Leo tarehe ya ishirini na sita ya mwezi wa Aprili mwaka elfu mbili na kumi (26 Aprili 2010), tumeadhimisha miaka arobaini na sita (46) tangu Waasisi wa Mataifa haya mawili yaani, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa iliyokuwa Tanganyika na hayati Abeid Amani Karume wa iliyokuwa Zanzibar, wakiri mbele ya kadamnasi kuwa nchi mbili hizi sasa zimeungana na kuunda Jamhuri ya Tanzania na hivyo kuwaunganisha wananchi hawa kuwa Taifa moja.

Maadhimisho ya sherehe hizo yalijumuisha pia vikundi vya burudani, na kama kawaida mara baada ya shughuli ya makundi mbalimbali ya Jeshi kukamilisha shughuli zao, Halaiki ya Vijana ilikuwa kivutio kikubwa.

Kwa sisi tuliofuatilia kwa njia ya redio, tulifaidi kusikia ujumbe wa Mrisho Mpoto, Nyimbo za Ngoma na nyimbo za Vijana wa Halaiki 'Tanzania Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote' na mwingine mpya ambao jina lake rasmi sijalifahamu, lakini wasema, 'Ni furaha kuzaliwa Tanzania', ukipenda kusikiliza haya yote, tafadhali bofya linki hiyo --> http://bit.ly/8X3QMS

Subi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. SUBI HATUPATI HIYO KITU UMETUWEKEA HAPA, IT SEEMS AS IF THERE WERE SOME ERRORS IN LOADING IT, IS NOT IT? TUJARIBIE KUTULETEA TENA AMA TUHABARISHE VINGINEVYO.

    ReplyDelete
  2. Nimemsikiliza Mpoto! He is just a brilliant artist..!

    ReplyDelete
  3. Kaka hebu tuweke sawa hapo umeandika "ilyokuwa Zanzibar" maana kitu kilikuwepo na sasa hakipo tena, lakini Zanzibar bado ipo.

    ReplyDelete
  4. yani wazanzibar wamekaa urojo urojo

    aggggrrrrrrrrr

    ReplyDelete
  5. Nenda Wavuti
    http://www.wavuti.com
    Utaipata



    B. Kimbache
    Kipatimu-Kilwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...