TANZANIA ILIADHIMISHA MIAKA 46 YA MUUNGANO WA NCHI YETU NCHINI UINGEREZA KWA IBADA MAALUM ILIYOANDALIWA NA KANISA LA WESTMINISTER ABBEY,LILILOPO WESTMINISTER HAPA LONDON, UINGEREZA.
KANISA HILO LA WESTMINISTER ABBEY, HUANDAA IBADA MAALUM KILA MWAKA KWA NCHI ZILIZO MWANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA (COMMONWEALTH COUNTRIES) NCHI HIZO ZINAPOFIKIA SIKU YA UHURU WA MATAIFA YAO.
UBALOZI WA TANZANIA KWA KUSHIRIKIANA NA BAADHI YA VIONGOZI NA WAWAKIRISHI WA JUMUIYA MBALIMBALI ZA WATANZANIA HAPA NCHINI UINGEREZA, WALISHIRIKI VYEMA KUIWAKILISHA NCHI KATIKA IBADA HIYO. MISA MAALUM ILIOANDALIWA NA KANISA HILO MWAKA HUU ILISOMWA NA DADA CAROLINE CHIPETA, MKUU WA UTAWALA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA.

Siyo WestminIster, ni Westminster, hiyo i hapo nilipoikuza hapo mwanzo haipo. Kunaitwa Westminster na si Westminister, watu wengi sana huwa wanakosea hii kitu.
ReplyDeletehii sia academic article mpaka umtake aandike bila kosa hata kidogo. na ikumbukwe blog kama hii hata editor haina. so when the message gets to ear that is enough. tutoe comment constructive tafadhali especially kuhusu general message please. nimeona niseme ili tumsaidie michuzi na wengine wasonge mbele na si kupoteza muda mwingi na unnecessary details like presence of i or its absence!
ReplyDeleteAnonymous wa pili, maelezo ya Anonymous wa kwanza ni ya kuilemisha jamii na yana umuhimu wake, tena mkubwa tu. Ikumbukwe kuwa Westminster ni jina la mahala, sasa likikosewa inaweza ikaleta matatizo.
ReplyDeleteNi sawa na mtu anataka kuja Dar, then anasema nipeleke Darussalam! Atapelekwa sehemu nyingine tofauti na Dar es Salaam, kwani kama inavyofahamika, Darussalam iko Brunei (South East Asia) wakati Dar es Salaam iko Tanzania (Africa).
Nadhani umeweza kuona na kujiridhisha na umuhimu wa kurekebishana humu ndani pamoja na kuwa maelezo yanzyowekwa humu kwenye hii blog sio academic articles.
Nawasilisha!