Afisa mradi wa Champion Dr.Yeronimo Mlawa(kushoto) akifafanua jambo katika uzinduzi wa kampeni ya uzinduzi wa mradi wa Champion uliokuwa na Kauli mbiu ya Vunja Ukimya Zungumza na Mwenza iliyofanyika jijini Dar es Salaam.(kulia)Meneja Mawasiliano wa champion Lindsay Hughes.
Mmoja wa wandishi wa habari waliohudhulia katika uzinduzi wa kampeni ya uzinduzi wa mradi wa Champion uliokuwa na Kauli mbiu ya Vonja Ukimya Zungumza na Mwenza akiuliza swali katika uzinduzi huo ulioandaliwa na shirika la Edgender Health kwa kushirikiana na Shirika la Academy For Educational Devolopment kwa ufadhili wa watu wa Marekani,iliyofanyika jijini Dar
Wasanii wa kundi la THT Eliasi Barnabas( kulia) na Linah Sanga (kushoto) wakiimba wimbo maalumu katika uzinduzi wa mradi wa Champion kuhusu kampeni ya Kutumia Vyombo vya Habari unaohamasisha mjadala wa kitaifa.Majukumu na nafasi ya Wanaume ili kupunguza Maambukizo ya Ukimwi iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya cort yard Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
MRADI wa Champion umezindua kampeni ya kitaifa ya kuhamaisha mawasiliano na majadiliano kwa wanaume, wanawake ili kupunguza Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) pamoja na matatizo ya uzazi.
Kampeni hiyo yenye kauli mbiu ya ‘Vunja Ukimya, Zungumza na Mwenzio’ ina lengo la kuwahamasisha wanaume na wanawake kuwa na mawasiliano mazuri kwa lengo la kudhibiti uwezekano wa kuwa na wapenzi wengi
Akizindua kampeni hiyo jijini Dar es Salaam, jana Meneja wa Mradi huo, Dk. Yelonimo Mlawa, alisema wameamua kuzindua kampeni hiyo baada ya utafiti walioufanya kugundua kuwa wenza wengi hawapo wazi juu ya mahusiano yao jambo linalowafanya wawe na wapenzi wengi.
Alisema katika utafiti walioufanya waligundua kutokuwapo kwa mawasiliano mazuri kwa wenza ni sababu kubwa ya watu kutoridhishwa na kutokuwa na furaha katika mahusiano yao jambo linalowafanya wavitafute vitu hivyo sehemu nyingine ambapo ndiyo huwa mwanzo wa kupata maambukizi ya ukimwi
Mlawa aliongeza kuwa katika utafiti huo walibaini watu wana hamu ya kuboresha mawasiliano ili kukuza uaminifu katika mahusiano yao kwani mawasiliano ni kiungo muhimu katika kuleta mafanikio
Dk. Mlawa alibainisha kuwa vyombo vya habari vitatumika katika kufikisha ujumbe kwa jamii ambayo inapaswa kuelewa na kutambua matatizo
yanayosababishwa na kutokuwapo kwa mawasiliano
“Champion ni mradi wa miaka mitano wenye lengo la kuhamasisha mjadala wa kitaifa kuhusu majukumu na nafasi ya mwanaume na kuongeza usawa wa kijinsia ili kupunguza uwezekano wa wanawake, watoto na wanaume kuambukizwa Ukimwi na matatizo mengine ya afya ya uzazi,” alisema.
Alisema mradi wa Champion unatekelezwa hapa nchini chini ya Shirika la EnderHealth kwa kushirikiana na Shirika la Academy For Edecational Development kwa ufadhili wa Marekani


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 11, 2010

    People need kumrudia Mungu and then professional couples therapy, professional marriage counseling or psychology counseling will at least do it. Practice communication techniques will never stop a cheating husband/wife nor stop him/her from wanting someone else. Once a cheater, always a cheater.

    Also we need to stop practice arranged and endogamy marriages that some people still do it and some still do it indirect or unintentional for social, economic, political or religion reasons. First arranged marriages restrict personal freedom that contribute matching people who have nothing in common. Parents need to stay away and let kids find their own true loves by themselves.

    Another thing we need to do is to teach people how to find true loves and to learn how to fall in love. People need to love a person for who he/she is and not what he/she has. Marrying to a rich, well known or highly educated person/family doesn’t guarantee happiness in a marriage.

    We need to teach self-esteem among women and reduce peer pressure among young generation. Just because all your friends are getting married and you should jump and find a man to marry you. Also adult should stop peer pressuring young people. Adult should know just because they got marry/married at the age of 21 or younger subsequently their kids needed to do the same. A lot of young people marry/married to please their parents and some are just doing the tradition norm but deep in their hearts they are not ready to settle down…

    Last but not least we need to teach people how to date or gender socialization. Dating in our culture is forbidden or it’s like a taboo. We need to teach people it is okay to socialize with different genders in an appropriate way. In our culture we don’t do the boyfriend/girlfriend thing. If one happens to have a male friend or a female friend you will never see them together in a public places and if parents happen to find it out is a bid deal. How should one find a perfect mate if they don’t hang out together and get to know eah other better? And making people hiding their relationships most of the time contributes to unwanted pregnancies because whenever they happen to meet it is at night or in private areas and letting young people meets in hiding places is not a good thing. If you trust your kids and give them freedon to socialize you will help them in a long run.

    It is better to teach young people gender socialization first and then they will learn how to be good communicators.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2010

    Mtoto wa kitasha katulia utafikir maji mtungini. Kaolewa? Mpeni email yangu mjanjaathumani@hotmail.com

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 12, 2010

    Sasa hizo bilinganya mezani kwenye picha ya kwanza hapo juu ni za nini? Bado sijapata picha ya uhusiano wake na uzinduzi wa hiyo kampeni. Kuna mtu anayeweza kutueleimisha?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 12, 2010

    dr mlawa umeoa???

    lol

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 12, 2010

    BILINGANYA NI MOJA YA LISHE NZURI ASILI KWA WALIOAMBUKIZWA, LABDA UNGEULIZA KWANINI KILA UZINDUZI LAZIMA UWEPO MUZIKI NA NGOMA? JE, HUWA HATUELEWI KITU BILA YA KUTUMIA MUZIKI AU TUNAPENDA STAREHE?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...