basi la Taifa Stars likiwa limegongana uso kwa uso na pick up leo sehemu za Millenium Towers, Kijitonyama, jijini Dar. Bahati hakuna aliyeumia katika ajali hiyo ambayo chanzo chake hakikuweza kufahamika mara moja. hili basi lilitolewa msaada kwa TFF na benki ya NMB kwa ajili ya timu za taifa
foleni kubwa ilizuka baada ya mzinga huo, na kabla ya trafiki hawajafika
taa ya mbele kulia na bampa kwishnei...
PICHA NA MDAU MAC TEMBA WA



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2010

    mh kweli ajali ni ajali tu, bus hilo lilikua hapa Mwananyamala Komakoma mida ya saa tisa katika msiba, mara hii tena limepata ajali. poleni sana mliokua ndani ya bus

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 20, 2010

    Issa muhidin michuzi, lazima nikupongezebkwa kazi nzuri unayoifanyia Tanzania . Hii blog Ina nguvu sana siyo Kama nilivyodhania.

    Mimi natarajia kustaafu kutoka serikalini miaka 10 kuanzia sasa Ila naingiwa sana na wasiwasi kuhusu maisha ya mbeleni hasa ukizingatia Hali halisi ya sasa kwenye NSSF

    Article iliyoandikwa na kijana wetu kipenzi John Mashaka inenifungua macho sana na wenzangu wengi tu tuliokutana nao Jana jioni, aisee Nina kukubali sana na tunaomba upost articles zaidi za huyu kijana wetu mahiri

    Asante sana bw muhidini michuzi

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 20, 2010

    Hii ajali hainishangazi kwa kuwa imetokea katika barabara ya ajabu ambayo hakuna mfano wake popote duniani. Kipande hiki cha Ali Hassan Mwinyi Road kati ya makutano na Barabara ya Kawawa na Mwenge kina njia (lanes) tatu ambapo njia ya katikati inatumiwa na magari yanayokwenda pande zote. Ni ajabu na kweli. Kama kuna barabara ambayo mimi hufanya kila njia kuikwepa ni hii. Kila nipitapo huwa nashuhudia kosakosa nyingi tu. Kimbembe kinakuja pale unapotaka kukata kulia. Wale waliowahi kundesha magari katika barabara hii ya ajabu kabisa wanaelewa nina maana gani. Pia nadhani hii ni barabara hatari zaidi kwa waenda kwa miguu kuliko zote duniani. Kujaribu kuvuka barabara hii ni kujitafutia kifo au kilema cha maisha. Kama kulikuwa na ulazima wa kuipanua barabara hii, basi ingefanywa ‘dual carriage’ ya njia mbili kila upande. Sijua wakubwa walikuwa wanafikiria nini walipoamua iwe na njia tatu. Kuna baadhi ya mambo yanaweza kutokea Tanzania tu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 21, 2010

    Mdau namba 3 sina cha kuongeza zaidi ya kukubaliana na wewe kwa asilimia 100%.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 21, 2010

    Michuzi..dereva wa bus la Taifa Stars ni tatizo kubwa. Sielewi ni tabia yake au kuna anachokiwahi asbh. Juzi asbh maeneo ya bamaga amekaribia kuniletea ajali kubwa sana akitoka Atriums akiwa na wachezaji garini. Muda kidogo kabla ya kufika taa za Science akamgonga jamaa aliekuwa mbele yake ila hakukuwa na tatizo kubwa wakamalizana kikubwa.Ifike wakati madereva kama hawa watimuliwe kaizni.

    Mdau Jimmy Sinza

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 21, 2010

    Mtoa maoni namba tatu.
    Barabara ya katikati ni kitu chakawaida especially kwa miji mikubwa na mara nyingi hutumika kulingana na mwelekeo wa traffic kubwa (rush hours) iko upande gani. Mfano asubuhi itatumika kwa wanokwenda kazini na jioni itatumika kwa wanaorudi kazini. Tatizo kwa hapo inakosekana taa au mwongozo kuonyesha ni wakati gani upande upi unatakiwa kuutumia matokeo yake ndio inakuwa ya hatari kama ulivyosema

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 23, 2010

    Nakubaliana asilimia 100 na mtoa maoni wa tatu hapo juu. Barabara hii ni tatizo kubwa sana. Kuna mdau hapo juu amesema barabara za aina hii ni kitu cha kawaida kwingineko na kwamba matumizi ya njia ya katikati yanategemea na ni wapi magari mengi yanaelekea. Hata hivyo napenda nimfahamishe kuwa njia hii ya katikati imechorwa mishale inayoonyesha kwamba inatakiwa itumike na magari yanayokwenda mjini tu. Lazima tukubali kuwa hapa wakubwa wamechemsha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...