, WAREMBO watakaoshiriki shindano la RBP Miss Dar Intercollege mwaka 2010 (pichani) kesho wataipa nguvu timu ya Taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’ katika mechi yao dhidi ya Eritrea itakayopigwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mratibu wa shindano hilo,Silas Michael warembo hao watahudhuria mechi hiyo kwa ajili ya kuwashangilia ili kuwapa moyo Twiga Stars waweze kucheza kwa nguvu zote na hatimaye kuibuka na ushindi. Alisema hudhurio hilo ni sehemu pia ya mikakati ya mlezi wa timu hiyo,Mama Rahma Al Kharoos ambaye amedhamini shindano hilo aliyepanga kuipeleka Twiga Stars nchini Marekani mwezi juni kwa ajili ya kujinoa zaidi.

Shindano la Miss Dar Inter college linatarajiwa kufanyika Mei 27 kwenye ukumbi wa Club Bilicanas ambapo warembo 15 watapanda jukwaani kuwania taji hilo wakisindikizwa na wasanii wa bongo fleva Amin na Barnabas.

Aidha kampuni za RBP Oil Industrial Technology Tz Limited, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji cha Redd’s Orijino, Tanzania Daima, Vodacom Tanzania, Shear Illussion, Condy Bureau De Change, Ndege Insurance, Dotnata Decorations,Michuzi Blog,Mtaa Kwa Mtaa Blog,Full Shangwe Blog na Club Bilicanas wamejitokeza kudhamini shindano hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 22, 2010

    hivi hawa jamii yetu wapi tunaelekea....sitoshangaa baada ya miaka kumi ijayo tukawa na jamii ya vichaa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2010

    Tukimaliza hili shindano, tunamtafura Ms. Globu ya Jamii.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 23, 2010

    kwani mkivaa magaunu marefu ama macharanga mtapungukiwa nini?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 23, 2010

    Msaada kwenye Tuta:

    Najua ni jina salon / beauty shop tayari ila ni ipi ni sahihi kutokana na shughuli ziendeshwazo? Ni

    Shear Illussion

    Au ni

    Sheer Illusion

    Najua kuwa zote Shear na Sheer zina maana katika kiingereza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...