Habari ya leo ankal,
natumaini u mzima wa afya tele. Pole sana na kibarua kizito cha kufanya dunia kuwa kijiji. Ubarikiwe kwa hilo na Mungu akutie nguvu ili libeneke liendelee mbele.
Baada ya salamu ningependa unitundikie tujiombi twangu ili wana libeneke wanisaidie. ningependa kujua kama bongo kuna vyuo ambavyo wanatoa external degrees za uk au marekani katika level za shahada ya kwanza na masters katika fani za computer na management.
natanguliza shukrani,

Ni mimi mdau sambukile.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2010

    wee uko wapi, andika basi halafu tutakujulisha. Unaposema external programme una maana gani. External programme inapatikana sehemu yoyote. Kama upo bongo unaweza kusoma shahada yoyote ya Kompyuta na management. Lakini sema kama kuna sehemu ambazo wanatoa tution hapa bongo kuhusu hizo degree.

    Mjinga Nguruwe

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2010

    Vyuo vinavyotoa shahada za nje kwa pale Bongo viko kadhaa. Kwa haraka haraka nakumbuka IFM wanayo hiyo program na vya Uingereza na India. Vingine utavijua ukienda pale kuulizia zaidi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 04, 2010

    Kuna chuo kikuu cha Marekani, jina limenitoka lakini wana chuo chao pale Maktaba (UWT road zamani) ambapo unasoma miaka miwili halafu unamalizia miwili chuo chao huko Marekani (Iowa state). Bei yao ni kubwa lakini unapata shahada ya kwao na unaweza kuhamia chuo chochote marekani kumalizia Bachelor's degree kwa kuwa shahada yao ya miaka miwili (Associate degree) inatambulika Marekani.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 04, 2010

    Nadhani unazungumzia Waldorf college. Waldorf college imeuzwa mwezi wa kwanza kama sitakosea.. Hivyo kama hicho huko tanzania bado kipo watu waangalie wajue ni nini hatma yao kabla ya kujiunga au kama bado wakimaliza diploma zao zitakua credited sawa kama zamani....

    Kuna vyuo vingi vinavyotoa mazomo yao online ukijua kilicho halali ni cheaper sana tu na inakusaidia unafanya mambo yako na kusoma.....

    Mimi nafanya master na chuo changu hakiko mbali sana ila nimeamua kuchukua online courses na tunakutana mara moja kwa week tu. Muda mwingi ni teleconference na video conference lakini yote ni kwa skype tu...

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 04, 2010

    IFM wanatoa masters'ya IT na Business wakishirikiana na vyuo UK.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 04, 2010

    Nenda Learn IT mtaa wa Lumumba Dar es Salaam. Lipia Pound zako kadhaa mitihani inaletwa kutoka UK.

    Au chuo kingine kinaitwa Horizons nacho kipo mtaa wa Bibi Titi Lipia dola zako mitihani ya marekani ipo.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 04, 2010

    Institute for Information Technology wanatoa kozi za vyuo vya UK. Nafikiri walianza mwaka 1992 kama sikosei. Wasiliana nao kwa 0715 25 25 25 au email admin@iit-tz.com

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 04, 2010

    Cheki open university ya UK utaweza kupata unachotaka http://www.open.ac.uk/

    Kila la kheri

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...