HABARI ZINASEMA KUMETOKEA AJALI YA MALORI AINA YA SEMI-TRELA MAWILI KUGONGANA USO KWA USO SEHEMU ZA MIKESE, MOROGORO, NA RIPOTA WA GLOBU YA JAMII ALIYE ENEO LA TUKIO AMESHUHUDIA WATU WATATU WAKIWA WAMEPOTEZA UHAI.
INASEMEKANA BAADA YA MAROLI HAYO MAWILI KUGONGANA, GARI LA TATU AINA YA FUSO NALO LILIANGUKA BAADA YA DEREVA WAKE KUJARIBU KUKWEPA KULIGONGA LORI MOJA KWA NYUMA NA KUTOKA NJE YA BARABARA NA KUPINDUKA.
AJALI HIYO IMETOKEA MAJIRA YA SAA MBILI USIKU HUU NA KUSABABISHA FOLENI NDEFU SANA KILA UPANDE WA BARABARA. JUHUDI ZA GARI LA JESHI LILILOKUWEMO KWENYE FOLENI HIYO ZIMESAIDIA KUSOGEZA KANDO MALORI HAYO YALIYOZIBA NJIA NA SASA SAFARI IMEANZA.
HATA HIVYO MIILI YA WATU WAPATAO WAWILI NDANI YA LORI LA FUSO BADO IMENASA NDANI NA JUHUDI ZA KUIONDOA ZINAENDELEA. MWILI WA MAITI MMOJA TAYARI UMESHATOLEWA, NA WATU KADHAA WALIOKUWA NYUMA YA FUSO WAMEJERUHIWA, WENGINE VIBAYA.
CHANZO CHA AJALI BADO NI KITENDAWILI.
HABARI ZAIDI ZITAKUJA KADRI ZITAVYOPATIKANA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 22, 2010

    Ankal,
    asante kwa kutupasha habari za TSE, tutapeleka watoto wetu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 22, 2010

    lazima tupate wakina Drogba na wengine hapo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 22, 2010

    mh! mbona km haya maoni hayaendani na story yenyewe??? au mi ndo nimechemka??
    Holland-mdau

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 23, 2010

    Mdau wa kwanza,

    What TSE is? Tanzania School of Engineering au nini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...