
Usiku wa Mzee Yusuf
Mzee Yusuf anaendelea vizuri na Jumapili 25/4/2010 (Mkesha wa sikukuu ya mapinduzi ya Zanzibar) atakamua vilivyo ndani ya ukumbi wa Travertine Hotel Magomeni katika onyesho kubwa la taarab linalokwenda kwa jina la Usiku wa Mzee Yusuf.
Jamaa atashuka na nyimbo zake zote zilizotamba tangu alipoanza kuimba taarab katika kundi la Zanzibar Stars Modern Taarab hadi Jahazi Modern Taarab, yaani ni kuanzia mambo ya Msumari, Soda ya kopo hadi Alamba alamba aam!
Lengo la onyesho hili ni kumpongeza Mzee Yusuf na kutoa changamoto kwa wasanii wengine waweze kulinda mafanikio yao na kupata heshima kama hii.
Lakini pia kubwa zaidi ni kuwaburudusha na kuwapa ladha tofauti wapenzi wa taarab kati ya nyimbo za zamani na mpya za mkali huyu anayechukuliwa kama mfalme wa modern taarab.
Katika onyesho hili Mzee yusuf ambaye aliaanza taarab kama mpiga kinanda katika kundi la East African Melody atasindikizwa na kundi zima la Jahazi Modern Taarab pamoja na wasanii wengine kibao wakiwemo Omar Tego kutoka Coast Modern Taarab pamoja msanii nyota wa Bongo Fleva Diamond anayetamba na nyimbo zake “Kamwambie” na Kwetu Mbagala”
hiyo ni siku ya muungano sio mapinduzi ya znz. mapinduzi ni trh 12 januari sio 25 aprili
ReplyDeleteSikuku ya mapinduzi? Mbona mie nilishiriki katika mapinduzi hayo na ilikuwa tarehe 12/jan/1964.
ReplyDeleteHii ni sikukuu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Muungano Oyeeeee
Bwana Mungu amejibu dua zetu tulizokuombea katika jina la Yesu. Haleluja. Fanya mazoezi ya mwili Mzee.
ReplyDelete