Baalozi wa Marekani Nchini Tanzania Bwana Alfonso E. Lenhardt kushoto akipata maelezo ya kipeperushi kinachoonyesha jinsi miundombinu ya Barabara ilivyoharibiwa vibaya na mvua zitokanazo na mabadiliko ya Tabia Nchi kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mh.Dkt Batilda Salha Burian, alipotembelea Ofisini kwake mtaa wa Luthuli Jijini dar es Salaam Leo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mh. Dkt Batilda Salha Burian(kulia)akiwa na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Bwana Alfonso E. Lenhardt, kwa pamoja wakionyesha zawadi Ambayo Mh waziri Batilda alimkabidhi alipotembelea Ofini kwake Mtaa wa Luthuli jijini Dar es salaam leo.


Na Evelyn Mkokoi
Afisa Habari Ofisi ya Makamu wa Rais


Serikali ina Jukumu kubwa la kutoa Elimu na taarifa ya kutosha kwa umma wa watanzania juu ya suala zima la madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi ambayo huweza kuleta madhara makubwa zaidi katika sekta ya kilimo, wanyama pori na Mazingira kwa ujumla.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mh. Dkt Batilda Burian alipokuwa akizungumza na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Bwana Alfonso Lenhardt, alipotembelea Ofisini kwake Mtaa wa luthuli Jijini Dar es Salaam.

Dkt Batilda ameeleza kuwa, ushirikiano uliyopo kati ya Serikali ya Marekani na Tanzania juu kupigana dhidi ya Malaria unaweza pia kutumika kama njia ya kupigana na Malaria kupitia utunzaji wa Mazingira.

“Wananchi wanaweza kupewa Elimu ya kutosha kupitia vipeperushi, vipindi vya Radio na Tv kwa lugha rahisi ya Kiswahili ili kuweza kuepukana na uharibifu wa Mazingira utokanao na ukataji miti na kilimo holela, Alisema.”

Akitolea mfano, Uharibifu wa Mazingira kwa upande wa Ziwa Victoria, Balozi wa Marekani Nchini, Bwana Alfonso E. Lenhardt amesema kuwa madhara mengi yanasababishwa na nchi jirani kwani Tanzania haitegemei zaidi ziwa Victoria pekee kwa uvuvi kutokana na utajiri wa maziwa mengi yaliyopo nchini, pamoja na Bahari ya Hindi.

Akitolea mfano wa Nchi zilizoendelea ambapo matumizi ya nishati ya jua yapo juu zaidi, Balozi Lenhardt, ameshauri kuwa,ni wakati muafaka sasa kwa Tanzania kufikiria zaidi matumizi ya nishati mbadala ili kuweza kunusuru Mazingira.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 10, 2010

    Hiyo zawadi iliokotwa tu fasta fasta au fikra ilitumika kabla ya kuinunua??? Looks strange and irrelevant to me, I wonder what the ambassador thought about it too.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 10, 2010

    Bendera za Zimbabwe, Zambia, Msumbiji, Ethiopia, Botswana nazo zingekuwepo nadhani ingependeza zaidi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 10, 2010

    Mdau kazi unayo, wewe ulitaka apewe zawadi gani? Hebu tupe ushauri wako kutokana na uzoefu ulionao wa kuwapa zawadi viongozi, pamoja na sheria zinazoelekeza kuhusu aina ya zawadi anayopaswa kupewa mgeni kama huyo!

    Mswahili

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 10, 2010

    Aah! nadhani iko haja ya kulijadili hili suala la zawadi. Si muda kulikuwa na mjadala mkali kuhusu kiongozi mkuu kupokea Jezi. Kuhusu zawadi hii, nadhani watu wa protocol watakuwa walichanganyikiwa kidogo kwa sababu, ukiangalia maana ya zawadi (keepsake - something of a sentmental value or memento - a reminder of past event). Kwa kuangalia sababu ya Mh Waziri nadhani ilikuwa ni kufurahishwa na ugeni huo na angependa basi kumpatia ki zawaadi ambacho kitamfanya akumbuke kumtembelea kwani kinakuwa ni chenye umuhimu kwa mtoaji ambaye ni waziri wetu. sasa ona kinachoonekana kwenye zawadi. Juu kabisa ni kama mpingo ulionchongwa- Ni kitu kizuri, Chini kuna bendera kubwa ya Marekani, aah!!! hapa kuna dosari. Kwanini waziri anampatia memento iliyo na picha ya bendera ya marekani!!!!!, kwa nini isiwe chochote kinachotambulisha tanzania na utanzania wetu au basi hata mazingira? hapo chini kuna bendera nne, Ya kwanza ni ya Kenya!!!! hapa napo inabidi ukashangae feri, inafuatiwa na ya Tanzania, kisha Africa ya Kusini na mwisho ya Uganda. na hapo chini sioni kama kuna maandishi yoyote ambayo yatamkumbusha mgeni wa Waziri itakapopita miaka mitano. Huu mchanganyiko hauleti maudhui yenye kueleweka kabisa. LAKINI NAWEZA KUSEMA, YA KWAMBA, HII INAONYESHA NAMNA GANI TUMEYUMBA SANA KATIKA MAMBO YETU. NA IMANI IDARA ZA ITIFAKI ZINA UTARATIBU UNAOONGOZA NINI KITOLEWE, NINI KIPOKELEWE NA KIFIKISHE UJUMBE GANI. kuna wakati nilikwenda kikazi nchi fulani ambayo Tanzania iliisadia katika kupata uhuru wake. Tulikuwwa tunawasema kuwa mambo yao yako shaghalabaghala, na tulikuwa tunajitahidi kuwaweka sawa. NAIMANI WAO SASA WANASEMA, HIVI NI HAWA WATANZANIA TUNAOWAJUA. SOMETHING HAS TO BE DONE. MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 11, 2010

    Hata mimi nasema hiyo zawadi walifikiria au ilichukuliwa tu na kwa kujilamba tena unampa mmtu michongo yetu na bendera ya USA....

    Akiangalia atafikiri hizo bendera zingine ni za ccm, chadema, CUF etc etc....LOL...

    Kweli Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 11, 2010

    Hiyo zawadi ingekuwa na bendera ya Tanzania na Marekani tu; hapo kingeeleweka kuwa inalenga kwenye mahusiano kati ya Nchi hizi mbili! Lakini kuwa na bendera za nchi nyingine hayo ni mapungufu makubwa kwa maana au tafasili harisi ya zawadi.Waziri umetuaibisha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...