Baada ya kazi kubwa ya kukonga nyoyo za washabiki wake Ali Kiba (shoto) leo jioni kaonelea lazima akajionee mwenyewe yanayojili Vincents Bar & Restaurant ambayo ndiyo Break Point ya Ukerewe katika mji wa Reading a.k.a Mji wa Kusoma. Hapa yuko na mwenyeji wake Ankal Gadol (wa pili shoto) na wadau wakijichana kama hawana akili nzuri vile...Libeneke Oye!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2010

    Ankal hizo sahani ni kubwa!! Duuu utafikiri za wabeba zege, inaelekea wabongo walilalamika sahani zilikuwa ni za kawaida ikabidi zitafutwe kubwa, kama huyo mdada atamaliza kweli msosi huo au atabeba kwenye lunch box?
    Na lunch sijui ni pounds ngapi ankal? Tupe bei ya mlo mmoja.
    Asante ankal kwa libeneke tupo mbele ya dunia habari zote kwa picha tunazipata!
    Ni mimi mdau wa Damu

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2010

    jamani wadau, reading panaonekana pazuri sana. natamani sana kufika hapo

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 04, 2010

    naomba kujua hiyo reading ni wapi?mnapoandika muwe mnaweka in bracket mfano dar( Tanzania) sio kila mtu anajua kila mahali, mfano leo ukienda china ukamwambia mtu nimetokea ilala hawezi kukuelewa mwambie nchi na mkoa. najua wengi hawapajui hiyo reading iko wapi, nawakilisha

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 04, 2010

    Wewe anony wa Tue May 04, 08:22:00 AM mbona unauliza majibu wakati umeambiwa ni UK-erewe na huo ni mji wa KUSOMA (Reading)... Karibu taratibu kwenye GLOBU (blog) hii ndio lugha yetu humu usiwe mkali utazoea tu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 04, 2010

    Mdau hapo juu, zoezi dogo la Copy and Paste kutoka Google unapata maelezo haya:

    Reading (pronounced /ˈrɛdɪŋ/ ( listen) RED-ing) is a large town in England, located at the confluence of the River Thames and River Kennet, and on both the Great Western Main Line railway and the M4 motorway, some 40 miles (64 km) west of London. For ceremonial purposes it is in the Royal County of Berkshire and has served as the county town since 1867.

    Reading was an important national centre in the medieval period, as the site of an important monastery with strong royal connections. Today it remains a commercial centre, with links to information technology and insurance. Reading also hosts two universities, a large student population, and is home to one of England's biggest music festivals.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 04, 2010

    mdau nami pia nakushauri kabla ya kuropoka na kuandika hapa kwanza soma vizuri post.

    post imesema ni ukerewe, jee hiyo haitoshi? au nawe hujui ukerewe ni wapi?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 04, 2010

    sasa mnaniponda nini nyie, kabebeni box huko

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 04, 2010

    Madu Hapo Juu,

    Karibu sana Reading. Hii ndio Dodoma ya United Kingdom.

    Hakuna mji nje ya Tanzania ambako ukienda utajisikia upo nyumbani kama Reading...Hakuna.

    Ni Reading peke yake ambapo ukienda Post Office unahudumiwa na Mtanzania, Ukipanda Bus linaendeshwa na Mtanzania, Ukienda Out kula kuna Restaurant ya Mtazania, Ukitaka kutuma Mizigo nyumbani Wakala ni Mtanzania, ukitaka Unga wa Sembe kwenye Mini Market mmiliki ni Mtanzania...duh..hata ukiugua ikabidi uende Hospitali huko nako Nesi wako utamkuta ni Mtanzania.

    Hapa ni Home Away From Home.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 04, 2010

    Huu ni mji ambao WaTZ (Bara na Visiwani) wanakula pamoja na mashekh Wanasali pamoja. Hapa hakuna udini wala Ukabila. Wachaga, Wahaya, Wapemba wote ndugu. WaTZ wajasirimali wanahudumia wananchi na hivi sasa tutagombea hadi udiwani. Mji Kusoma ndio mfano wa Disapora ya kweli, achana na wazembe wa miji mingine (Wanaendekeza kuchoma nyama tuu). Hapa ukitaka lolote kuanzia Mwanasheria, Madaktari, Wahasibu, Walimu wote wapo (to mention the few) Wote ni WATZ. Ankal, Uchaguzi ujao tutaomba tuwe na Mbuge wetu ili tuweze ku-deal na mafisadi vilevile. Kama hujaijua Reading boda tafadhali ingia kwenye Web... KARIBU MJINI KUSOMA....

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 04, 2010

    Wewe hapo juu unachanga Reading na Miji kama Leicester na North London. Huku watu wanatengeneza Pauni sio Umbea wala pesa za Queen. Waulize waliokuambia kwanza ndugu yangu. Huu ni mji Shule bwana sio mambo ya Kitchen Party! Huku hata Wapemba wanabeba Boksi sio mambo ya kulalala... Karibu mji Kusoma. Daima mbele

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 05, 2010

    haya sasa mara reading, sijui kusoma sijui box! mie simo! ushauri wangu ni kwa ali kiba: Hizo ziara unapata chochote kweli au UNAFURAHI KUPANDA NDEGE TU! BE CAREFUL KIJANA MAANA USANII WA BONGO HUCHELEWI KUISHA HALAFU WATU WAMEKULA KWAKO. USIDHANI WASANII WOTE HAWAWEZI KUJA HUKO, NI MASLAHI HAYALIPI TU! B CAREFUL BRO, KILA KITU KWENYE MAANDISHI USIJEKUISHIA KUWA GOLDEN GOOSE AU CASH COW KWA WENGINE WAJANJA. HEED MY ADVICE!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...