Marehemu Mzee Joseph Lebulu Mushi wakati wa uhai wake


Ndugu Victor Joseph Lebulu wa Tegeta,Dar es Salaa.anasikitika kutangaza kifo cha baba yake mzazi,Mzee Joseph Lebulu Mushi kilichotokea jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Moshi kwa mazishi inafanywa nyumbani kwa mtoto wa marehemu Tegeta,Dar es Salaam.Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili mpaka hapo utaratibu wa kusafirisha utakapokamilika.


Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki woote popote pale waliko.


Kwa taarifa zaidi wasiliana na:-
Victor Joseph Lebulu:
kwa namba hizi 0784/0655 721 003

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU PAHALA PEMA PEPONI
– AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mungu ailaze roho ya mzee lebulu pema peponi. Kwadeni sana womi sha mangi esho.Kullaya uk

    ReplyDelete
  2. Michuzi I wish ungekuwa umemjua huyu baba wakati wa uhai wake. Alikuwa mtu anapenda watu sana, na alithamini utu. Ni msiba ambao haugusi tuu familia ya Lebulu, bali wakibosho wengi - matajiri na maskini.

    Nakumbuka alikuwa na Toyota Stout yake ya ranfi ya njano miaka ile ya sabini na mwanzo ya miaka ya themanini. Usafiri huu ulisaidia sana kusafirisha abiria kutoka Kibosho Uchau kupitia Kibosho Nkoring'a - Kirima Juu- kwenda mjini Moshi.

    Wakati huo kulikuwa na shida kubwa sana ya usafiri kibosho kwani mabasi yalikuwa machache sana.

    Yeye alipenda sana kusaidia akinamama maskini, na hasa wale waliokuwa wanakwenda kulima mashamba yao maeneo ya Sangiti na Maili Sita. Siku moja aliijaza ikapata pancha mara nyingi tuu, lakini alijitahidi wote tukaweza kufika makwetu salama.

    Nakumbuka sana upendo wake na Mungu ampumzishe salama. Ana klabu yake ya Mbege pale nyumbani ambayo inashika chati katika kutengeneza mbege yenye viwango. Poleni sana Akina Victor na ndugu wote.

    DEO MUSHI wa Daily News

    ReplyDelete
  3. Pole sana wafiwa, namwomba Mungu awazidishie nguvu na imani mvuke kipindi hiki kigumu. Pia tuongeze maombi ili Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi. Joseph, CHN.

    ReplyDelete
  4. poleni sana familia ya joseph lebulu.kwade paul,sitasahau tulivyokuwa tunapata lift ya pick kwenda nsoo sec,mzee akitushusha kirima.

    ReplyDelete
  5. Tunawapa Pole kwa Msiba wa Baba. Ms Thresia Pole sana na pia familia yako.
    Ee Bwana Umaptie Mwanga wa Milele.
    NEw York City.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...