Asalam Alykum
Kaka Issa
Naomba uzimuvuzishe hizo picha za ajali niliyopambana nayo nikielekea Tanga sehemu iitwayo Hale. Ingekuwa vizuri wadau na ndugu jamaa na marafiki wa majeruhi kuweza kutambua rafiki zao Tuwaombee kwa Mungu waweze kurudi katika hali zao za kawaida Pia tushukuru Mungu hakuna aliyepoteza maisha zaidi ya majeruhi tu.

Ni dereva wa Haice mzembe alikuwa anataka kumpita wa hilo fuso bila kusoma nyakati na gari ilimshinda na kuivamia fusso kwa nyuma

Libeneke oyeee!
Mungu akupe afya njema uendelee kutuhabarisha ya ulimwengu
Ripota wa Globu ya Jamii Wajuu
Basi iliyopata ajali
wasamalia wakisaidia majeruhi
majeruhi wakisaidiwa
Askari walifika eneo la tukio chap chap





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. inasikitisha sana lakini pia nashauri upana wa barabara pia uongezwe maana huu tulionao ni ule ule wa land rover 109 sasa hivi magari ya uwezo zaidi

    ReplyDelete
  2. KalikaliMay 18, 2010

    Hii nchi sasa inahitaji sheria za Kichina. NYONGA HADHARANI madereva wa aina hii. Haki za binadamu ndiyo - lakini vipi haki za wale ambao wanakufa kwa uzembe wa hawa madereva? Vipi haki za watoto wanaokosa walezi baada ya baba/mama kufariki katika ajali za kizembe?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 18, 2010

    Sasa imefikia wakati abiri tuwe makini na wakali kwa hawa madereva wa kununualeseni,haiwezekani mtu mwenye dhamana ya roho zetu hata alama za barabarani hasizifahamu.
    Pili hata huyo mtu aliye kaa siti ya mbele ilipaswa amuonye dereva tena kwa kumnasa makofi ma2.ma3.

    Madereva wa abiria inapaswa wapimwe akili kabla hawajapatiwa hizo leseni.
    Vile vile abiria wapewe elimu ya kutoshajuu ya Usalama wao.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 18, 2010

    Bongo hatari na inasikitisha Jamaa kapata ajali anabebwa hovyo hovyo tu, inawezekana kavunja uti wa mgongo na kumchukua kwa style hii ndo kwanza unamalizia.

    Ama kweli bado safari ni ndefu tuendako. ni hayo tu.

    MDAU UKEREWE

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 18, 2010

    Sheria hazina maana bila kusimamiwa (enforcement). Hili ndio tatizo kubwa Tanzania. Vile vile barabara katika milima zinabidi ziwe pana, ili magari makubwa yapishe magari madogo kuovateki (crawler lanes). Barabar mpya zozote zinabidi zijengwe kwa kutilia maanani madereva wetu wa bongo! Ankal mimi hii ndio kazi yangu huku UK, yaanin Highway and Traffic Engineering. Inashangaza Serikali yetu haijatilia maanani jambo hili kama vile Malaria na Ukimwi. Hili ni janga la Taifa! Tunapoteza familia na jamaa zetu wasio na hatia. Jamani tuamkeni sio blah blah tu!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 18, 2010

    Most discrimination hotel in the city of Dar es salaam New Africa Hotel no respect to its loyal customers. A short lil flow manager was at level 8 i think they dumb him for his behaviour as well and he managed to transform same discrimination attitude to the new africa empire oh dear who will want such bad behaviour once he chose your hotel as a place to eat and drink and you want to em to pay you for get in ur one star hotel May God help you with all ya workers to get rid of that bad attitude which is nah our culture and norm in this heaven of peace TZEEE baby. Osheni nafsi zenu ubaguzi rudisheni kwenu sio Tanzania.
    Dissapointed loyal Customer(s)

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 18, 2010

    WAKUU ANGALIENI BARABARA HILIVYO NDOGO.KWANINI HAKUNA 2 LANES KWENDA NA 2 LANES KURUDI WAKATI NAFASI PEMBENI NI POLI TU? SERIKALI INAMAANA HAINA WATU WENYE AKILI YA KUJUA KWAMBA HIZI AJALI ZINATOKANA NA BARABARA KUWA NDOGO.


    TUNAWALAUMU MADEREVA NDIO LAKINI KWENYE PICHA YA JUU EBU JIULIZE UTAKAA NYUMA YA HILO LORI LA MAGOGO MPAKA WAPI? PEMBENI YA BARABARA NI POLI TUPU AMBALO LINGETUMIKA KUONGEZEA 2 LANES ZINGINE ZIKATUMIKA NA KUEPUSHA AJALI KILA SIKU WATU WANAKUFA BILA SABABU.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 19, 2010

    Jibu ni moja tu!

    Watumiweni Ma-Civil Engeneers waliotumiwa kujenga daraja la Umoja! Baaaas! Si wote mmelicheki jinsi lile daraja lilivyotulia? Full Kiwango!

    Wahanga, poleni sana.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 19, 2010

    na hayo magogo yanaenda wapi

    ReplyDelete
  10. KalikaliMay 19, 2010

    Wewe anonymous unayedai LANE 2. Kujenga lane 2 ni luxury kwa serikali masikini kama ya Tanzania. Kwa nini ujenge dual carriage wakati Arusha-Dar wakati Kigoma, Rukwa, Tabora, Ruvuma, Mtwara, Lindi hakuna hata hiyo ya LANE 1? Serikali haiendeshwi na watu wajinga kama wewe wasiokuwa na vipau mbele vyenye akili.

    Lane ni 1 lakini umewekewa alama kwenye barabara kwamba usi-overtake hapa. Sehemu ambayo ni salama ku-overtake pia alama zinaonyesha. Kwani kusubiri dakika 2-5 nyuma ya lori mpaka ufike sehemu ambayo ni salama na kuokoa maisha yako na ya watumiaji wengine wa barabara, wewe unaona ni ujinga? Basi huo wa kwako ndio ujinga.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 19, 2010

    Nyie mnaongelea upana mnakaa wapi, Tanzania au sayari nyingine? Unaongelea upana wa barabara 1 wakati barabara nyingi za vumbi hazipitiki! Mnashangaza sana Wabongo wengine. Hakuna kisingizio kwa kutofuata sheria za barabarani.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 19, 2010

    hao jamaa maaafande wananishangaza sana mimi yaani maana ata kwenye ajari ili kuchora mchoro wa tukio wanataka takrima wananikera sana maana washa wahi nitenda

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...