Makamu wa Rais Dr. Mohamed Shein akivishwa Skafu na Elizabeth Gasper wa Shule ya Sekondari ya Babati Day ,alipotembelea Mkoa wa Manyara akisubiri kuzindua mbio za Mwenge zinazotegea kuzinduliwa mjini Babati kesho tarehe 29.5.2010.Makamu wa Rais Dr. Mohamed Shein (wa tatu kulia akisikiliza Risala ya Wilaya ya Babati kwa kiongozi aliyeteuliwa ambae hayupo pichani na wengine wa kwanza kulia ni Waziri wa kazi Maendeleo ya Vijana Zanzibar Mhe. Asha Abdallah Juma anaefuata ni Waziri wa kazi na Maendeleo ya Vijana Tanzania bara Mhe. Juma Kapuya na wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara ndugu Hendry Shekifu akifurahia Risala hiyo leo kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Babati .
viongozi wa Chama na Serikali wakimsikiliza Makamu wa Rais Dr. Mohamed Shein (ambae hayupo pichani ) akiwahutubia viongozi hao mjini Babati leo.Makamu wa Rais Dr. Mohamed Shein pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Hendry Dafa Shekifu wakifurahia ngoma illiyokuwa ikichezwa ijulikanayo kama Msanja ngoma wakati wa mapokezi ya mgeni wao Mkoani Manyara –Babati
Akina mama wa Mkoa wa Manyara wakifurahia ngoma yao ya Msanja ngoma wakati wa mapokezi ya Makamu wa Rais Dr. Mohamed Shein Mkoani Manyara –Babati leo.
(Picha na Anna Itenda wa Maelezo ).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2010

    Nashangaa sana waandishi wahabari walioenda shule kusomea uandishi wa habari bado kila siku wanaandika "viongozi wa Chama na Serikali" Kwanini hawaandiki viongozi wa vyama mbali mabali na serikali......Ina maana miaka yote toka imeanzishwa vyama vingi bado wengine hawalijui hilo au ni makusudi au ni ignorance?...

    Najua kiongozi hapo alikua katika shughuli za kiserikali na anatumia hela ya serikali kwenda huko. Na mwenge ni wa Taifa sio CCM...

    Whats happening? Ina maana hawajui au wanafanya makusudi? Hata hapo ukiangalia ni kijani kijani tu. Ina maana vyama vingine haviruhusiwi kukimbiza mwnge huu?

    Ni heri kuwashirikisha watu katika kila jambo na kusikia walilonazo rohoni kwao (vyama mbali mbali vina sauti pia) kusuppress feelings za watu wengine sio vizuri...siku wakiamka huko itakua taabu...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...