
Kaka Issa
Naomba uzimuvuzishe hizo picha za ajali niliyopambana nayo nikielekea Tanga sehemu iitwayo Hale. Ingekuwa vizuri wadau na ndugu jamaa na marafiki wa majeruhi kuweza kutambua rafiki zao Tuwaombee kwa Mungu waweze kurudi katika hali zao za kawaida Pia tushukuru Mungu hakuna aliyepoteza maisha zaidi ya majeruhi tu.
Ni dereva wa Haice mzembe alikuwa anataka kumpita wa hilo fuso bila kusoma nyakati na gari ilimshinda na kuivamia fusso kwa nyuma
Libeneke oyeee!
Mungu akupe afya njema uendelee kutuhabarisha ya ulimwengu
Ripota wa Globu ya Jamii Wajuu

inasikitisha sana lakini pia nashauri upana wa barabara pia uongezwe maana huu tulionao ni ule ule wa land rover 109 sasa hivi magari ya uwezo zaidi
ReplyDeleteHii nchi sasa inahitaji sheria za Kichina. NYONGA HADHARANI madereva wa aina hii. Haki za binadamu ndiyo - lakini vipi haki za wale ambao wanakufa kwa uzembe wa hawa madereva? Vipi haki za watoto wanaokosa walezi baada ya baba/mama kufariki katika ajali za kizembe?
ReplyDeleteSasa imefikia wakati abiri tuwe makini na wakali kwa hawa madereva wa kununualeseni,haiwezekani mtu mwenye dhamana ya roho zetu hata alama za barabarani hasizifahamu.
ReplyDeletePili hata huyo mtu aliye kaa siti ya mbele ilipaswa amuonye dereva tena kwa kumnasa makofi ma2.ma3.
Madereva wa abiria inapaswa wapimwe akili kabla hawajapatiwa hizo leseni.
Vile vile abiria wapewe elimu ya kutoshajuu ya Usalama wao.
Bongo hatari na inasikitisha Jamaa kapata ajali anabebwa hovyo hovyo tu, inawezekana kavunja uti wa mgongo na kumchukua kwa style hii ndo kwanza unamalizia.
ReplyDeleteAma kweli bado safari ni ndefu tuendako. ni hayo tu.
MDAU UKEREWE
Sheria hazina maana bila kusimamiwa (enforcement). Hili ndio tatizo kubwa Tanzania. Vile vile barabara katika milima zinabidi ziwe pana, ili magari makubwa yapishe magari madogo kuovateki (crawler lanes). Barabar mpya zozote zinabidi zijengwe kwa kutilia maanani madereva wetu wa bongo! Ankal mimi hii ndio kazi yangu huku UK, yaanin Highway and Traffic Engineering. Inashangaza Serikali yetu haijatilia maanani jambo hili kama vile Malaria na Ukimwi. Hili ni janga la Taifa! Tunapoteza familia na jamaa zetu wasio na hatia. Jamani tuamkeni sio blah blah tu!
ReplyDeleteMost discrimination hotel in the city of Dar es salaam New Africa Hotel no respect to its loyal customers. A short lil flow manager was at level 8 i think they dumb him for his behaviour as well and he managed to transform same discrimination attitude to the new africa empire oh dear who will want such bad behaviour once he chose your hotel as a place to eat and drink and you want to em to pay you for get in ur one star hotel May God help you with all ya workers to get rid of that bad attitude which is nah our culture and norm in this heaven of peace TZEEE baby. Osheni nafsi zenu ubaguzi rudisheni kwenu sio Tanzania.
ReplyDeleteDissapointed loyal Customer(s)
WAKUU ANGALIENI BARABARA HILIVYO NDOGO.KWANINI HAKUNA 2 LANES KWENDA NA 2 LANES KURUDI WAKATI NAFASI PEMBENI NI POLI TU? SERIKALI INAMAANA HAINA WATU WENYE AKILI YA KUJUA KWAMBA HIZI AJALI ZINATOKANA NA BARABARA KUWA NDOGO.
ReplyDeleteTUNAWALAUMU MADEREVA NDIO LAKINI KWENYE PICHA YA JUU EBU JIULIZE UTAKAA NYUMA YA HILO LORI LA MAGOGO MPAKA WAPI? PEMBENI YA BARABARA NI POLI TUPU AMBALO LINGETUMIKA KUONGEZEA 2 LANES ZINGINE ZIKATUMIKA NA KUEPUSHA AJALI KILA SIKU WATU WANAKUFA BILA SABABU.
Jibu ni moja tu!
ReplyDeleteWatumiweni Ma-Civil Engeneers waliotumiwa kujenga daraja la Umoja! Baaaas! Si wote mmelicheki jinsi lile daraja lilivyotulia? Full Kiwango!
Wahanga, poleni sana.
na hayo magogo yanaenda wapi
ReplyDeleteWewe anonymous unayedai LANE 2. Kujenga lane 2 ni luxury kwa serikali masikini kama ya Tanzania. Kwa nini ujenge dual carriage wakati Arusha-Dar wakati Kigoma, Rukwa, Tabora, Ruvuma, Mtwara, Lindi hakuna hata hiyo ya LANE 1? Serikali haiendeshwi na watu wajinga kama wewe wasiokuwa na vipau mbele vyenye akili.
ReplyDeleteLane ni 1 lakini umewekewa alama kwenye barabara kwamba usi-overtake hapa. Sehemu ambayo ni salama ku-overtake pia alama zinaonyesha. Kwani kusubiri dakika 2-5 nyuma ya lori mpaka ufike sehemu ambayo ni salama na kuokoa maisha yako na ya watumiaji wengine wa barabara, wewe unaona ni ujinga? Basi huo wa kwako ndio ujinga.
Nyie mnaongelea upana mnakaa wapi, Tanzania au sayari nyingine? Unaongelea upana wa barabara 1 wakati barabara nyingi za vumbi hazipitiki! Mnashangaza sana Wabongo wengine. Hakuna kisingizio kwa kutofuata sheria za barabarani.
ReplyDeletehao jamaa maaafande wananishangaza sana mimi yaani maana ata kwenye ajari ili kuchora mchoro wa tukio wanataka takrima wananikera sana maana washa wahi nitenda
ReplyDelete