Waziri Mkuu nchini Uingereza Mh. Gordon Brown (pichani) atajiuluzu kuwa kiongozi wa Chama Cha Labour Party.
Mh. Brown ametangaza uamuzi huo baada ya Chama chake kushindwa kupata kura za kuongoza nchi katika uchaguzi uliofanyika Alhamisi.
Uchaguzi huo uliwafanya wananchi wa Uingereza kushindwa kuamua chama ambacho kitaweza kuwaongoza baada ya vyama vyote kushindwa kufikia viti 326 vinavyowezesha kuiongoza nchi.
Mh. Brown ataendelea kuingoza nchi na kuwa kiongozi wa chama hicho mpaka atakapopatikana kiongozi mwingine wa kukiongoza chama na Serikali.
Akizungumzia kuhusu masuala ya serikali ya nchi amesema kwamba shughuli zote za kiserikali zinaendelea kama kawaida.
Wakati huohuo chama cha Labour Party na Liberal Democrats vinakutana kujadili mwelekeo wa kuweza kuungana na kuunda serikali ya kuingoza nchi.
Ally Muhdin

wa
habari kamili

Siyo kweli wananchi wa Uingereza wameshindwa kuchagua chama wanachokipenda.
ReplyDeleteMatokeo rasmi ya uchaguzi na viti vyama walivyonyakua ktk mabano:
Conservative 306
Labour 258
Liberal 57
vyama vingine 28
Sheria ya Uingereza ili chama kiweze kutambulikana kama chama kinachoongoza serikali lazima kipate angalau viti vya ubunge 326.
Ikiwa hakuna chama kilichopata viti hivyo, basi itabidi vyama viwili au zaidi viendeshe serikali ya mseto itakayokuwa na viti angalau 326, ili kuwezesha serikali kupitisha miswada na sheria kwa wingi wa kura 'majority'.
Majority hiyo hupatikana kwa chama kuwa na viti 326 au kwa mseto wa vyama kuwa na viti angalau 326.
Kifupi sheria ndiyo imevibana vyama, lakini watu wanajua vyama vipi vinakubalika na wananchi wa Uingereza.
hawa viongozi wa vyama vitatu wangejifunza kama yale yaliyotokea Kenya na Zimbabwe haya ni makoloni yao na walikua wakishabikia hivi vyama kuungana kama vile haitoshi walitishia vikwazo kama wasinge ungana je! wao watatishwa na nani? kizungumkuti hicho baba.
ReplyDeleteMaana ya kushindwa ni kutokuwa na msimamo wa kuchagua chama gani kiweze kuwaongoza siyo kupiga kura.
ReplyDeleteWananchi wote wanajua kama viti vingapi vinatakiwa ili chama kiweze kuongoza nchi lakini wamegawanyika katika msimo na maamuzi yao. hiyo ndiyo sababu ya kushindwa kuchagua chama cha kuwaongoza.
Ikiwa kama Labour Party imeweza kuongoza nchi tangu miaka 13 iliyopita kwanini wasiendelee kukichagua hicho chama?
Wameamua kufanya mabadiliko ya kuchagua chama cha Conservative lakini mabadiliko hayo hayakuwa na nguvu.
Kama umefuatilia uchaguzi Wanachi wa Barking na Dagenham kwanini walijitokeza kwawingi kwenda kupiga kura? ni jimbo ambalo liliongoza nchi nzima kwa kuwa na wapiga kura wengi katika uchaguzi huo. Sababu walichoka na sera za ubaguzi ambazo chama cha BNP zilionyesha kwenye kampeni zake
Chama cha BNP kilishindwa vibaya sana na kupokonywa uongozi wote uliokuwa maana walikuwa na wawakilishi 13 katika jimbo hilo NA WOTE WALISHINDWA.
ELEWA MAANA YA KUSHINDWA NI KUTOKUWA NA MSIMAMO WA CHAMA GANI WANATAKA KIWAONGOZE MAANA WANGEPENDA CHAMA KIMOJA KATI YA HIVYO BASI KINGESHINDA BILA MATATIZO NA SIYO KAMA HALI ILIVYO HIVI SASA.