
Wiki hii Balozi wa Uingereza hapa nchini, Diane Corner, pamoja na Inspecta Generali wa Polisi, (IGP) Saidi Mwema wamezindua programu ya mafunzo ya uongozi kwa Jeshi la Polisi la Tanzania inayodhaminiwa na Serikali ya Uingereza.
Mafunzo hayo, ambayo yataendeshwa na Mamlaka ya Kitaifa ya Kuboresha Idara ya Polisi ya Uingereza (NPIA) pamoja na ile ya Hampshire kwa muda wa miezi tisa (kuanzia mwezi ujao), yatakuwa na lengo la kubadilishana uzoefu na mbinu bora - kwa kujikita zaidi katika masuala ya kiuongozi na kimenejimenti.
“Mafunzo hayo ni muhimu sana kwetu hasa kwa kipindi hiki cha maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao, lakini pia ni muhimu zaidi katika jukumu zima la kudumisha amani hapa nchini,” alishukuru IGP Saidi Mwema.
Ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mafunzo hayo, hivi karibuni Ubalozi wa Uingereza uliwapeleka kuhudhuria mafunzo huko NPIA na Hampshire nchini Uingereza IGP Saidi Mwema pamoja na maafisa wengine wa Jeshi la Polisi la
Tanzania, ambao ni Kamishna wa Polisi anayeshughulikia Utawala na Rasilimali, Clodwig Mtweve, Mkuu wa Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Abdulrahman Kaniki na Kamanda wa Chuo cha Polisi Dar es Salaam, Elice Mapunda.
Ujumbe huo ulipata mafunzo huko NPIA katika masuala ya utekelezaji oparesheni za kipolisi kwa kuzingatia haki za binaadamu, utoaji huduma za kipolisi, uchunguzi, utafiti na masuala mbalimbali ya kiutawala. Pia walipata fursa ya kujiunga na jeshi la Polisi Hampshire na kufanya doria, pamoja na kujenga ujirani mwema na jamii zinazozunguka.
Uzoefu huu umewezesha kujenga ushirikiano wa karibu zaidi kati ya Jeshi la Polisi la Tanzania na Hampshire, na hivyo kupanua wigo wa kujifunza kutoka pande zote mbili.
"Ninayo furaha kubwa kuzindua programu hii ya Polisi. Ninatumaini ya kuwa mafunzo haya yatakuza ushirikiano baina ya Jeshi la Polisi la Tanzania na lile la Uingereza ambao kila upande utakuwa na mengi ya kujifunza kutoka kwa mwenzake,” alisema Balozi Corner.
Mafunzo haya ya Uongozi kwa Jeshi la Polisi, ni miongoni mwa misaada inayotolewa Serikali ya Uingereza kupitia mfuko maalumu Ubalozini. Pia mafunzo haya yanafadhiliwa na Idara ya Misaada ya Kimataifa ya Uingereza (DFID.
Baada ya kuhudhuria mafunzo ya awali nchini Uingereza maofisa wa jeshi la Polisi, Elice Mapunda na Abdulrahman Kaniki wamepandishwa vyeo hivi karibuni, kutoka nyadhifa za Ukamishna Msaidizi na kuwa Makamishna Waandamizi.
Hivi huyu jamaa anakijua kiinglish kweli?!?
ReplyDeletewe anony wa kwanza umenichekesha sana! lkn sio kosa lako! bado unafikiria tz ya sasa ni ya enzi za mwl! Saidi mwema namjua vizuri sana! anaongea lugha ya kwa bibi vizuri! pia ana shule! alishawahi kuwa kamanda mkoa wa mbeya wakati nami nilikuwa nimejiunga na jeshi hilo kabla sijaacha na kuja utumwani kubeba box! miaka ya sasa hivi 90% ya maras waliopo maofisini wanashule! stashahada za kumwaga tena za UDSM, MZUMBE NK! kasheshe kwa wale wavaa nyeupe barabarani! Wenye uniform wasio na vyeo vyovyote na maCID wasiokuwa na vyeo(namaanisha nyota nk)siku hizi polisi km hana shule kupata nyota afanye kazi ya ziada!
ReplyDeletekwani kwenda shule ndo kujua english??? English bado matatizo sana kwa awaliokuwepo ma offisini hata kama shule hipo !! kuongea english si mchezo wewe!!
ReplyDeleteHeshima kwako Mkuu IGP
ReplyDeleteMabadiliko mengi mazuri tunayaona katika jeshi la polisi. Usikatishwe tamaa na watendaji kazi wachache wanaovuruga, wasiojua kuwa ubabe enzi zake zimeisha. USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO NI PAMOJA NA HESHIMA KWA RAIA WEMA.
PILISI YA LEO SIO YA MIAKA 5 ILIYOPITA. WATUMIE VIJANA WASOMI ZAIDI.
nakuunga mkono ijp mwema ni msomi mzuri hukumbuki pia ktk kundi la mwsho la mawakili wa kujitegemea naye amefaulu mitihani hiyo, pia alituwakilisha vizuri interpol pale nairobi, kusema kweli jeshi la polisi lina wasomi wengi kwa sasa kulinganisha na kipindi chochote kile
ReplyDelete