Ismail Aden Rage (pichani) usiku huu amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa klabu ya Simba baada ya kushinda kwa idadi ya kura 785 dhidi ya mpinzani wake Hassan Hassanoo aliyepata kura 435 katika uchaguzi uliofanyika katika Bwalo la Maofisa wa Polisi lililopo Oysterbay, jijini Dar.Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imekwenda moja kwa moja kwa Godfrey Nyange Kaburu ambaye amepita bila kupingwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 10, 2010

    Kama mpenzi mkubwa wa Simba natoa shukurani zangu kwa Mwenyekiti wetu aliemaliza muda wake kwa kutuwezesha kupata ubingwa katika uongozi wake na kumaliza ligi kuu bila kufungwa.
    Bwana Rage hongera sana kwa ushindi na natumai utatufanyia mengi mema wana Simba na sio kututumia kama ngazi ya kupandia TFF au Ubunge.

    Che.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 10, 2010

    Michuzi maandishi mekundi huwa yanatumika kwa tangazo la kifo tu unajua nimeshituka sana

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 10, 2010

    Sasa Uchaguzi si ulisimamishwa na mahakama.Kwa hiyo Simba wamedharau mahakama ya Wambura?.

    Kwa hiyo mahakama ya wambura itasema uchaguzi huu sio halali?.Wadau mnaojua sheria za FIFA na za nchi mtufafanulie kama Wambura aendelee na kesi zake mbili na pia afungue nyingine mbili moja ikiwa ni kusimamishwa uanachama kinyume na court order na nyingine ya kubatilisha uchaguzi(sio halali kwa mujibu wa Wambura)ili awe na kesi nne('akishinda atapata pesa nyingi').

    Mimi kama mimi nawapongeza Simba kufanya uchaguzi halali na namsihi Wambura afute kesi kwa kuwa hata akishinda kesi wanachama wa Simba kamwe hawatamchagua kuwa Mwenyekiti. Daniel- Moshi

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 10, 2010

    This dude is still working?? Its time to retire, sorry.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 10, 2010

    Kamichu nilishtuka nilifikiri katutangulia mwenzetu kumbe ni cheo tu pls tumia maneno madogo na rangi nyeusi tu manake wengine tuna presha

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 10, 2010

    michuzi tusaididie kwenye hili, uchaguzi si ulisimamishwa na mahakama?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 10, 2010

    Jamani muwe mnafatilia habari na sio kukurupuka tu hivi hamkusikia kama uamuzi wa kusimamisha uchaguzi umetenguliwa au ndio yale yale tu

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 10, 2010

    Mahakama ilitengua pingamizi la Michael Wambura, na hivyo kuufanya uchaguzi wa simba uendelee kama ilivyopangwa.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 10, 2010

    Ndugu watanzania wote napenda kuwaambia kwamba kama tabia hii itaendelea nchini kwetu basi itakuwa ni miujiza soka letu kufikia la hao tunaowatamania kila siku.

    Nani ambae hajui kwamba WAMBURA ni mtu wa kweli asiependa rushwa na mchapa kazi?ambae angewaza kuleta mabadiliko makubwa kwenye klabu ya SIMBA.

    Huyu RAGE alikwisha fungwa kwa kosa la WIZI sasa mnamchagua tena na inavyosemekana ametumia pesa nyingi tu, tukae tuone mwisho wa simba.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 10, 2010

    kila la heri Aden Rage.
    inaonyesha wanachama wa simba wana imani kubwa nawe,ndio maana wamekuchagua kwa kura nyingi kiasi hicho.
    Hivyo nawe wape uongozi uliotukuka

    ReplyDelete
  11. Mweeh!

    Kama Mahakama Kuu kumbe inaweza kusikiliza kesi na kutoa maamuzi kwa haraka hivyo, tena siku isiyo ya kazi-Jumamosi, sasa kwa nini kesi zingine huwa zinachelewa sana hata miaka kadhaa?

    Kumbe tukiamua kufanya jambo tunaweza ila tunafanyaga makusudi tuu?

    Khaah!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 10, 2010

    hakuna mapenzi kwa simba wala nini!! wanachama wa simba ni kama wale wazee wa ccm waliokuwa wakishangilia hotuba ya mh kikwete, bila kujali madhara yaliyokuwa yakitarajiwa. hivi Rage ana jipya gani mpaka aweze kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa simba? kafanya fitna kwa wambura ili achaguliwe yeye na aendeleze yale yote ya hovyo aliyoacha hapo klabuni. kweli sikio la kufa alisikii dawa.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 10, 2010

    Ndolanga na wewe tunakusubiri Jangwani.
    "KHAMSA - MABATA USHUNGU WALLAHI"

    Mji bariiidi, hakuna matusi

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 10, 2010

    Kwa taarifa yenu Bw. Rage alisafishwa na mahakama maana yake ni kuwa hukumu aliyopewa mwanzo haikuwa sahihi. Mbele ya sheria ni mtu asiye na kosa lolote na safi kabisa, vinginevyo hata katiba ya simba isingemruhusu!!! Hongera sana Rage, tunataka mabadiliko ya haraka katika systems zote za utawala wa simba ili twende na wakati.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 10, 2010

    SAIGON OYEE...ADEN OYEEE..SIMBA WAZEE WA 5 MKO JUU LAKINI C KWELI KWAMBA NYIE NDIO MNAWAWEZA WAARAB,NO..HATA ADEN ANALIJUA HILO

    sayz HADJ DROGBA

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 10, 2010

    ankali Misupu

    mi na mshangao sana juu ya hili,hivi simba si ina wanachama mpaka mikoani?mbona wao hawajapiga kura?na hao waliopiga kura hawafiki hata 2000?hivi kweli huu uchaguzi ulikuwa makini au ndio kiini macho????wajumbe wa mikoani wao vp?yaani simba sc ina wanachama hao tuu kama 1500 tu waliopiga kura????

    kweli tuna kazi sana mbeleni kama kundi hili dogo litakuwa na maamlaka wa kumweka mtu madarakani...

    ni rahisi sana kwa mgombea mwenye hela kununua wajumbe hawa 700 na kumweka madarakani.

    pole wambura maana simba ni kijito cha maji matamu yaani hela za kumwaga wala hakuna system ya kudhibiti so Rage is for that,Wambura wanamjua ni mtu makini na mkalim kwenye matumizi ndio maana hata TFF wanamfanyia mizengwe ili awe mbali na klabu ili finally asiweze kurudi pale TFF karume maana atawaharibia keki yao wanayoila kutokana na hela za mpira na wadhamini wa taifa starz...

    haya Rage hongera kweli hela haisemi uongo kwa wapiga kura.

    SIMBA SIMBA SIMBA POLENI KAMA MNASUBIRI MIUJIZA YA RAGE NENDENI MKAWAULIZE MORO UNITED SI ALIKUWA MWENYEKITI MTAAMBIWA ALIFANYA NINI...

    MDAU KITAA CHA SINZA

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 10, 2010

    Tupate kwanza tangazo harafu tukirudi tutaendelea na sehemu ya pili! Simbaaaaaa ah!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 10, 2010

    Color Red:
    Red is the warmest of all colors. Red is the color most chosen by extroverts and one of the top picks of males. On the negative side red can mean temper or anger. In China, red is the color of prosperity and joy. Brides wear red and front doors are often painted red. Red is Tuesday's color. Red roses symbolize passionate love. Ruby rings should be worn on the left hand. Red is the color of Mars. This planet is known as the God of War.

    Red Energy
    Red is associated with fiery heat and warmth. It can also mean danger (burning).

    Red is the color of blood, and as such has strong symbolism as life and vitality. It brings focus to the essence of life and living with emphasis on survival. Red is also the color of passion and lust.

    Put some red in your life when you want:

    increased enthusiasm and interest
    more energy
    action and confidence to go after your dreams
    protection from fears and anxieties

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 10, 2010

    RANGI NYEKUNDU WALA HAINA MAANA YA KIFO AU HUZUNI:


    Color Red

    Red is the warmest of all colors. Red is the color most chosen by extroverts and one of the top picks of males. On the negative side red can mean temper or anger. In China, red is the color of prosperity and joy. Brides wear red and front doors are often painted red. Red is Tuesday's color. Red roses symbolize passionate love. Ruby rings should be worn on the left hand. Red is the color of Mars. This planet is known as the God of War.

    Red Energy
    Red is associated with fiery heat and warmth. It can also mean danger (burning).

    Red is the color of blood, and as such has strong symbolism as life and vitality. It brings focus to the essence of life and living with emphasis on survival. Red is also the color of passion and lust.

    Put some red in your life when you want:

    increased enthusiasm and interest
    more energy
    action and confidence to go after your dreams
    protection from fears and anxieties

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...