Ankal naomba uwekee hii habari kwa faida ya wengine.
Jana nilienda kutibiwa pale Regency Hospital Mida ya saa 10, bahati mbaya nikakosa parking space kwenye parking ya hospital, hivyo nikalazimiaka kuweka gari langu kando ya ukuta wa DIT, Dakitari alichelewa kidogo kwahiyo mpaka napata huduma ikawa mida ya saa moja, Lahaula nikakuta wameng"oa vioo vya mbele.
Pia muelewe hivyo vioo vilikuwa vimendikwa namba ya gari, wengi walikuwa wanaamini kwamba ukishaweka namba kioo hakiibiwa, It has proved wrong! Nilienda kituo cha police kilichoko mkabala na regency hospital. Nikarudi kwa askari aliyekuwa analinda pale nje ya hospital akasema wao ile haiwahusu kabisa! eti ni nje ya lindo lao!.
Jamani mnapokuwa pale muwe waangalifu, ita ni cost elfu 70 kurudishia maana mimi sinunuagi vitu vya wizi!!!

Mdau Aliyelizwa
Ulienda kunini huko regency? Pole kwa kulizwa.
ReplyDeleteNILIENDA KUTIWA PALE REGENCY HOSPITAL jamani kiswahili kigumu!!!!!!!!
ReplyDeleteAnkal tafadhali uwe ukipitia maoni kabla yakuyarusha hewani, naomba wananchi mchukulie kama typing error acheni kuhighlight bwana, nawewe mtu kua makini soma kabla yakutuma au ni panic?
ReplyDeleteHivi ulienda kufanya nini hapo hospitali? huyo daktari nae mapozi, kwanini alichelewa kuja kukutia?
ReplyDeletePole mdau kwa kulizwa. Siku ukiibiwa spare ambayo haipatikani kirahisi Tz then najua uta opt kununua tu vya wizi.
ReplyDeletepole mdau. mie vyangu vya noah washaiba sana mpaka nimechoka. nilichofanya, wkt wa kufitisha kipya nakivunja kidogo pembeni mradi niweze kuangalia, wala hawajarudi tena. dawa ya kukomesha ni kununua kingine kipya na si kuwafuata gerezani maana wanajiona wafalme.....
ReplyDeleteHongera kwa kutokununua vya wizi. Ama kweli kununua vya wizi ni kuwapa soko wezi ili wazidi kuiba na kuzingusha. Kama wote tungekuwa kama wewe ingependeza. Wizi ungepungua kama si kuisha. Mwizi asingeiba kwa vile asingepata soko hata kama angeiba.
ReplyDeleteNAFIKIRI ULIKUSUDIA KUTUAMBIA 'ULIENDA KUTIBIWA'. MAANA KISWAHILI CHA KWENDA KUTIWA HOSPITALI HATUKIELEWI, HATA HIVYO POLE KWA KUUMWA NA KUIBIWA, NA HONGERA KWA KUTUTAHADHARISHA, NA MUNGU HUENDA AKAKUPA NAFUU KWA MATIBABU HAYO NA AKAKUFIDIA HASARA ULIOPATA.
ReplyDeleteKumbukeni kutonunua vya wizi si suluhisho, kwani msiponunua kwao wanaenda kumuuzia muhindi then ukienda dukani unakutana nacho tena. hata hivyo pole sana ndugu yangu
ReplyDeletepole sana mdau -mwenzako sina hamu na vitara kabisaaaaaaa nimezikchukia sana na zinanitia kichefuchefu! nikiwa home nimelala walianza na distribuita taa zote power windo mziki na spika zote! nikaenda gerezani nikauziwa vile vile vya kwangu siku ya nne kontroo box loo nilikaa juu ya mawe wiki nikaenda nunua nyingine nahisi ilikuwa yakwangu tuu nikaamua kuuza na gari kabisaa kwa bei ya kutupa manake niliona sasa watakuja kulibeba kabisaaaa nachukia vitara saana yani wezi ni mbwa sana kazi kurudisha maendeleo ya wenzao nyuma ndo mana watu wanakuwa na hasira kali hadi wanaamua kuwakaanga!
ReplyDeleteHuo mchezo wa kuibiana vioo hata hapa USA upo sijui ni state zote ama ni huku ninakoishi tu. Wee utaponea na elfu 70 tu mimi ilinicost $399 plus tax and shipping charges roho iliniuma sana. Nafanya kazi downtown ndio maana walikwapua side mirror halafu nikaenda kwenye junk yard kununua sikupata kwa vile gari langu wakati huo niliambiwa bado ni "new model" hivyo magari ya hiyo model bado mengi yalikua hayapata ajali yakawa written off na kupelekwa huko kwenye junk yard na marekani spare za gari ni heri kununua gari jipya...Kitu kidogo tu unachrgiwa so much.
ReplyDeleteInauma sana sana sana
We una pesa bwana unatiwa Regency Hospital, una mkoko wa nguvu, Sasa elfu sabini unalalamika nini!!
ReplyDeleteYale yale!
ReplyDeleteNatumaini wanaougulia hiyo typing error ni wavulana wanaobalehe na wasichana wanaovunja ungo!
Ndo kilema kinaanza hivyo hivyo, hutaki kuangalia point una....
JAMANI HIYO KUTIWA MBONA MIMI SIONI KWENYE HABARI HII AU MNAOTA NINI?
ReplyDelete