Meneja wa Bia ya Safari Lager,Fimbo Butallah akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) namna bia ya safari Lager itakavyoweza kufanikisha mashindano ya Pool kwa wanafunzi wa elimu ya juu katika mkutano uliofanyika leo.
Naibu Waziri wa Michezo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kayumba Torokoko akiongea na waandishi wa habari waliofika katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Safari Pub uliopo ndani ya TBL.Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager,Fimbo Butallah.
Baadhi ya washiriki wa mchezo wa Pool kutoka katika vyuo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja.

HIGHER LEARNING SARARI LAGER POOL COMPETITION 2010

Bia ya Safari Lager, inayozalishwa na Tanzania Breweries Limited (TBL) na ambayo ndio mdhamini mkuu wa mchezo wa pool hapa nchini imetangaza kuyadhamini mashindano ya kucheza poolkwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu yanayofahamika kwa jina la (Higher Learning Safari Lager pool Competition 2010).

Mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha vyuo vikuu kumi na vyuo vya kati kumi na vinatarajiwa kutoana jasho kwenye mashindano hayo yatakayofanyika katika ufukwe wa coco Beach kuanzia may 14 hadi may 16,2010 jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naimu Waziri wa Utamaduni na Michezo Mh. Joel Nkaya Bendera.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Meneja wa bia ya Safari Lager, Fimbo Butallah alisema “Azma ya Safari Lager ni kuleta mapinduzi ya kweli na mafanikio makubwa katika mchezo wa pool hapa nchini, hivyo udhamini huu wa mashindano vyuo vikuu na vya kati ni moja kati ya malengo ya bia ya Safari kuhakikisha inatambua na kuthamini mchango wa wanataaluma katika nyanja ya michezo nchini Tanzania.”

Bwana Fimbo aliendelea aliendelea kusema “Washindi wa mashindano hayo watajipatia zawadi zenye thamani ya Tsh. 3,000,000/= za kitanzania –ambapo ni Chuo Bingwa 1,000,000/= mshindi wa pili 600,000/= na Chuo cha tatu 400,000/=. Kwenye mchezo mmoja mmoja mshindi atajipatia Tsh. 200,000/= wa pili Tsh. 150,000/= na wa tatu Tsh. 100,000/= yote ni kwa wanawake na wanaume na pia Mchezaji bora wa kike na wa kiume kila mmoja atapata 50,000/= huku Chuo bingwa kikijipatia Kombe kubwa la Safari Lager2010.”

Wakielezea juu ya uthamini huo wawakilishi wa vyuo hivyo wakiongozwa na Naibu Waziri wa Michezo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bwana Kayumb Torokoko alisema “Udhamini huo umefika wakati muafaka kukokana na ukweli kwamba mchezo wa pool ni miongoni mwa michezo inayohitaji matumizi makubwa ya akili na kufikiri tofauti na michezo mingine ambayo hutumia nguvu zaidi.”

Aliendelea kusema “Ni nafasi nzuri kwa wanataaluma kote nchini kushiriki katika mashindano hayo ili kuweza kutoa nafasi kwa kila mmoja wetu kuonyesha uwezo wake kwenye kucheza pool.

Aidha waliipongeza TBL kwa mchango wake wa dhati kwa mchezo huu kwa kusema “Tungependa kutoa shukrani zetu kwa bia ya Safari Lager na TBL kwa ujumla kwa mchango wao katika kuhakikisha mchezo huu wa Pool unakuwa na kuomba waweze kutoa nafasi ya kuukuza zaidi kwenye vyuo vilivyopo nje ya jiji na Dar es Salaam.

Wamekuwa ni mfano mzuri kwa kuweza kuutambua mchango wetu katika ngazi ya vyuo vya elimu ya juu nchini na pia kutoa ushirikiano mkubwa katika mchezo huu, na hivi leo mchezo wa Pool umekuwa na taswira tofauti na yenye matumaini makubwa kwenye ngazi ya vyuo vya elimu ya juu nchini Tanzania.”

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ni watengenezaji na wauzaji wa bia, vinywaji vya matunda vyenye asili ya kilevi (AFB’s) na visivyo na kilevi ndani ya Tanzania. TBL inazo hisa pia katika Tanzania Distilleries Limited na kampuni shirika, Mountainside Farms Limited.
Bia maarufu za TBL ni pamoja na Safari, Kilimanjaro, Ndovu Special Malt na Castle.Vinywaji vingine vya TBL ni Konyagi Gin, Amarula Cream, Redds Premium Cold.

TBL imo pia katika Soko la Hisa la Dar es Salaam na imeajiri watu kiasi cha 1,300 huku ikiwa na wawakilishi katika sehemu kubwa na Tanzania na viwanda vitatu vya bia na depot nane kwa ajili ya kusambazia bia na vinywaji vingine vya kampuni hiyo.

Kwa mawasiliano zaidi
Fimbo Butallah,
Safari Lager Brand Manager,
Fimbo.Buttallah@tz.sabmiller.com

Dorris Malulu,
Corporate Affairs Administrator,
Doris.malulu@tz.sabmiller.com

Innocent Melleck,
Integrated Communication Ltd,
Project Manager,
+255 786 110 150
innocent@integrated.co.tz

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Safari Lager imebadilisha walengwa na imeanza kuingilia soko la Kili na Ndovu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...