ANKAL NA WADAU WOTE
-ASALAMALEKO
-TUMSIFU YESU KRISTO
-BWANA ASIFIWE
KUMRADHI KWA HILI NDUGU ZANGU. JANA NIKISIKILIZA CLOUDS FM JIONI NILISIKIA WAKIONGELEA SWALA AMBALO BAADA YA KULIFIKIRIA SANA NIKAONA NI NYETI, NA NI KWELI WENYE KULITUMIA SANA NI WAHESHIMWIA WABUNGE WAKIWA WAKIJADILI MJENGONI DODOMA.
NENO LENYEWE NI "MTANZANIA WA KAWAIDA"
UTAKUTA MH. KAKAZANA TU KUFAFANUA JAMBO NA KUSISITIZA KWAMBA JAMBO HILO 'KWA MTANZANIA WA KAWAIDA' LINA MAANA YA HIKI NA KILE.
NAMI LEO NIMEONA NIOMBE MSAADA KUULIZA HUYU 'MTANZANIA WA KAWAIDA' YUKOJE YUKOJE NA NI NANI? NA JE WAH. HUMAANISHA NINI WANAPOMTAJA HUYU 'MTANZANIA WA KAWAIDA????'
MDAU
URAMBO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. kaka unapoongea kuhusu mtanzania wa kawaida kwa hali halisi ni yule aliyemo ktk lile kundi kubwa la watu milioni 30,anayeishi kwa chini ya nusu dola kwa siku, hilo ni neno la kupunguza makali kisiasa

    ReplyDelete
  2. Mdau wa Kwanza..,

    HakiElimu ( an organisation deals with education and democracy in Tanzania) would have a significant definition for "mtanzania wa kawaida". Ordinary Citizen.

    ReplyDelete
  3. Inategemea na isue yenyewe. Kama inahusu kipato, basi ni yule mwenye kipato cha wastani (sio cha juu sana au chini sana), kama ni ufisadi, basi ni yule asiye na nafasi ya kufanya kufisadi, kama ni elimu, basi huyo ni darasa la saba!!

    ReplyDelete
  4. 'Mtanzania wa kawaida' ni yule mtanzania 'mchovu kiuchumi' anayedanganyika kisiasa kwa urahisi zaidi.

    ReplyDelete
  5. Mtanzania wa kawaida = common man = ordinary "people" = middle and lower classes = (sometimes) hoi polloi = mlala hoi = below a certain "wealth" line/level = every Tom, Dick, and Harry == kwa ufupi ni wapiga kura na wavuja jasho.

    Ni lugha ya kawaida katika jamii yeyota duniani. Hata wakati wa Yesu wa Nazareth walikuwepo, ndio aliokuwa akizunguka nao na kuwapa mafundisho.

    M-tizii wa kawaida ndio anatakiwa kuwezeshwa ili awe na maisha bora!!

    ReplyDelete
  6. AVERAGE JOE

    ReplyDelete
  7. Mtanzania wa kawaida ni mkulima. Mkulima sio mtu ashikaye jembe kwa kupata ridhiki ya kila iku. Mkulima ni mtu ambaye yuko yuko tu, hana mbele wala nyuma kutokana na sera maalumu ya sisiemu ya kuwanyima wa2 elimu ili kuwatawala kiurahisi. Ndio, ukumnyima m2 elimu na kumwacha shidani hatakuwa na la kufanya zaidi ya kufikiria cha kupeleka 2mboni.
    Hicho ni kifungu cha maneno 'phrase' ambacho kama mdau hapo juu amesema, ni kwa ajili ya kupunguza ukali kwa hao wakulima! Hee heee

    ReplyDelete
  8. Ni mtu yeyote mlalamishi!!

    ReplyDelete
  9. Ni majority ya watanzania, yaani walio tayari kuuza kura ili mradi apate sahani ya ubwaubwa ama sh5,000

    ReplyDelete
  10. mtanzania wa kawaida ni yule asiyejuwa haki yake, anaekubali kundanganyika na mafisadi wachache

    ReplyDelete
  11. Anonymous kwa kiswahili ataitwaje?

    ReplyDelete
  12. MTANZANIA WA KAWAIDA NI YULE AMBAYE MAISHA YA ANATUMIA SIO ZAIDI YA $ 1 KWA SIKU NA NDIYE MPIGA KURA NAMBA MOJA KUCHAGUA CCM

    ReplyDelete
  13. mtanzania wa kawaida ni yule akiambiwa na ccm kuwa ukichagua wapinzani wataleta vita kama ya burundi na rwanda naye anamini kwa 100%

    ReplyDelete
  14. mtanzania wa kawaida ni yule ambaye anasikiliza longo longo hajui haki zake za msingi

    ReplyDelete
  15. Mtanzania wa kawaida ni 'a downtroden person' kwa lugha nyingine unaweza ukamwita 'MSAKANYOKA'. Huyu shughuli zake na muda wake anaumalizia vumbini. Huyo ndiyo Mtanzania wa kawaida

    ReplyDelete
  16. ...anaitwa anonimia.

    ReplyDelete
  17. ni wewe.

    ReplyDelete
  18. mtanzania wa kawaida si ni mtanzania wa kawaida? yani ordinary tanzanian kwa kiswahili mtanzania wa kawaida, embu tuiandike kwa herufi kubwa ili tuielewe vizuri MTANZANIA WA KAWAIDA. huyu ni mtu wa kawaida sana. umeelewa? 'KAWAIDA'unajua maana yake? sasaongeza mtanzania af utapata jibu. usisahau kufanya hom work.
    TEACHER.

    ReplyDelete
  19. hili swali ni nzuri sana na tena ni chemsha bongo kali. mtanzania wa kawaida ni mimi na wewe tusiojuwa haki zetu au tunajuwa ila hatujiamini. ila mtanzania asiye wa kawaida ni mafisadi ambao ni wachache, mimi ktk nchi nazani wakulima wanaamani kwani wao wasiwasi wao ni vua tu ikoinyehesha basi hawana shida lakini mimi na wewe hasa ninyi mnao fanya vibaruwa kutwa barabarani na foleni za magari,vumbi,joto,mbu,mshahara mdogo hao ndiyo watanzania wa kawaida. matokeo yake umeshikwa na hasira nunatamani uwamalizie wakulima wakulima ni bora kuliko mfanyakazi wa kawaida asiye fisadi kwani they have peace of mind if you now what i mean!!!!! kuwashuhudia mafisadi wanavyoikongorowa nchi ina uma sana unaweza kufa na presha

    ReplyDelete
  20. Mtanzania wa kawaida ni raia wa Tanzania ambaye anaishi tu kwa vile kumekucha. Hajui haki zake za kiraia anavunwa (exploited class) na kila kundi la kijamii hapa nchini na zaidi sana wanasiasa.

    Ni watu walioshikilia makali ya panga mpini hawajui ulipo mpini.

    ReplyDelete
  21. mtanzania wa kawaida ni yule anayehongwa kanga na t-shirt na CCC wakati wa uchaguzi ili aichague huku akitaraji kuwa nchi bado changa na CCM ikiondoka kutatokea vita.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...