msaada wa haraka ukiendelea kutolewa ili kunusuru waliomo ndani ya gari hilo.
Kaka Michu habari za mchana,Pole na shughuli za kila siku ktk kuhabarisha jamii.Niko safarini natoka Singida kurudi jijini Dar,tumekutana na ajali mbaya sana maeneo ya Bwawani karibu kidogo na Moro.
Aboud Bus limepinduka hakuna aliyekufa ila watu wameumia sana na wengine bado wanaendelea kutolewa ndani ya Basi hilo wakiwa wamekatika baadhi ya viungo vyao.
Mdau,
Sent from my
BlackBerry® smartphone from Zain Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 22, 2010

    jamani hizi ajali vipi. kikwete tuongezee lane nyingine barabarani. looh jamani kwa mwendo huu sirudi tanzania

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 22, 2010

    AJALI AJALI AJALI!!!!
    Tanzania ajali zitamalizwa na nani??
    Mbinu gani itumike kupunguza hizi ajali za kila siku.
    Mungu Ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 22, 2010

    ...Wa Tz msirudi; Wakenya tuchukue nnji isiyo na mwenyewe!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 23, 2010

    Kulikuwa na mfululizo wa makala za mwananchi mmoja ajiitaye "Born Again Pagan" juu ya ajali Tanzania katika gazeti lilokufa la KwanzaJamii...lakini maoni hayakufa!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 23, 2010

    Poleni sana wahanga. Madereva muendeshe kwa usalama, abiria muache kuchochea madereva waongeze speed, bora kuchelewa lakini mtu ufike salama, kulikonia hivi. Pia, lanes inabidi ziongezwe kwa kweli, tena zitenganishwe kabisa (sio kuchora mstari mweupe tu katikati ya barabara - kama upo), za wanaokuja na wanaorudi, kama jinsi ilivyo Morogoro Road ama Ally Hassan Mwinyi Road (kuanzia pale Morocco hadi Palm Beach nadhani).

    ReplyDelete
  6. MwananchiMay 23, 2010

    Hapo mahali panateleza sana hapo.

    Mshua wangu ameshawahi kujibwaga na Hilux Double Cabin pickup yake hapo. Bahati hakuumia wala kupoteza maisha.

    Nasikia hapao ama palimwagika diesel au lami yake wameweka laini.

    Na magari yanajibwaga kila siku lakini serikali wala haijishughulishi kubadilisha hiyo lami.

    Labda mpaka wajibwage wenyewe wakati wanaenda Bungeni ndio watastuka na kubadilisha hiyo lami.

    Khaah!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 24, 2010

    wameanza kutoa watu kafara kama kawaida yao na uchaguzi umekaribia!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...