Hawa ndio mashuhuda watatu kati ya wanne waliotaka kusahaulika wa Muungano. Hawa ndio waliobeba vibuyu na chungu wakati wa tendo la uchanganyaji udongo lililofanywa na Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Aman Karume katika picha hii hapa chini.
Nao ni toka shoto ni Bi. Sifaeli Shoma, ambaye ndiye aliyebeba kibuyu kilichokuwa na udongo wa Tanganyika na kumkabidhi Mwalimu Nyerere tayari kwa zoezi la kuunganisha nchi hizo mbili,
Bw. Omar Hassan Mzee Huyu alibeba chungu kikubwa kilichotumika kuchanganyia udongo wa Zanzibar na Tanganyika ambapo baada ya uchanganyaji udongo huo, ndipo lilipozaliwa taifa jipya la Tanzania.
Khadija Rajabu Abass Alibeba kibuyu kilichokuwa na udongo wa Zanzibar na kumkabidhi Rais Karume wakati huo ili aweze kushiriki vema katika zoezi la kuunganisha Zanzibar na Tanganyika na wakati huo alikuwa na umri wa miaka 16, akiwa mwanafunzi wa Sekondari ya wasichana ya Towa.


POLE NA KAZI ANKALI NA TIMU YAKO NZIMA YA WANALIBENEKE MIMI NAPENDA TUU KUZIPONGEZA HIZI NCHI ZETU MBILI KWA KUENDELEZA MUNGANO WAO,PIA MUUNGANO UNDELEE KUDUMU NA KUKAKA MAA SIKU ZOTE KWA PAMOJA TUNAENDELEZA LIBENEKE YA GLOBU YA JAMII.


MDAU WA HABARI POPOTE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. EBU ZITAFUTE HABARI KAMILI ZA HAWA WATU UTULETEE HAPA, WAKO NA WANA FANYA NINI SASA, NA MAISHA YAO YALIENDELEAE HADI SASA? NI HISTORIA NZURI KUIFAHAMU, AU KAMA UNAWEZA KUWAPATA NA KUWAHOJI NA KUTULITEA KIDEO HAPA KUPITIA YOU TUBE.

    ReplyDelete
  2. Nilipokuwa mtoto, nilidhani Nyerere ana kilema cha mikono. Nilikuwa siilewi kabisa hii picha

    ReplyDelete
  3. HIVI MICHUZI HUO UDONGO SASA HIVI UKO WAPI? MAKUMBUSHO AU?

    ReplyDelete
  4. ukweli usemwe ilivyo takikana haswa huu udongo ulikuwa uchanganywe na viongozi wote wawili wakiwa kila mmoja kashika kibuyu chake. ndipo ingeleta picha kamili, lakini hewalwa ndo muungano.

    ReplyDelete
  5. mdau wa kwanza naungana na wewe ni vizuri tukajua historia ya hawa watu, i hope sio walala hoi kwani kwa tendo la historia kama hii wangetakiwa wawe watu wa juu zaidi ya wote waliopo madarakani.

    ReplyDelete
  6. Kweli Nyerere alikuwa ndio mpishi mkuu wa Muungano! Karume anaangalia tu Mwalimu akichanganya 'madawa'. Nina hakika udongo wa kutoka upande wa Zanzibar haukutoka Pemba huo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...