Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Netiboli Tanzania Shy-Rose Bhanji na viongozi wengine wakiagana na kocha wa timu ya Netiboli Tanzania bara 'Taifa Queens" Mary Protase na wachezaji wa timu hiyo waliokuwa wakielekea nchini Uingereza kwa mwaliko wa wiki mbili ili kupata mazoezi na kujipima nguvu na timu za huko. Timu hiyo iliondoka leo na Shirika la Ndege la Emirates katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julias Nyerere jijini Dar. Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Netiboli Tanzania Shy-Rose Bhanji na viongozi wengine wakiagana na kocha wa timu ya Netiboli Tanzania bara Mary Protase na wachezaji wa timu hiyo waliokuwa wakielekea nchini Uingereza kwa mwaliko wa wiki mbili ili kupata mazoezi ya kujipima nguvu. Timu hiyo iliondoka jana na Shirika la Ndege la Emirates katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini DSM.
Viongozi wa chama cha mpira wa netiboli wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya mpira wa netiboli ya Tanzania Bara mda mfupi kabla ya timu hiyo kuendelea nchini Uingereza.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Duuh!!!! hawa mechi watachezea wapi twende kuangalia-sisi tumesahaukama mchezo wa netballbado upo

    ReplyDelete
  2. tusubiri habari ni wangapi watajichimbia hahaha hahaha!

    ReplyDelete
  3. hongereni sana uongozi mpya wa chama cha netiboli, jitihada zenu tunaziona!

    ReplyDelete
  4. KWELI KABISA , UONGOZI MPYA UNAOKANA UNA JITIHADA FULANI.NI NADRA SANA KUTOKEA TIMU KUPELEKWA KUPATA MAFUNZO ULAYA. HIYO NDIO FAIDA YA MABADILIKO.
    HONGERENI AKINA SHY-ROSENA WENZIO.

    mZOZAJI

    ReplyDelete
  5. Hizi netball ipo UK pia. Nilizania ni mchezo wa Tanzania tu au labda East Africa tu?

    Sikujua hilo...

    ReplyDelete
  6. watanzania tuonyeshe mapenzi katika mchezo huu wa netball kama ilivyo kwa soka

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...