Mdau akilamba Nondozz yake toka kwa mkuu wa chuo kikuu cha University of Mysore katika mahafali ya tatu yaliyofanyika jana huko Mysore,India
wadau wakila pozz na Bango la chuoni hapo
baadi ya wanafunzi waliomaliza mwaka huu chuoni hapo wakionekana kutokea kideoni
furaha ya kula Nondozz ilitawala kwa kila mtu
wadau waliolamba Nondozz mbali mabli katika chuo kikuu cha University of Mysore wakiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa chuo hicho katika mahafali ya tatu ya chuo hicho yaliofanyika jana Mysore nchini India.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Hiki Chuo wanasoma watu WEUSI tu au ndio Wahindi hawataki kujichanganya?

    ReplyDelete
  2. Hivi hiko chuo ni wa Waafrika tu? au ni picha tu? sababu sioni hata mhindi mmoja katika picha hiyo. Hongereni sana kwa mahafali yenu.

    Mdau

    MD

    ReplyDelete
  3. Hii dunia ya ajabu saana. Wahindi wanakimbilia kusoma Ulaya na Marekani, Watanzania wanaenda India. Sijui ubora wa chuo hiki lakini vipo vyuo India ni vizuru. Kwahiki??? Kwanini watu wasiende South Africa ambako Tz km SADC wanaiver ya fees?

    ReplyDelete
  4. haijalishikama hicho chuo ni cha watu wakijani wa pink au njano watu wamekula nondo zao full stop!! hayo mengine hayahusu kwani ishu ni nini? eboh? hongereni wadau woooote kwa kula nondo as long zinakubalika kimataifa mko juu tuu mtakuja kuwa mabosi wa hao hao wanaouliza ati chuo sijui ushuzz gani hongereniiii sanaaaaaaa

    ReplyDelete
  5. oh hii picha wameamua kupiga wanafunzi blacks only au chuo chote ni black students only au katika darasa hilo kulikuwa na blacks only.chuo kiko india sioni hata muhindi hapa.

    ReplyDelete
  6. Hapo ndio inaonesha hiko chuo dili tu La wahindi wanakuja kuchukuwa pesa Africa sasa sibora Wajengee humuhumu Africa Tanzania hiko Chuo asilimia kubwa hapo ukichunguza utaona ni Watanzania pia.

    ReplyDelete
  7. Wajinga ndio waliwao.

    ReplyDelete
  8. MDAU MMOJA ANASEMA NENDENI SOUTH AFRICA NA TZ KAMA SADC WANAIVER FEES , HII MAANAKE NINI MIMI SIELEWI? WANAIVER!!!!!!! EBU TUELEZE VIZURI TUFAIDIKE

    ReplyDelete
  9. Wadanganyika, jamani: Logi, logic, logic... aliyepiga picha hizi na kuzituma kwenye blog gii ya jamii ni mtanzania, mwanafunzi, na mhitimu. Je, kulikuwa na haja ya yeye kulenga Camera yake kwa Wahindi, ambao hawatuhusu sisi.
    Hizi picha zilikuwa zinachukuliwa kwa ajili yetu sisi watanzania, ndio maana hakuna muhindi humo.
    Hii University ina wanafunzi 4200, na asilia 96 ni Wahindi, sio watanzania.

    ReplyDelete
  10. Hongera zenu sana. Sie huku tunabeba maboxi halafu twende shule ni ngumu sana inaelekea wenzetu mmesoma kwa dezo.Mmekula kitabu tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...