Mkutano wa kumi na tisa wa Bunge unatarajia kuanza Jumanne tarehe 13 Aprili na kumalizika tarehe 23 Aprili 2010 mjini Dodoma. Katika mkutano huu wa Bunge, shughuli za Mkutano mzima zitakuwa kama ifuatavyo:
1.0 SHUGHULI ZA SERIKALI

A. MISWADA YA SHERIA YA SERIKALI:

(Kusomwa mara ya kwanza na hatua zake zote)

katika Mkutano huu wa Kumi na tisa wa Bunge, Jumla ya Miswada mipya nane (8) itasomwa kwa mara ya kwanza na kupitia hatua zake zote. Miswada hiyo ni :-
1. Muswada wa Sheria ya Watu wenye Ulemavu wa Mwaka 2010, [The Persons with Disabilities Bill, 2010].

2. Muswada wa Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji wa Mifugo wa Mwaka 2010 [The Livestock Identification, Registration and Traceability Bill, 2010].

3. Muswada wa Sheria ya Kusimamia na Kudhibiti maeneo ya Malisho na vyakula vya Mifugo wa Mwaka 2010 [The Grazing-Land and Animal Feed Resources Bill, 2010]
4. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali za Fedha wa Mwaka 2010 [The Financial Laws [Miscellaneous Amendments) Bill, 2010].

5. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Masoko na Mitaji na Dhamana wa Mwaka 2010 [The Capital Markets and Securities (Amendments) Bill, 2010].
6. Muswada wa Sheria ya Madini wa mwaka 2010 [The Mining Act, 2010]
7. Muswada wa Sheria ya Madawa wa mwaka 2010 [The Pharmacy Act, 2010]
8. Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa mwaka 2010 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments ) Act, 2010]
B. MAAZIMIO YA BUNGE:

Halikadharika, Bunge linatarajia kuazimia Azimio litakalowasilishwa na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambalo ni Azimio la Kuridhiwa kwa Itifaki ya Soko la pamoja la Afrika Mashariki
2.0 MASWALI:

Aidha, katika Mkutano huu wa Kumi na Tisa, Jumla ya Maswali 125 yanatarajiwa kuulizwa na Kujibiwa ambapo Maswali 14 yanategemewa kuulizwa kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu.
3.0 TAARIFA ZA KAMATI:

Kwa Mujibu wa Kanuni ya 114 (15) ya Kanuni za Bunge, Toleo la 2007, Kamati zote za Kudumu za Bunge zitawasilisha Mezani Taarifa za Mwaka, na kwamba taarifa hizi zitapangiwa muda wa kujadiliwa katika Mkutano ujao wa Ishirini wa Bunge.

KAMATI YA MIUNDOMBINU:

(i) Taarifa ya Kamati ya Miundombinu kuhusu Taarifa ya Serikali ya Utekelezaji wa Azimio la Bunge kuhusu Uendeshaji Usioridhisha wa Shirika la Reli Tanzania. uliofanywa na Kampuni ya RITES ya India.

(ii) Taarifa ya Kamati ya Miundombinu kuhusu Taarifa ya Serikali ya Utekelezaji wa Azimio la Bunge kuhusu utendaji wa kazi usioridhisha wa Kampuni ya Tanzania International Container Terminal Services (TICTS).

4.0 SEMINA ZA WABUNGE WOTE:

Katika mkutano huu wa Kumi na Tisa, Ofisi ya Bunge imepokea maombi ya kufanyika kwa semina zifuatazo:

i. Semina kwa Wabunge wote kuhusu Mapitio ya MKUKUTA - I na mwelekeo wa MKUKUTA –II itakayotolewa na Wizara ya Fedha na Uchumi tarehe 15/4/2010

ii. Semina kwa Wabunge wote kuhusu Soko la Pamoja la Afrika Mashariki, itakayotolewa na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Semina hii imepangiwa tarehe 17/4/2010 siku ya Jumapili.

Imetolewa na
Owen Mwandumbya
Kny: KATIBU WA BUNGE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hivi hatima ya Mpendazoe ni nini sasa, ina maana ubunge basi au mpaka uchaguzi? Kama hivyo ndivyo, kwanini kawafanyia hivi wapiga kura wake? Kwanini kahama chama kabla ya kumaliza kipindi chake cha kuwatumikia wananchi na bunge kuvunjwa? Na mafao yake je? This was a craziest decision of all time, pamoja na kwamba mimi naichukia CCM kwa damu yangu yote!!!

    ReplyDelete
  2. Wataalamu wetu wa Kiswahili saidieni kuokoa jahazi jamani. Matumizi ya 'r' badala ya 'l' na 'l' badala ya 'r' yanazidi kushamiri.

    ReplyDelete
  3. Pat-MagazetiApril 13, 2010

    Hivi Bunge na Wabunge wetu wamelala usingizi wa pono. Ajali zinatokea kila siku na hakuna mapendekezo au sheria mpya bunge imefikiria juu ya ajali barabarani..watu wanakufa kila siku..hii ni aibu kubwa sana kuona tunasahau kujilinda kwanza. Pili, rushwa na wizi umezidi serikali na kote kwenye vyombo vya serikali na binafsi mbona hakuna marekebisho ya sheria na muswada. Tatu, juu ya electricity, this is national security issue na bunge na wabunge why they shy away from it. Bunge wana mpango gani juu ya upungufu wa umeme Tanzania na Zanzibar.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...