Nao ni toka shoto ni Bi. Sifaeli Shoma, ambaye ndiye aliyebeba kibuyu kilichokuwa na udongo wa Tanganyika na kumkabidhi Mwalimu Nyerere tayari kwa zoezi la kuunganisha nchi hizo mbili,
Bw. Omar Hassan Mzee Huyu alibeba chungu kikubwa kilichotumika kuchanganyia udongo wa Zanzibar na Tanganyika ambapo baada ya uchanganyaji udongo huo, ndipo lilipozaliwa taifa jipya la Tanzania.
Khadija Rajabu Abass Alibeba kibuyu kilichokuwa na udongo wa Zanzibar na kumkabidhi Rais Karume wakati huo ili aweze kushiriki vema katika zoezi la kuunganisha Zanzibar na Tanganyika na wakati huo alikuwa na umri wa miaka 16, akiwa mwanafunzi wa Sekondari ya wasichana ya Towa.

MDAU WA HABARI POPOTE
EBU ZITAFUTE HABARI KAMILI ZA HAWA WATU UTULETEE HAPA, WAKO NA WANA FANYA NINI SASA, NA MAISHA YAO YALIENDELEAE HADI SASA? NI HISTORIA NZURI KUIFAHAMU, AU KAMA UNAWEZA KUWAPATA NA KUWAHOJI NA KUTULITEA KIDEO HAPA KUPITIA YOU TUBE.
ReplyDeleteNilipokuwa mtoto, nilidhani Nyerere ana kilema cha mikono. Nilikuwa siilewi kabisa hii picha
ReplyDeleteHIVI MICHUZI HUO UDONGO SASA HIVI UKO WAPI? MAKUMBUSHO AU?
ReplyDeleteukweli usemwe ilivyo takikana haswa huu udongo ulikuwa uchanganywe na viongozi wote wawili wakiwa kila mmoja kashika kibuyu chake. ndipo ingeleta picha kamili, lakini hewalwa ndo muungano.
ReplyDeletemdau wa kwanza naungana na wewe ni vizuri tukajua historia ya hawa watu, i hope sio walala hoi kwani kwa tendo la historia kama hii wangetakiwa wawe watu wa juu zaidi ya wote waliopo madarakani.
ReplyDeleteKweli Nyerere alikuwa ndio mpishi mkuu wa Muungano! Karume anaangalia tu Mwalimu akichanganya 'madawa'. Nina hakika udongo wa kutoka upande wa Zanzibar haukutoka Pemba huo!
ReplyDelete