kassim manara akichachafya enzi hizo. yeye ndiye mdogo katika familia ya soka ya manara, ambapo wote walijaaliwa vipaji vya hali ya juu katika uchezaji na hadi sasa hakuna ukoo uliotoa nyota wengi kwa mpigo kama kina manara. Kassim alichezea Yanga kabla ya kuhamia Pan African na baadaye kwenda ughaibuni ambako yuko hii leo ila kwa sasa kastaafu.
Sunday Manara akikata mbuga. Huyu alipewa jina la Kompyuta kwa uwezo wake. Kumbukumbu zinaonesha yeye ndiye mwanasoka wa kwanza kwenda kucheza soka la kulipwa ughaibuni kwa mafanikio makubwa. Hivi sasa amestaafu na yupo nyumbani

Kitwana Manara 'Popat' alianza kama golikipia kabla ya kuamua kuwa mshambuliaji ambapo alitisha sana katika umaliziaji hasa kwa vichwa. Yeye pia amestaafu na anajishughulisha na siasa akiwa diwani na pia mmoja wa washauri kwa shirikisho la soka TFF



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. "Ukoo ulitoa nyota wengi kwa mpigo"
    Hii fact sio sawa maana kuna ukoo wa kina Kihwelo

    1. Mussa
    2. Jamhuri
    3. Muhesa
    4. Mwanamtwa

    ReplyDelete
  2. Kuna huu ukoo wa kina Kiwelo, nafikiri nao walikuwa wengi sana kwenye "premier league" ya Tanzania. Ninaoweza kuwakumbuka kwa sasa ni Musa, Jamuhuri, Muhesa, Mwanamtwa. Kama Ankal unaweza kutusaidia kujua kwa sasa wako wapi tutashukuru.

    ReplyDelete
  3. Hebu waweke hapa akina Njohole ukianzia na Nico halafu ndio uangalie wapi walikuwa wengi. Umalisie na akina Kihwelu.

    ReplyDelete
  4. what>>> nani kama manara??? manuuuu!!

    ReplyDelete
  5. Vilevile wapo wakina MWakatika kama mtakumbuka

    Joram Mwakatika
    Julius Mwakatika
    Isaac Mwakatika

    ReplyDelete
  6. Baba UbayaApril 25, 2010

    hapa cjaelewa kidogo.wadau mnazungumzia wingi au umahiri?yani ukoo uliowika zaidi ktk kusakata soka la Tanzania au ukoo uliokuwa na wachezaji wengi ktk soka la TZ?

    ReplyDelete
  7. Kama ni kuchezea clubs kubwa au hata kuwakilisha mkoa kama katika Taifa cup, enzi hizo.
    Familia ya Mzee Seif Tanga nadhani walikuwa ni wengi katika umahiri wa soka.

    !.Nassor Seif, alihamia Feisal Club, Mombasa, kabla ya kufariki bado kijana.
    2.Marshed Seif,TPC, Coastal Union,Tanga, National Team.
    3.Hemed Seif....TPC, Tanga National team.
    4. Rashid Seif huyu Polisi ka-retire nadhani miaka michache tu nyuma. Alikuwa midfield kali mno kwenye National team.
    5. Selemani Seif, probably the most talented of the Seif family brothers, his career was short as he hated upuuzi and uhuni unaombatana na kucheza mpira enzi hizo. He was a deeply religious person.
    6. Ali Seif, he went as far as playing for the junior National team.

    At one time the National team had Marshed, Hemed and Rashid Seif all in the field playing at the same time. Add that to the two Zimbwe brothers,(Saleh and Omar) nusu ya timu ya taifa ilikuwa ni familia 2.

    Inawezekana nimesahau kidogo, lakini hizo data wazee, hasa wa Tanga watazikumbuka.

    ReplyDelete
  8. MPIRA ENZI ZA AKINA SUNDAY MANARA ULIKUWA MPIRA SI MCEZO NA WACHEZAJI WALIKUWA VIPANDE VYA WATU NA WALIKUWA CELEBRITY KWELI WAKIPITA MTAANI WALIKUWA WANAFUATWA KAMA NINI SIJUWI. NA HUYU SUNDAY MANARA ALIITWA KOMPUTA KUTOKANA NA CHENGA ZAKE ZA MWILI, HAKUNA BEKI AMBAYE ASINGWEZA KUPOTEA KWA CHENGA YA YA MWILI, KITWANA ALIKUWA HODARI KWA KICHWA KWANI WAKATI HUO KUKIWA NA KONA HESABU GOLI

    ReplyDelete
  9. ukoo wa kina 'Muchacho' Ankal umesahau?

    ReplyDelete
  10. mmesahau na ukoo wangu jamani wa varangati unaitwa kaka michuzi.

    ReplyDelete
  11. Naungana na mdau kuwa si familia ya Manara pekee iliyowahi kutoa nyota wa mpira Tanzania kwa sababu tuna familia ya Kiwelu na Njohore mfano.

    1.Mussa Kiwelu (Simba)
    2.Mwanamutwa Kiwelu Yanga, Red Star
    3.Jamuhuri Kiwelu Simba, Plisner
    4.Mwesa Kiwelu (Red Star)
    5. Muhehe Kiwelu.

    Njohore family, kuna Nico Njohore, Deo Njohore, Lucas Njohore na Renatus Njohore, pia kuna akina Peter Tino, Gebo Peter, Emma Peter

    ReplyDelete
  12. Halafu kuna baba na mwana: (1)Awadhi Ghesani katika miaka ya 60 alichezea DMT (shirika lililoitangulia UDA) na Young Africans zote za Dar, na (2) mtoto wake Anwar Awadhi pia alichezea Young Africans ya Dar miaka 35 baadaye!!!!! Wale mnaoijua kile kiota cha (chips kuku na vinywaji usiku) Swahili street karibu na Morogoro road mtakua si wageni na jina la "kwa Maghesani".

    ReplyDelete
  13. Hawa ndio walikuwa wacheza soka baba. Angalia miili hiyo. Futi sita kwenda juu na lishe ya kueleweka. Sio tulionao sasa wakipigwa pushi kidogo tu wanaanguka. Anon uliyemtaja Anwar Awadhi hapo juu umenikumbusha sana enzi za Yanga "Yosso" huku Nonda Shabani akipiga center forward. Anwar Awadhi, Salvatory Edward, Silvatus Ibrahim, Nonda Shaaban, ????

    ReplyDelete
  14. Mmesahau familia ya magolikipa Kina Idd Pazi na nduguze.

    ReplyDelete
  15. Pia Kuna uko wa Kina Magongo
    Abbas khamis Magongo(RIP)
    Ibrahim Magongo
    Khalfan Ngassa
    Rashid Abdalah
    Shafie Magongo
    Mrisho Ngassa
    Wote Timu Ya Taifa Kasoro Shaffie
    lakini waliobaki ama waliwahi kuitwa timu ya Taifa ama ila Ya bara na Juu Marehem Abbas Khamis Magongo AKA Zamelek Kenya Harambe Stars Mpaka leo Hawajapata Midle Kama Yeye anaebisha Aseme sio hawa kina echeisa,mukenya na maringa

    ReplyDelete
  16. Nakubaliana na wewe ndau hapo juu familia ya Magongo haikuwa ya kawaida pia katika midani ya soka hizi data zimechalenji usemi wa kwamba familia ya Manara ndo ilitia fora kwenye soka hongereni kwa data wadau.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...