Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Vicky Nsilo Swai, akishirikiana na Kamati ya maandalizi Dar es Salaam ana Heshima ya kukualika/kuwaalika kuhudhuria hafla ya Chakula cha Jioni cha Hisani Mei 14 2010,saa 1.00 kamili jioni kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro wa kugharamia shughuli za uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Mgeni Rasmi ni Mwenyekiti wa CCM Taifa
Mheshimiwa Rais Jakaya M. Kikwete.
Kiingilio: Shs. 50,000 kwa mtu mmoja Shs. 60,000 kwa Bwana na Bibi
Ukumbi: Golden Tulip Hotel,Masaki,Dar es Salaam

Tiketi zinapatikanaOfisi za:

Frontline management
2nd Floor S&F Building
Mwinjuma Road, Kinondoni
Tel: 0614 105 136
Email: info@frontline.co.tz

Au wasiliana na:
Brig Gen (rtd)- R.N. Chonjo- Mwenyekiti,Cell: 0754 320 740
Innocent Macha- Mtunza Hazina, Cell: 0754 222 036
Aggrey Marealle- Mjumbe Cell: 0784 266 782

`

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 12, 2010

    Watanzania alietuloga kafa

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2010

    Ndesamburo Moshi mjini, Mbowe Hai. CCM hata mkusanye milioni ngapi hatuwataki sisi huku, tutawalia hela zenu lakini kura hatuwapi ng'o!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 12, 2010

    nani kakudanganya ndesamburo atalitetea jimbo la moshi mjini,katika majimbo ya chadema ambayo ccm wanauhakika wa kuyarudisha ni moshi mjini na karatu,hesabuni siku tu nyie.habari ndo hiyo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 12, 2010

    Kwa kusisitiza tu hoja za mdau hapo juu Sisi ndo wakazi wa moshi hakuna cha JK hakuna cha Aggrey Marreale CHADEMA tu mpaka kieleweki waizi wakubwa hawa

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 12, 2010

    Jamani hivi hatuwezi kuwa tunafanya harambe kama hizi tusaidie mahospitali na kujenga mabarabara, usafi wa majiji etc. Sisemi CCM wamekosea kufanya harambee ni haki yao kama chama. lakini as a country hizi strategy ni muhimu kutumika kusaidia nchi nzima kama tunaona kodi haitoshi kumpa kila mwananchi basic needs. Pamoja tunaweza jamani.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 12, 2010

    kiingilio 50,000/=

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 12, 2010

    ni wazo zuri sana kuchangia chama ktk mazingira ya uwazi, lakini ni vyema rais jakaya kikwete angewataarifu wanasisiemu kwanini wasitumie utaratibu wa zamani kupata fedha za kampeni... angetaja ni wapi uchaguzi uliopita alipata fedha na ktk mazingira yapi na kwanini utaratibu huo hautatumika sasa, kwanini umeshindwa na kutuingiza ktk utaratibu huu mpya

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 12, 2010

    I stand to be corrected....but this biashara inakidhalilisha chama......sorry if CCM will feel offended!......but wazee wangu HII KITU HAIPENDEZI kabisa.

    ReplyDelete
  9. Kura ya wafanyakazi - JKMay 12, 2010

    50,000 kiingilio kuchangia CCM ili muendelee kuiba .... tehee teheeee teheeee tuhuu tuhhuuuu, si asafari niitumie kuingia miss tanzania, kenge nyie CCM.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 12, 2010

    Kwa uchungu gani uliowashika mpaka kupata wazo kuita wananchi wawape mchango?........Kwanini wazo kama hili msingelitumia kuombea PESA YA BARABARA say FLY-OVER japo moja!!Wewe anon namba moja hapo juu niko pamoja na wewe.......JK acha kucheka na watu...hivi kweli una ADVISORS?.....halafu hao vikongwe uliowarithi kutokea ENZI ZA MWALIMU wanakusaidia nini JK??.....Ebwana unatakiwa ukaze buti kweli kweli....dakika ndo zinayoyoma na inaelekea kwamba pamoja kwamba tunakuaminia wewe ni mtoto wa mjini lakini your leadership imetetereshwa na WACHOVU waliokuzunguka na wanaoshindwa KUKUSHAURI IPASAVYO.....endelea kuwakumbatia na kuwachekea-chekea...ila usije kumtafuta mchawi wako!

    ReplyDelete
  11. SASA HAWA JAMAA, MIAKA YOTE WALIKUA WANATOA WAP? HELA ZA KAMPENI , NA HAWA HAWA WAMEKATAA KUONGEZA MISHAHARA KWA WAFANYAKAZI NA KUWATUKANA SASA WANATAKA MICHANGO GANI? NA TUTOE WAP?

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 12, 2010

    Nimejaribu kuDeep namba ya Mjumbe naona haipatikani.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 12, 2010

    Hivi kima cha chini cha mtu ukachangie chama cha siohasa jamani hii imekaaje

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 12, 2010

    Wazo la mchango ama harambee sii baya ila liliko tokea ni msala mbaya sana kwa maana mwenye kiti wa mkoa mama nsilo swai ndio chanzo cha kuzorota kwa maendeleo ya chama. Sijui kwanini mwenyekiti wa taifa hulioni hili. watu hawapendi chadema wanampenda ndesa kwaajili ya uzembe na upofu wa mwenyekiti wa ccm taifa. Kwa mikono na akili yake mwenyewe anakimaliza chama

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 12, 2010

    Tusiwe na maneno tu. Tuwe na matendo pia. Sasa jamani wenzangu mmejiandikisha kupiga kura? Kama tayari, basi poa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...