Mratibu wa Miss Dar Inter College,Silas Michael akiongea na waandishi wa habari wakati akiwatambulisha wasanii watakaotumbuiza siku hiyo,ambao ni Amini (Kushoto) na Barnabas (Kulia) katika mkutano uliofanyika leo ndani ya klabu ya kimataifa ya Bilicanas.

Amini na Barnabas wakiimba moja ya nyimbo zao watakazoimba siku hiyo.
toka kulia ni Meneja Huduma wa Kampuni ya RBP OIL & INDUSTRIARTECHNOLOGY (T) LIMITED ambao ndio wadhamini wakuu wa Miss Dar Inter College 2010,Ibrahim Khatrush ,Msanii wa Bongo Flava Barnabas Ernest (Barnaba),Mratibu wa Miss Dar Inter College.Silas Michael na Msanii mwingine wa Bongo Flava,Amini Mwinyimkuu (Amini)

*************************

Wasanii wa Muziki wa Bongo fleva Amin na Barnabas leo wameongea na Waandishi wa Habari namna watakavyoweza kuwaburudisha mashabiki wao katika mkutano na waandishi hao uliofanyika kwenye klabu ya kimataifa ya Billicanas.Wasanii hao ambao ni wadogo kiumri lakini mambo yao ni makubwa kuliko,wameahidi kutowaangusha mashabiki wao kwani wanavitu vingi vipya ambavyo watavitoa siku watakapo panda jukwaani katika onyesho lao litakalofanyika kwenye shindano la kumsaka Mrembo wa RBP Dar Inter College litakalofanyika Mei 27 kwenye klabu ya kimataifa ya Billicanas.

"Mimi pamoja na mwenzangu Barnaba tutaweza kutoa burudani ya aina yake kwa mashabiki wetu kwani tunavitu vikali sana ambavyo tutaviachia siku hiyo kwa mara ya kwanza na naamini kina mtu atakubaliana nasi na atavipenda"alisema Amini na baadae Barnaba alisema kwamba "Hatuongei maneno mengi leo bali kila kitu tutakionyesha siku hiyo na kila mtu atatoka anafuhi".

Dar Inter College ni kitongoji kipya na cha kwanza kushiriki katika nyanja ya Urembo hapa Dar es Salaam ambacho kimeanza rasmi mwaka huu,kitongoji hicho kinashirikisha warembo 16 toka vyuo mbali mbali vya elimu ya juu vya jijini Dar es Salaam.

Warembo hao wanatarajiwa kuchuana vikali katika shindano hilo linarotarajiwa kuwa la kuvutia kutokana na warembo wote watakaoshiriki kuwa katika viwango vya ushindani ambapo washindi watatu watakwenda kushiriki katika shindano la Miss Highlearning.

Warembo hao wananolewa na Miss Vodacom Tanzania namba mbili 2009 Beatrce Shelukindo huku kwa upande Dansi wako na Mwalimu wa siku nyingi katika fani hiyo,Richard Yalomba a.k.a "Bob Rich" akiwapa mazoezi makali ya kucheza kwa ajili ya Shoo ya ufunguzi kwa siku hiyo ya shindano.

Mratibu wa shindano hilo Silas Michel amewataja warembo wanaoshiriki katika shindano hilo kuwa ni Agness Francis , Sanza Mukajanga , Rosemary Muhoza , Pilly Hashim , Rahma Sway , Shone Mwanyanje , Basilisa Biseko , Catherine George , Rose John , Mary Lidya na Cassian Milinga.

Shindano hilo linadhaminiwa na RBP Oil & Industrial technology Ltd, Kampuni ya bia TBL kupitia bia ya Redd's Original , Vodacom Tanzania , Shear Illusion , Michuzi blog, Janejohn5 blog, Fullshangwe blog, Mtaa kwa Mtaa blog, Condy Bureau Change ,Tanzania Daima , Ndege Insurance na Dotnata Decorations

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...