
Mwanamziki mkongwe wa mziki wa dansi nchini toka nchini Kongo Kinshasa, Fredy Mayaula Mayoni (RIP) amefariki dunia siku ya 27-05-2010 huko jijini Brussels, Ubeligiji, kwa ugonjwa kansa ya ubongo (brain trumour).
Marehem Mayaula Mayoni (64) ni mwanamziki aliyekulia na kusomea jijini Dar wakati wa utoto wake miaka ya 60s, kwani baba yake alikuwa ni moja wanadiplomasia katika ubalozi wa Kongo(Zaire) nchini Tanzania. Marehem pia aliwahi kucheza kandanda katika timu maarufu nchini Yanga(Young Africa) ya jijini Dar.
Vijana wa kizamani watamkumbuka marehemu Mayaula pale alipojiunga na bendi ya TP OK Jazz,iliyokuwa inaongozwa na gwiji Franco Luambo Makiadi, uko Kongo. Mayaula alijiunga TP OK Jazz baada ya kurudi kwao Kongo (DRC) na kujikita katika ulimwengu wa mziki ,ambako aliachia wimbo maarufu "Cherie Bondowe" au "Sherry bondowe", wimbo ambao ulimpa umaarufu sana.marehemu pia aliwahi kufanya kazi na mwanamziki ambaye pia marehemu Mpongo Love.
Mungu amlaze pema peponi Mayaula Mayoni
Amin
May the Lord Our God Shine His (God's) Eternal Light Upon Him, and May He (Deceased) Rest in Peace. Amen.
ReplyDeleteA Loss is a Loss, but, WHAT A LOSS!
His (Deceased's) Legacy will live on, definitely.
Amen.
Mayaula Mayoni(RIP)mungu akaulaze mahala pema peponi.
ReplyDeleteAnkal misupu asante kwa taharifa hizi za kusikitisha.naukumbuka wimbo wa Sherry bondoe,wimbo ambao nikiusikiliza unanikumbusha ujanani,na wakati kilo ya sukari sent 80,ambapo dar maisha yalikuwa poa.
Rest in Peace,we are all in the same way.Amen
ReplyDeleteMjusi
Ankal Michuzi,
ReplyDeleteNajua wewe ni Bingwa wa kubana maoni Africa Mashariki na Kati. Hii pia naomba usiirushe hewani, ni kwa taarifa tu.
Kuna maoni nimetuma hapo kuhusu, WHAT A LOSS! sawa, sikumaanisha kumlenga mtu yeyote yule zaidi ya wale watu wangu waleee.
Hivyo waambie wadau wa Sherry I Love You, Sherry na Motema ee; wasijishitukie. Shukran.
Mungu akulaze pema Mayaula,utakumbukwa kwa yale ulioyafanya.
ReplyDeleteYanga Imara
Rest in Peace MAYAULA, u'll be remembered much! Your time @ youn african fc, and the unforgetable music of your own creation! Bwana ametoa na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe!
ReplyDeleteKembaseke nzela ya moto nyoso(kaburi ndio njia ya watu wote) mungu amlaze mahali pema Mayaula Shemeji yetu huyo kwa akina Ted Amri -Mwambungu Mbinga,Ruvuma.
ReplyDeleteMayaula ingawa ulikuwa mkongo lakini wewe ni mtanzania, u r one of us, RIP, we love u.
ReplyDeleteOh Mayaula Mayoni tulifurahia mno nyimbo zako lakini tunakuombea heri Mungu akulaze pema peponi. Amen
ReplyDeleteRIP Brother. You will be missed.
ReplyDelete