27.04.2010 (kushoto)
AKIWA NA MAREHEMU KIBWANA (Tall)
aliefariki 19 .04 .2010.
MARAFIKI NA JAMAA TUNAMJUA MAREHEMU KWA NICKNAME YA SEFU DJIBOUT, NA HATUNA MAELEZO YAKE KIREFU. YEYOTE ANAEIJUA FAMILIA YAKE AJARIBU KUWASILIANA NASI. INASEMEKANA ALIKUWA NI MKAAZI WA KEKO JIJINI DAR. WAZAZI WAKE NI WAZALIWA WA KUSINI MWA TANZANIA. AMEONDOKA TANZANIA MIAKA YA 85-90. ALIWAHI KUBANKA DJIBOUT KABLA HAJAWASILI UGIRIKI.
KAMA KUNA MTU YOYOTE ANAYEJUWA NDG WA MAREHEMU SEFU DJIBOUT TUNAOMBA MUWASILIANA NA KATIBU WA JUMUIYA HAPO CHINI
1- Lemesoy Str. T.K.11252,
MARAFIKI NA JAMAA TUNAMJUA MAREHEMU KWA NICKNAME YA SEFU DJIBOUT, NA HATUNA MAELEZO YAKE KIREFU. YEYOTE ANAEIJUA FAMILIA YAKE AJARIBU KUWASILIANA NASI. INASEMEKANA ALIKUWA NI MKAAZI WA KEKO JIJINI DAR. WAZAZI WAKE NI WAZALIWA WA KUSINI MWA TANZANIA. AMEONDOKA TANZANIA MIAKA YA 85-90. ALIWAHI KUBANKA DJIBOUT KABLA HAJAWASILI UGIRIKI.
KAMA KUNA MTU YOYOTE ANAYEJUWA NDG WA MAREHEMU SEFU DJIBOUT TUNAOMBA MUWASILIANA NA KATIBU WA JUMUIYA HAPO CHINI
1- Lemesoy Str. T.K.11252,
Athens-Greece,
E-mail:tanzathens@yahoo.com
Tel.+302110115337
MOB +304945347085 (KAYU LIGOPORA)
MOB +304945347085 (KAYU LIGOPORA)
Poleni sana watanzania Ugiriki watanzania wote kwa ujumla.Kitu hii niliwahi kuongea na wenzagu kama wawili huku ninakoishi,jamani watanzania tuwe makini katika kujiandikisha na kueleweka tunakotokea.Ikiwezekana balozi zetu zilifanyie kazi hili jambo UPYA, watu wote wakajiandikishe upya watoe na majina,simu,anuani na mahali pakazi pa ndugu/jamaa hata watano(5) ambao wanaweza wakatafutwa incase of anything.Ikiwezekana na maelezo kwa ufupi ya kufika kwa nduguzo huko nyumbani.
ReplyDeleteWengine wako huku wana ndugu zao wengi, hao wana afadhali lakini kuna wengine hana ndugu huku, na wala marafiki zake wa karibu hawamjui kihivyoo.Inakuja inaleta shida kukitokea mambo kama haya,anyway, yameshatokea, tusaidiane kusambaza habari kwenye mablog mengine huko, labda jamaa zake watapatikana.
Mungu amlaze marehemu Seifu mahali pema peponi,Amina.
Michuzi huyo Tall naye kafia huko au? just curious, its very sad.Mwishoni tunakuja kuzikwa kwenye manchi ya watu bila hata kupenda, duuuu,Eeh mola tusaidie.
Mdau
Finland
Jamani hawa watu wamefariki mwezi mmoja walikuwa wanaumwa au nini?
ReplyDeleteMungu azilaze roho za marehemu hawa marafiki mahali pema pepon
schola
Duh kweli ubinadamu kazi sasa nyie mmeishi na baharia mwenzenu miaka yote hiyo lakini hata kujua jina lake hasilia mmeshindwa. mna kalia kumwita majina yanu ya kibaharia. msela kwa sababu alisha zamiaga Djibout basi mna mwita Djibout kazi kweli kweli. Sisi wa Africa tuna kazi. just basic things we cant deal with Ndo nchi hitajengeka kweli!!
ReplyDeleteR.I.P Djibout as they call you my friend .
MAISHA YA UZAMIAJI SI MASIRI KWA KWELI MJOMBA KAZAMIA MIAKA YOTE HIYO NA BADO AKUTOKA. MLIO HAI HUU NI JIULIZENI NA NYIE BADO UNA GANGAMAA UKO ADI LEO NI BORA MRUDI MA HOME WAZEE. MAISHA YA KUDANDIA DANDIA YANA MWISHO WAKE. COME BACK HOME PPL. KAMA AMNA NAULI NENDENI UBALOZINI MTAFIKIRIWA
ReplyDeletepoleni watanzania wote kwa ujumla
ReplyDeletesayas boka
Embu sema hawa jamaa marafiki imekuwaje wamefariki wote kwa muda mfupi?
ReplyDeleteKujitambulisha ubalozini ni kupoteza muda. Balozi zetu nyingi hazina muda na Watanzania ughaibuni. Nimepata kujitambulisha kwa email kwenye balozi tatu tofauti huku nje lakini email zangu hazikujibiwa. Ni kama vile zilipotea tu. Ajabu nikiandikia balozi nyingine (za kigeni) huwa najibiwa lakini wangu mwenyewe (Tanzania) sijibiwi! Kwa kweli inakatisha tamaa. Labda kuna mawazo kuwa kila mtu anataka kuomba msaada Ubalozini. Kuna watu tuna hela zetu na tunaweza hata kuchangia Ubalozi. Kujitambulisha ni kutimiza wajibu tu.
ReplyDeleteWatanzania Ugiriki mnaishije? watanzania wenzenu mnaishi katika mji mmoja mnashindwa kujuana miaka yote hiyo? Shame on you guys. Igeni mifani ya wenzenu Uingwereza (TZUK), Canada (TZCA), US, Watanzania Oslo, India nk, wote wanaumoja thabiti, na wanasaidiana katika mambo mbalimbali ya raha na shida.
ReplyDeletenafikiri ni vizuri habari hii ikatoka kwenye ma-TV na Maredio huko Bongo kwani jamaa wengi hawajui hata hii technohama.Hususan maeneo yaliyotajwa.Itabidi maredio yanayosikilizwa sana kama Redio Mawingu(nimesahau kizungu chake) , Radio One, ITV ,DTV ,CTN na vituo vingine vya Habari na magazeti ya udaku(Global Publisher)
ReplyDeletePia kuna masela waliowahi kuzamia wako mitaa ya keko wajulishwe kuhusu hizi habari wao wengi hujuana sana(Mabaharia)!!
Niliwahi kufika pia Sudan nikakuta Mabaharia wa Kibongo kibao wameshaoa na kuwa wenyeji hapo na hawana nauli ya kurudi Bongo , yupo mmoja alirudi Bongo na amekufa mwaka 2005 hakuwahi kuonana na wazazi wake toka mwaka 1979.Kuna wadau kibao(Mabaharia) South kwa babu, wameeka lakini bado wanatafuta ''safari''kuna wengine wamekuwa mateja na wengine ''makontena'' hawajawahi kurudi Bongo kwa miaka kibao
Huko Mozambique usiseme, Mombasa
Jenerali Ulimwengu aliwahi kurusha kipindi DTV akihojiana na Mabaharia bahati mbaya alikikatisha kipindi hiki na baada ya wiki aliyekuwa akihojiwa akafariki, alianza kutoa habari nyeti mno ya maisha ya Kibaharia, hatukujua kwa nini Jenerali alikizima kipindi kile.
Bwana Issa Michuzi na timu yako mnaweza kufanya Documentary ya ''Mabaharia '' kwa nchi hizi na kuangalia jinsi gani ya kuwapa msaada, wengi huona aibu kurudi nyumbani kwani ni chooka mbaya na hawana sehemu ya kufikia.
Kuna wale waliokufa Sudan , walitekwa na Jeshi la Garang miaka hiyo ya 80, kuna Mdau mmoja anaitwa Hamis Kanene anaweza kukupa data nyingi mno.Ukitaka mawasiliano naye jibu hapa nitakutafuta nikupe details ili kujua maisha ya Mabaharia
Kimaelezo huyu jamaa aliyekufa kama napata picha yake, aliwahi kusafiri kupitia Somalia miaka ya mwishoni mwa 80 na mwanzoni mwa 90 akanusurika vita akarudi Bongo kupanga safari kupitia Djibout.Alikuwa akiishi mitaa ya Kinondoni ni mtu wa Pwani ya kusini
Mdau , Holland
Greese Tz Poleni. Ila ningependa kuwaeleza wengine kuwa kuna watu wanaficha backgrounds zao. Wengine wanatoka Peramiho kama mimi na wakifika kwanja wanabadilisha majina na kuweka life story ili waonekane kuwa wao no born here here au kuficha makovu ya maisha yaliyopita. Kuirudisha story hiyo kwenye ukweli, wengi wanashindwa na wanabakia akina "Mzungusha hodari" mpaka kifo. Kumfuatilia mtu ajieleze yeye ni wapi na vipi ni kujitafutia matatizo Inabidi mdau ajiweke "uchi" yeye mwenyewe kwanza. Pia msisahau nchi nyingi kuna watanzania waishio kama wasomali/waburundi nk.
ReplyDeleteBlackmpingo
shame on you too...mtu anajiita mwenyewe djibout.msela kwa sana,hana story na watu ktk jamii yake,kutwa na masela wenzie ukimuuliza jina lako atakwambia oo naitwa ngumi jiwe,ooo naitwa kalkiti ooonaitwa blaa blaa hata huko uk na canada mnajipa uraia wa kirwanda na kisomali mbona mimi najulikana majina yangu yote matatu na wapi natoka nawapi nduguzangu watapatikana msilaumu tu watu ni akili tu za baadhi ya watu.mdau greece
ReplyDeletemjomba naye kajitakia yani kaishi na wenzake miaka yote hiyo kauchuna tu hata kuwaambia wenzake anatokea wapi akuna!! awa ndo wale marafiki mnajuana maofisini tu na kwenye vilabu vya pombe hila kamwe akuonyeshi hata anaishi wapi. kweli jamba jamba !!
ReplyDeletehali kama hii wana ndugu hata wakisikia lazima wakaushe kwani wanajua next ni kudahiana michango ya kuusafirisha mwili wa marehemu!!kama waliokuwa wanaishi na maremu tu awajuhi habari zake hinaonekana marehemu alikuwa mtu mnoko sana hata sizani kama alikuwa anakumbuka hakutuma h viji cent kwao.
ReplyDeletemimi ninavyo wajua wabongo lazima wamkaushie hata mkitangaza redioni.Mtu kalowea miaka yote uko.Na siyo hajaku akuagaga kwao.
r.i.p sijuhi niseme nani sasa kwani hatukujuhi jina
WABONGO KAZI NI KUCHONGA. HAPA NI HABARI ZA MSIBA SI KUJARIBU KUZUNGUMZIA WATU WANAOTAFUTA MAISHA VIPI. WENGI WENU HAPA KWA KUANDIKA TU MNAONEKANA WAZAZI WAMEWASAIDIA KIMAISHA SI KAMA MAJAMAA WALIOKWENDA KUTAFUTA MAISHA. WAZUNGU WENYEWE WALIKWENDA DUNIA NZIMA KUTAFUTA SIO VILE MNAVYOCHONGA TU HAPA WATU WANAJITUMA KUTAFUTA. KWENYE KUTAFUTA KUNA MENGI KUPATA MAFANIKIO AU KUKOSA KWA HIVYO MUHIMU HAPA KAMA HUJUI JAMAA WA MAREHEMU WEWE NYAMAZA AU KAMA WEWE NI MWANADAMU OMBA DUA KWA NDUGU YETU ALIYETUTANGULIA SI KUCHONGA HAPA NI KITU MUHIMU KWA NDUGU HUYU TAHARIFA ZIFIKE KWA NDUGU ZAKE. JARIBU KUFIKIRI KAMA UNGEKUWA KWENYE MATATIZO KAMA HAYA. SIKU HIZI KUWA WATANZANIA WANACHONGA SANA WANASAHAU KUWA WENGI WETU NI MASIKINI SANA WACHACHE WENYE MAFANIKIO.KWA HIYO ANDIKENI KUHUSU NDUGU YETU ALIYETUTANGULIA JAMAA ZAKE WAPI WATAPATIKANA' SI KUANDIKA WAPI ALIKWENDA AU VIPI ALIKWENDA. SHUKURU KAMA UNAMAFANIKIO KIMAISHA SI KUKAA KUCHONGA. NA KWAMBIA WEWE KAMA MTANZANIA UNA NDUGU ZAKO WENYE SHIDA SI ALL YOUR FAMILY WANAVYO KILA KITU. HAPA SI PA KUKOSOA WAPI AU VIPI UMETAFUTA MAISHA YAKO HAPA NI MSIBA WA MTANZANIA MWENZETU ALIYEKUWA NJE YA NCHI AKITAFUTA MAISHA YAKE. MSAADA MICHICHANI SI WATOTO WA MAMA KAMA WEWE.
ReplyDeleteASANTE.
TEMEKE POLICE CHAN'GOMBE
NIMEAMINI WAJINGA WENGI SANA NA WATU WASIOJUA MAISHA WALA MAANA YA MAISHA WAKO WENGI SANA,NA WOTE PIGA DOMO NI KULA KULALA WALA HAWAJUI KUTAFUTA HELA ZAO WAO WAMEKUWA NA KUSOMESHWA NA BABA NA MAMA NA KUPATA KILA KITU ILA KAMA UKITAFUTA MAISHA MWENYEWE NDIO UTAJUA NINI MAANA YA MAISHA..WENGI WANAMLAUMU MAREHEMU KWANINI HAKUTAJA JINA LAKE HALISI,HIVI NYINYI MNAJUA MAISHA YA ULAYA YALIVYO?WENGINE WAMEKUJA HUKU KUTAFUTA MAISHA BABA ZAO NA MAMA ZAO HAWAKUWEZA KUWASOMESHA NA HAWANA UWEZO KABISA NA KULINGANA NA NATURE YA WABONGO KUWA WAMBEA JAMAA WANAAMUA KUFICHA UKWELI WAO ILI WASICHOMEWE KURUDISHWA MAKWAO MAANA WANAJUA MAISHA KWA BI MKUBWA WALIYOYAACHA..NYINYI NINI BWANA..MSHUKURUNI MUNGU MMEZALIWA KWENYE FAMILIA BABA MAMA WANAWEZA KUWASAIDIA WENGINE WANATOKA FAMILIA HATA CHAI KUNYWA SIKUKUU..ANYWAY SWALA HAPA NI KUWATAFUTA JAMAA WA HUYU JAMAA HILO NDIO LA MUHIMU SANA ACHENI KUPIGA DOMO.POLENI SANA NDUGU ZETU WA UMANGANI.
ReplyDeleteNDUGU YENU KWA MAMA HAPA.
I second you Temeke Chang'ombe.
ReplyDeleteRIP Djbout
Watanzania tumezidi sana midomo juu linapotokea jambo...It's what it's ...sasa tatizo ni kujua ndugu zake....maneno mengine ya why this why that keep it to urself.....
nyinyi msipate tabu huyo jibut atafutwe ndugu yake marehem kitgeng,wa keko pale mitaa ya fenicha.then yule ndugu yake kitgeng alikaa mageto manne na kina elia ,moshi bombay,huyo ndugu wa marhem kitegeng anaitwa sultan kitupula kitgeng ww ukienda keko fanicha uliza hapo ni maarufu sana kuna hemedi macho anauza fenicha ,au muwasiliane na walienda bongo wabongo wenzenu wafatilie hiyo ...huyo jibut mpelekeni bongo kwa umoja wa mabaharia bagej room watamzika ,iko siku watapatikana familia yake wataoneshewa kaburi la mwanawao...one peace mabaharia wenzangu..mungu amlaze mahala pema peponi..seif djibut.ameen
ReplyDeleteNadhani kama mtu hana taarifa yoyote inayoweza kusaidia kupatikana kwa ndugu wa marehemu ni bora asiandike commments maana hatokuwa na faida yoyote.Ndugu zetu wa Uigiriki wanajitahidi kumsaidia mwenzao na sisi huku bongo tumebaki kulalamikia jinsi wanavyoishi ulaya........Kama tunadhani maisha ni rahisi kwa nini tunabaki hapa na kulalamika?Wengine tangu asubuhi tunakuja kunywa chai saa nne usiku je hii chai ya saa nne usiku ni ya kulalia au ni kifungulia kinywa? Hebu tusichanganye mambo
ReplyDeleteI salute you..POLICE CHANG'MBE.
ReplyDeleteTutafute solution hatutafute mchawi.
Sina taarifa za kusaidia hili tatizo.
ReplyDeleteNina sad feelings kwa watanzania tuliojitoa mhanga kutafuta maisha ya ubaharia/uzamiaji na tukafika mahali tumekwama.
It is always a game wengine wameshinda na wengi tumeshindwa. Kibaya ni kwa walioshindwa wanakuwa hawana njia ya kurudi kwa kukosa nauli ama hata kujisikia aibu ya kurudi mtumpu.
bado wengine wengi wana mitazamo ya kuuza madawa ambayo ni out of fashion na system kwakuwa utaishia jela.
I pray watu tupate mwanga wa kurudi TZ mapema no matter what.
Sisi ni wajeshi ambao hatujakata tamaa. Ila kukubali kushindwa na kufanya retreat ni sehemu ya vita.
Turudini home ndugu zangu. Wako ambao hata kula na kulipa nyumba ni ngumu. Wako wengine Brazil hata kazi ya mkate hawana
SAD SAD SAD SAD jamani
Please tuangalie vinginevyo
Salut Temeke Chan'gombe.
ReplyDeleteVery sad indeed.
Kuna mtu hapo kasema huyu jamaa alikaa Kinondoni, je unajua kinondoni ipi au unamjua aliyekuwa akifahamiana nae kipindi hixho? If so jaribu kutafuta tafuta maybe tutapata ndugu.
Na kwa habari kuwa alikaa Keko, humu hakuna wenyeji wa Keko wakajaribu kuuliza ktk familia zilizoishi kwa muda mrefu Keko?
Nasikitika sana maana kaka yangu aliondoka nikiwa la kwanza (1979), hatujui alipo, aliondoka akaenda Ilaly kupitia huko huko Somalia na Djibout, then alituandikiaga akiwa Greece miaka ya 80 mwishoni, then kimya mpaka leo. Kila baharia naekutana nae namuulizia lakini waaapi. Nimekuwa touched sana na hili jambo I wish ningekuwa na msaada, but sina zaidi ya kutoa pole kwa wana ugiriki.