HABARI ZILIZOIFIKIA GLOBU YA JAMII HIVI PUNDE TOKA HOSPITALI YA MWANANYAMALA JIJINI DAR, ZINASEMA KWAMBA MUASISI WA SANAA YA UIGIZAJI NCHINI, MZEE RAJABU HATIA A.K.A PWAGU AMEFARIKI DUNIA JIONI HII MAJIRA YA SAA KUMI KATIKA HOSPITALI YA MWANANYAMALA JIJINI DAR ALIKOKUWA AMELAZWA KWA MARADHI YALIYOKUWA YAKIMSUMBUA KWA MUDA MREFU.
MZEE PWAGU NDIYE MUASISI KUNDI LA SANAA KAOLE GROUP AMBAYO IMETOA WASANII WENGI SANA MPAKA SASA, WAKIWEMO RAY, KANUMBA NA CLAUDE. ALITAMBA SANA KATIKA KIPINDI CHA PWAGU NA PWAGUZI CHA RTD ENZI HIZO AKISHIRIKIANA NA MAREHEMU ALLY KETTO.
MAZISHI YANATARAJIWA KUFANYIKA KESHO KWENYE MAKABURI YA KIGOGO JIJINI DAR. MSIBA UPO NYUMBANI KWAKE HAPO HAPO KIGOGO KARIBU NA ROUND-ABOUT YA KIGOGO NA MAGIMENI.
TIMU NZIMA YA GLOBU YA JAMII TUNAMUOMBEA KWA MUNGU AIWEKE ROHO YA MZEE PWAGU MAHALA PEMA PEPONI. SISI TULIMPENDA LAKINI MOLA ALIMPENDA ZAIDI....
-AMIN
------------------------------
HABARI ZAIDI ZA MZEE PWAGU
R.I.P naona hata wakina zekomedi waliiga kidogo kutoka kwake
ReplyDeletepole sana wafiwa namkumkuba sana huyu mzee.
ReplyDeleteUpumzike kwa amani Mzee wetu Pwagu. Asante kwa kutuburudisha. Tutakukumbuka milele. Poleni sana familia ya mzee Pwagu.
ReplyDeleteKwanza Shukrani sana bro Michu kwa habari hii. Hiki kifo kimenigusa sana kwani mzee pwagu ni kama mzee we2 pale Kigogo Mbuyuni mpaka Kigogo CCM. Mzee ambae anajulikana sana, mkalimu na msaidiaji wa jamii kwa lolote.
ReplyDeleteKigogo Boi
ama kweli kamichu thanks na pole manake mzee pwagu kusikia habari zake nimesikitishwa sana ila umenikumbusha nyumbani kweli kweli nikikumbuka radio tanzania walivyokuwa wanaweka kipindi cha pwagu na yule mwenzie nimemsahau jina ila ndio mungu kapenda.
ReplyDeleteR.I.P Pwagu sote twaelekea huko.
Poleni familia nzima ya pwagu, kwakweli hawa ndio maselebrity tunaopenda kuwasikia hawana makuu na wanafanya kazi zao kimapenzi, si kwa pesa wala si kwa kujulikana, pwagu kwa kweli kipaji chako hakitapatikana tena bongo siku hizi watu wanaweka pesa mbele, ila mfano wako ni utang'aa milele. asante kwa yote.
Nimepokea habari hii kwa masikitiko makubwa sana. Kifo cahake ni pengo kubwa sana katika tasnia ya sanaa nchini Tanzania. Mungu aiweke roho yake mahala pema peponi AMEN.
ReplyDeleteMpg bx
inalillah wainaillahi rajiun. Inshallah Allah amsamehe dhambi zake.
ReplyDeleteDuh, rest in peace mzee wetu.
ReplyDeletehuyu mzee kwa kweli enzi za utoto wangu alinifanya nisikae mbali na redio siku ya kipindi cha "pwagu na pwaguzi".
ni msiba kwa kweli!
mdau- amsterdam
Pumzika kwa amani kiongozi, tutakukumbuka kwa mchango wako katika tasnia ya sanaa nchini, ulikuwa chachu muhimu sana. Sitasahau utangulizi wako na Pwaguzi katika kipindi cha mama na mwana Radio Tanzania enzi zile..."mahokaaaaa!" Japo hadi leo sijajua maana yake :-0
ReplyDeletePole sana kwa familia, ndungu, jamaa, marafiki na jamii nzima ya Watanzania kwa msiba wa nguli huyu.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi, Amina.
INNA LILLAHI WAINNA ILAIHI RAAJIUN.
ReplyDeletekila kilichoumbwa kitakufa 2 kitake
kisitake,wewe,mm,yule na vyote vitaondoka isipokuwa MUUMBA 2.
2JIANDAE VEMA DUNIA ISHAKWISHA HIII
2PO WAUNGWANA ???????????????????????
inna lillahi waina illahi rajiun, rahman atiye peponi awe miongoni mwa waja wa peponi. Allah ma amin.
ReplyDeletemdau new york
So sad... may his soul rest in peace.
ReplyDeleteR.I.P mzee wetu,umetungalia mbele ya haki.
ReplyDeleteNapenda kutoa pole kwa ndugu,jamaa,majirani na wale wote wanaoguswa na msiba huu. Mwenyezi mungu awape nguvu katika kipindi cha msiba.
Amen
RIP Sir. Kipaji chako kiligusa maisha ya wengi.
ReplyDeletePoleni ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu popote pale mlipo.
RIP
ReplyDeletenatumaini jina lake litawekwa kwenye vitabu vya sanaa pia
Huyu alitufurahisha wengi tukiwa wadogo.. pwagu na pwaguzi
NIMEPOKEA KWA MAJONZI MAKUBWA KIFO CHA MZEE WETU PWAGU NAANDIKA HII COMMENT HUKU MACHOZI YANANITOKA
ReplyDeleteKINACHOFANYA MACHOZI YANITOKE NI KUMBUKUMBU KUBWA YA MZEE PWAGU NA MWENZIE PWAGUZI KATIKA VIPINDI VYAO RTD
NIKIKUMBUKA MAJIRA YA USIKU USIKU BAADA YA KUPATA CHAKULA CHA JIONI KULE KIJIJINI KWETU AMBAPO HATUKUWA NA UMEME KWENYE NYUMBA YETU
ILIKUWA NI KIRADIO CHA MBAO KINACHOJULIKANA KWA JINA LA 2 77 CHA KUTUMIA BETRI
ILIKUWA KILA SIKU IKIFIKA MAJIRA HAYO LAZIMA TUSOGELEE RADIO YETU TUNAKUWA KIKUNDI TAKRIBANI MTAA MZIMA TUNAKAZUNGUKA KARADIO KUPATA UHONDO WA KIPINDI CHA MZEE PWAGU
POLENI SANA WANA FAMILIA NA NAWATAKIA UVUMILIVU KATIKA KIPINDI HICHI KIGUMU
MSIBA WA MZEE PWAGU NI MZIBA WA WATANZANIA WOTE KWA UJUMLA
WAZEE KAMA HAO WANAPASWA KUKUMBUKWA KWA MCHANGO WAO KATIKA JAMII KWANI KILA ALIETAKA KICHEKESHO ENZI HIZO HANA BUDI KUSIKILIZA KIPINDI CHA PWAGU NA PWAGUZI
MUNGU AKULAZE PEMA PEPONI MZEE WETU PWAGU DAIMA TUTAKUKUMBUKA MBELE YAKO NYUMA YETU
RADIO ZA TANZANIA NA TV ZINAPASWA KUWEKA VIPINDI VYA MZEE PWAGU KATIKA WIKI HII YA MSIBA WAKE ILI KUMUENZI
mdau wa mahakama kuu ya dunia nipo kwenye huzuni na majonzi makubwa
inna lillahi wainna ilaihi raji'un.kila nafsi itaonja maut,mwenyezi akulaze mahala pema peponi amin.pwagu na pwaguzi was entertainment for a lot of us who did not own a tv.
ReplyDelete