki au wingi wa wateja,mtu huyu ili afanikiwe lazima kwanza awe ANAJIAMINI yaani (self confidence) hii ndio nguzo ya kwanza,harafu ndizo hizo sifa zingine.
    Franco Luambo(RIP) hakuwa mwanamziki mwimbaji mzuri kushinda Tabu ley,bali franco alikuwa anajiamini na kuwavuta watu upande wake.
    Bob Marley hakuwa mwimbaji mzuri zaidi Jimmy Clif ! bali alikuwa anajiamini na kuto kuyumba mara kabiga mtindo huu kesho ule hapana.
    Self Confidence ndio roho ya msanii,mwanamichezo,mwanasiasa,mfanyibiashara,hata mwanafunzi bilia ya kujiamini ni sawa na 0+0=0.
    Sidhani kama maoni ya KIDAKA TONGE
    yanamvunjia heshima Lister hapana,bali yana sisitiza na kuongeza uzito

    ReplyDelete
  5. Hiyo mifano ya mchangiaji kwamba ya mwanamuziki fulani hakuwa na mafanikio kulinganisha mwingine sababu ya 'self confidence' haina mantiki. Umefanya utafiti gani wa mafaninio yao kwa kipengele hiki? Luambo na Tabu Ley kila mmoja alikuwa na washabiki wake, kama simba na yanga.Bob Marley na Jimmy Cliff aina za mziki wao hazikufanana sana. Labda Bob Marley na Peter Tosh? Ingawa confidence inahitajika kwa mambo mengi maishani ni vigumu kulinganisha mafanikio ya musicians kwa kipengele hicho. Kwa hiyo, mifano uliyotoa si sahihi. Hongera Lister na endelea kupeperusha bendera.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...