Bro Michuzi,
Tafadhali saidia kuirusha hii picha mtandaoni kufikisha kero ambayo wananchi tunaipata kwa watu kutofanya kazi zao inavyostahili.Huu ni mfano mmojawapo tu!

Hivi ni nani mwenye mamlaka ambaye anaruhusu vibao vya biashara vinavyowekwa kiasi cha kama mita 3 tu toka usawa wa ardhi na kusababisha madereva kushindwa kuangalia 'comfortably' magari yakayotokea upande fulani wa barabara kabla ya wao kuingia barabarani?

Hii inahatarisha usalama barabarani. Hapa ni maeneo ya Oysterbay karibu na TTCL, lakini huu ni mfano tu, matatizo haya yapo sehemu nyingine nyingi tu na katika idara nyingine nyingi tu, na ni vitu vidogo kama hivyo tunapo vidharau, kwenye kwa ujumla wake vinaturudisha nyuma kimaendeleo. Nitaendelea kukutumia picha hizi uzirushe, labda wahusika bado hawajatambua makosa yao hivyo watatambua na kurekebisha.

Asante Ankal
MDAU OSTABEI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Asante mdau kwa kulirusha hili. Kama kumbukumbu yangu iko sawa hapo ni kona ya Haile selasie na Karume mkabala na TTCL na Oysterbay Shule ya Msingi. Mimi mwaka 2006 nikitoka ofisini hapo TTCL niliwahi kugombana na jamaa moja ambaye alikuwa amepaki hapo akiongea na mwenzake(mwanamke) ambaye nae alikuwa amepaki gari. Na wakati huo hayo mabango hayakuwepo kabisa. Kama unatokea mtaa wa Karume huwezi kabisa kuona gari ambalo linatokea Saint Peters. Nilijaribu kulifikisha kunakohusika lakini ndo yaleyale unampigia mbuzi gitaa. Ajabu ni kwamba mtaa huo huo ndio unaotumiwa na Makamu wa Rais wakati akitoka na kurudi nyumbani. Kwa kuwa yeye anapita na msafara hawawezi kabisa kuliona tatizo hilo. Kweli Bongo tambarare.

    MDAU USA.

    ReplyDelete
  2. kwa kuwa umeanza wacha na mimi ninene kwa lugha .
    kuna ajali nyingine watu wa jiji wanafaa kulaumiwa.
    mimi nashangaa barabara kubwa kukosa ZEBRA CROSSING na kuwekwa miti mirefu katikati ya barabara.
    sina taswira ya barabara ya mandera kwa sasa, ila kwa miaka niliyokuwa home, sehemu kibao ambapo kuna crossing, hakuna alama za crossing... mfano mzuri, mabibo hostel, river side, external, garage, relini ..... na barabara ilijaa miti katikati mirefu ambayo tabu kwa wavuka barabara kutizama upande wa pili wa barabara kabla ya kuvuka.
    mko wapi watu wa jiji ?
    serikali yetu iko wapi jamani ?

    aaaaaaaaaaaaaagh @#@$$#@##@#@ !

    Mdau No 5 .

    ReplyDelete
  3. Tunashukuru mdau kwa hii habari,maana wenzetu kama wa mji wa houston na mingineyo mabango yameshushwa/yametolewa yote maana acha kuwa ni hatari kwa madereve,kuharibu uonekano wa mazingira ni polution pia.

    ReplyDelete
  4. Katika nchi ya kifisadi,kila mtu anajali tumbolake. Sheria hazifuatwi hata kama zipo, who cares? Mdau Utajiju!

    ReplyDelete
  5. Wadau mezeeni hamuoni hapo kati ya mabango kuna bango la mdhamini wetu mkuu wa Globu ya jamii?? Mnataka tukale wapi jamani..??

    Glober

    ReplyDelete
  6. Mapedestrian wala hatushtukiagi mambo hayo.

    ReplyDelete
  7. Sisi wakatiza mbuga huwa hatusumbuliwi na mabango.

    Magari ya nini wakati miguu unayo?

    Bongo tambarare.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  8. BONGO HAKUNA SHERIA HUKU USA NI MARUFUKU MABANGO KAMA HAYO BARABARANI KAMA UNAENDESHA UTAKUTANA NA ROAD SIGNS ONLY KAMA SPEED LIMIT,ONE WAY,NO U TURN NK

    ReplyDelete
  9. ni kweli hayo mabango yanamfanya dereva asiweze kuyaona magari,mwendesha baiskeli/pikipiki/msukuma mkokoteni na hata mtembea kwa miguu,hata walioko main road hawawezi kuyaona magari yanayo aproach at the junction! kwanamna hiyo ni rahisi mno kutokea ajari maeneo kama haya,hayo mabango yangesogezwa mabli kutoka barabarani pia hiyo barabara haina michoro inayotenganisha lanes wala inayoashilia junction ahead ukikama ni new driver utastukia unaingia main road bila kufaham ni hatari!ukizingatia tunalipa road tax daily.

    ReplyDelete
  10. bango la mdhamini mkuu wa libenee liko poa ni lirefu hayo mengine ni viandunje na ndo yanaleta hatari hapo

    ReplyDelete
  11. Kuna vibao vingine barabara ya garden road mitaa ya mikocheni, unapotoka Kwenye nyumba za mawaziri kuingia garden road upande wa kushoto kwako kuna vibao vinakuzuia kabisa kuona magari yanayotoka upande wa rose garden hadi uingize pua kidogo barabarani!! manispaa ya kinodndoni sijui wanafanya nini kwa sababu kuna sheria kabisa inayoelekeza jinsi ya kuweka mabango barabarani

    ReplyDelete
  12. acha kuumiza kichwa subiri maafa yatokee ndipo uone viongoz wanapojitokeza kuuza sura kwenye TV wakijifanya hilo tukio limewakera saaaaaana na watahakikisha vibao vyooote visivyo na mpangilio vinatolewa.. zikipita siku tatu yaleyale... ha ha ha bongo tambarale


    MDAU KUTOKA UKANDA WA GAZA
    TARIME

    ReplyDelete
  13. nimekoswakoswa mzinga jana sehemu hiyohiyo...dah kwenye picha hii ndio naona kwanini jamaa hakuniona kama niko barabarani

    ReplyDelete
  14. Masahihisho wadau, Neno "mita 3" lisomeke "Futi 3", yaani ruler 3 hivi.

    Wadau mnaweza kuona kibao cha mdhamini kipo poa kabisa, labda utake kuangalia ndege angani, japo kama wasemavyo wadau wa ng'ambo kwamba huko vibao havitakiwi kabisa, huku tunalalamikia positioning tu.

    Kuna vingine kama vitatu hivi navyo nitawaletea... Cha serikali ya mitaa/ Mtendaji mitaa ya Oysterbay polisi ambaye tena yeye ndio alitakiwa asimamie haya; then kuna cha Chama cha walimu Tanzania mitaa ya Kinondoni baada ya kituo cha basi cha Kanisani.

    ReplyDelete
  15. Asante sana kwa mdau ulioleta hili. mimi nafanya shughuli zangu maeneo hayohayo ni kwamba kila baada ya wiki hakukosekani ajali kwa kiwango cha chini ni moja au mbili hivi na hapohapo ndipo mzee wa vijisenti alipowasulubisha wale kina dada wawili. tulijaribu kushauri eneo hilo liwekwe matuta lakini nasikia matuta hayaruhusiwi eneo analopita Makamu wa Raisi lakini sasa bora ni lipi waachwe watu wafe au makam wa raisi aende faster? kwa kweli hii sio fair serikali liangalieni hili

    ReplyDelete
  16. THAT IS OLD FASHION MARKETING AND PROMOTION, WHY DONT USE TV, RADIO, MAGAZINE, NEWSPAPER, VIBANDA VYA BUS STOPS, KWENYE MAJENGO. ACHANE KUWEKA MATANGAZO BARABARANI, BARABARANI HUWEKA ALAMA ZA KUMUUONGOZA DREVA AELEKEAKO SI MATANGAZO, KUNA INTERNET MOBILE PHONE WEKENI MATANGAZO HUKO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...