Mratibu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Angelo Luhala akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari walifika katika mkutano wa waandishi wa habari ulioitishwa leo na kampuni ya bia TBL katika ukumbi wao wa mikutano.katikati ni Mkurugenzi wa TBL,David Minja na kulia ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe.
Mkurugenzi wa masoko wa TBL,David Minja (kati) akiwa na Mratibu wa BASATA,Angelo Lihala (shoto) pamoja na Meneja wa bia ya Kilimanjaro,George Kavishe kwa pamoja wakionyesha mfano wa tuzo watakazopewa wasanii washiriki wa Kili Music Awards.
Baadhi ya wanahabari waliofika katika ukumbi wa mikutano wa TBl,wakifuatilia kwa makini mkutano huo uliofanyika leo.
Hatimaye safari ya mchakato wa kumpata mshindi wa Tunzo za Muziki Tanzania umefikia ukingoni. ambapo.
Mchakato wa upigaji kura ulianza rasmi tarehe 1 mwezi Aprili 2010 na unaendelea hadi tarehe 13.Mei.2010. Taarifa kamili kuhusu mchakato huu unapatikana kupitia tovuti ya www.kilitimetz.com pamoja na vipeperushi na magazeti mbali mbali.
Tarehe 14 mwezi wa Mei ndio usiku wa kuwatunuku washindi katika vinyang’anyiro mbali mbali vya Tunzo za Muziki Tanzania. Usiku huu ni kwa mwaliko tu. Wana habari watapata mialiko kupitia vyombo vyao vya habari na kutakuwa na pasi maalumu kwa ajili yao ikiwa ni pamoja na eneo lao liliotengwa mahksusi kuwawezesha kufanya kazi yao kwa ufanisi. Na tahere 15, yaani siku ya pili hapohapo Diamond Jubilee kutakuwa na tamasha la washindi na hili ni kwa wadau wote.
Usiku huo utapambwa na burudani kutoka kwa wasanii wa ki Tanzania pekee.
Nao ni:
1. AY.
2. Fid Q.
3. Joh Makini.
4. Marlow.
5. African Stars – Twanga Pepeta.
6. Mwansiti.
7. Lady Jaydee.
8. Mzee Yusuph na Offside Trick
9. Wahapahapa
10. Ali Kiba
Mwaka huu Kilimanjaro Premium imeboresha zawadi mashindano hayo pamoja na Tunzo yenyewe.
1. Zawadi za pesa taslim zitakazotolewa kwa ujumla ni TZS 15M.
2. Katika maboresho ya Tunzo zenyewe, Tunzo mbili kubwa za Hall of Fame zitakua “GOLD PLATED”.
3. Kila mteule na mshindi watapata cheti cha utambulisho wa ushiriki wake katika Tunzo za Muziki Tanzania.
Msanii Sean Kingston kutoka Marekani ndiye atapamba hafla ya Tunzo na kushiriki kwa kutoa Tunzo ya wimbo bora wa RAGGA.Taarifa kamili na ujio wa msanii huyu zitatolewa katika mkutano na wana habari utakaofanyika tarehe 13. Mei. 2010.
Taarifa ya ziada
Kilimanjaro Tanzania Music Awards inayofuraha kuwakaribisha Malaria No More (MNM) katika kinyang'anyiro cha Msanii bora Anayechipukia.Malaria No More (MNM) wameongeza thamani Tunzo hiyo kwani mshindi atakayepatikana atakwenda nchini Senegal katika shughuli na onyesho la pamoja na Msanii mkongwe wa Africa anaefahamika kwa jina la Youssou N'dour.


MSONDO OYEEE,HAYAHAYA SHIME WANANCHI MNAOMBWA KUIPIGIGIA KURA BENDI BORA KILO YA TANZANIA KATIKA CATEGORI YA WIMBO BORA KIBAO NI HUNA SHUKURANI.MSONDO NGOMA NI YETU SOTE WATANZANIA "MSONDO NGOMA YA WATANZANIA HA HA HA HAAAA"
ReplyDeleteTahadhari! Hao watu wa Malaria No More muwe makini nao sana tafadhali, maana usanii umezidi. Hiyo offer yao inaweza kuwa ni sound, mwishowe watampeleka mshindi mpitimbiii!
ReplyDelete