kikosi cha timu ya waandishi wa habari washabikiao Yanga
kikosi cha timu ya waandishi wa habari washabikiao Simba
refarii akiingia uwanjani na vuvuzela ambazo alizitumia kama filimbi mara baada ya kuisahau nyumbani ile cha kwake anayoitumiaga kila siku.
streika wa yanga akikabwa na mabeki wa simba
beki wa yanga,muhidin sufiani akimzuia kiungo wa timu ya simba,mroky mroki ili asiweze kuuwahi mpira katika mechi iliochezwa jana katika ufukwe wa hotel ya South Beach resort,Kigamboni
gemu likiendelea hadi majini.wadau hii ilikuwa ni mechi ya kujifurahisha ambayo iliwahusisha waandishi wa habari za michezo ambao ni washabiki wa timu ya Simba na wale ambao ni washabiki wa Yang,a ambapo mpaka dakika tisini zinamalizika timu ya Yanga ilikuwa ikiongoza kwa bao 2 na Simba 0.mechi hiyo iliandaliwa na kampuni ya bia ya TBL,kupitia kilaji chake cha Kilimanjaro wakishirikiana na kampuni ya Exective Solutions.mechi hii ilichezwa mara baada ya kumalizika kwa semina ya siku moja ya namna ya kuandika habari za mashindano ya Kili Taifa Cup kwa waandishi wa habari za michezo,iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mjimwema uliopo ndani ya hotel ya south beach resort,Kigamboni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. that's a wrong decision by the organisers, where is impartiality and independence?

    sasa wakiandika habari za hizo timu wataacha kupendelea? use your heads, training inakuwa si training bali upotoshaji.

    ReplyDelete
  2. duu hao wachezaji wa simba mbona jezi ni suruali iliyokunjwa this is a new style

    ReplyDelete
  3. Kweli wazungu walinena pale waliposema NO LOVE LOST maana nilivyoona tu Simba na Yanga hata ya washabiki moyo wangu ulikuwa una shauku ya kujua kama Yanga wameshinda au la.Na baada ya kuona Yanga imeshinda moyo umetulia,ni ajabu ukichukulia mimi sipo bongo kama miaka 10 na wala sijafuatilia Simba na Yanga tangu mwishoni mwa miaka ya 90.

    ReplyDelete
  4. Na hayo ndio matokeo ya Jumapili, tukae mkao wa kula!

    ReplyDelete
  5. Ndio maana nimeacha kununua magazeti ya michezo ya Tanzania hasa yanayoandikwa kwa lugha ya kiswahili maana yamejaa ukiukwaji mkubwa wa kanuni za uhandishi wa habari, na sababu kubwa ni hii tabia ya ushabiki.

    ReplyDelete
  6. bongo hamna mchezo mwingine ni soka tu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...