Uncle Michuzi,
I have to congratulate you for keeping Libeneke moving.

We have the below vacancies for well qualified and experienced people:-
1. Database Administrator (2)
2. Systems Administrator (2)
3. Hardware Engineers (10)

Please Email us your Resume/CV with 2 referees and all will be called for the Interview

Women are highly encouraged to apply
Deadline is 21st April 2010

Quality Systems (T) Limited
eMAIL: qstzltd@yahoo.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Du..!! , hii kampuni ina email ya yahoo. Naogopa kupeleka CV

    The Kalija

    ReplyDelete
  2. Ankol, mara nyingi nishatuma post zangu hapa na unazibania, lakini ninahakika msemo wangu huu unaukumbuka, maana kila nikiaandika nautumia. Hii ni blog yako na ni uamuzi wako unayoweka hapa, lakini ningelikushauri uwe makini na matangazo mengine.

    Ni vizuri basi kwanza ungelikuwa unafanya utafiti mdogo tu wa matangazo kama haya, sio vizuri kuwapa vijana tamaa ya kuwa kuna kazi kumbe ni uongo mtupu.

    sisemi kuwa hii kampuni ni ya uongo lakini inashangaza kuwa kampuni yenye nafasi kibao namna hiyo na ina email ya yahoo? Kampuni hata zilizo kuwa ndogo basi zinakuwa na email za uhakika, seuze hii ambayo inasema ni ya IT.
    isitoshe na kiingilishi kinachemsha na nafasi ni kibao hivyo na ameshindwa hata kusema ni sifa gani anatafuta kwa muombaji?

    Ankul tunaomba utuulizie zaidi kabla hatujatuma cv zetu.

    ReplyDelete
  3. hii kampuni ni ya kweli ankal? au tunafanyiana joke hapa? hapajeweka requirements za muombaji, hakuna jina la mtu tukaweza kumu-address katika email, email yao ni yahoo, wanatafuta wafanyakazi 14 kwa mpigo? nina wasi wasi sana.

    ReplyDelete
  4. mbona taarifa haipo kamili,toa vigezo basi vya hao watu unao wataka.
    kama ni database adm ni mysql,Ms-sql or oracle?
    na system adm wa nini?windows or Linux?lete kitu kimekamilika!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. Sio tu kuwa wana email ya yaho, ila mtumaji naonakatoka usingizini katuma tangazo. hizo kazi zote alizotuma zina specialisations...sasa utasema hardware tu au system administrator? wa windows, version gani, unix/linux, flavour gani. tangazo la ajabu.

    ReplyDelete
  6. brother michuzi, unazo details zaidi za kampuni hii? jee unajua lolote kuhusu kampuni hii, nauliza kama tahadhari kabla sijatuma cv yangu. wasi wasi wangu ni kuwa kampuni sijaona website yao na mtangazaji anatumia yahoo address. labda ndio kwanza inaanzishwa, ikiwa ni hivyo ni vizuri tukaelezwa mapema ili tusifikiri ni kanyaboya.

    ReplyDelete
  7. HAMNA PESA, VIMISHAHARA VYENU MBUZI SANA. HAOMBI MTU

    ReplyDelete
  8. Hii Kampuni itakuwa ni ya kubeba mabox maana huyo anayetafuta wafanyakazi naona hajui anachotafuta. Cha msingi tu awe serious na tangazo lake. Kutumia e-mail ya yahoo sio ajabu tumeona Wizara ngapi zinatumia yahoo domain? hata Ikulu waliwahi kutoa Id yao kwenye domain ya yahoo.

    ReplyDelete
  9. haikukaa sawia hii. Kiingilishi kimenitia wasi wasi, pia ni ahadi gani ya kuwa kila atakayepeleka cv yake ataalikwa kwenye intavyuu?

    hivi kweli kama watu zaidi ya mia wakileta cv zao utawaita wote kweli? hakuna shoti listi kabisa? sijapatapo kuona kuwa watu kuitwa katika intavyuu kwa sababu tu wamepeleka maombi yao, daima watu hutizamwa elimu yao na expiriansi yao kama ziko sambamba na nafasi zilizotangazwa.

    Jengine nafasi za kazi zinatangazwa lakini hapajatajwa sifa za muombaji, hii pia imenitia wasi wasi.

    ReplyDelete
  10. 'all will be calledfor the interview'

    hii ahadi in matatizo sana.

    kwanza inakuwaje uwape waombaje wote interview wakati watakuwepo amabao hawa qualify, why waste their time and your time na wasio na sifa ili mradi wame apply.

    kwa nini 'the interview' kwani kila muombaji hana interview yake?

    You need to hire pro wa HR and Recruitment, nyinyi focus with what you do best.


    (US Blogger)

    ReplyDelete
  11. Au anamaanisha kuwa hao ma-referee ndio wataoitwa for intavyu? Sa si angeandika "both" na si "all"? Halafuuu, ni referee ama references? Au yote A na B ni sawa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...