Kaimu Balozi Mh. Victoria Mwakasege akiwa na
Haruna Moshi 'Boban' (shoto) na Afisa Ubalozi, mdau Yusuph Mndolwa
Kaimu Balozi Mh. Victyoria Mwakasege akiwa na Haruna Moshi Boban na Afisa Ubalozi, mdau Jacob Msekwa
Mwanasoka wa kulipwa anaesakata kabumbu kwenye timu ya Gefle IF nchini Sweden Haruna Moshi 'Boban' wiki hii alitinga Ubalozi wa Tanzania jijini Stockholm na kukaribishwa na Kaimu Balozi, Mhe. Victoria Mwakasege, ambaye alimpongeza sana Moshi kwa mafaniko makubwa aliyopata ya kucheza kwenye ligi kuu ya Sweden. Kaimu Balozi alimtaka mchezaji huyo mwenye kasi asiridhike na hatua aliyofikia na aendelee kuongeza bidii. Pia alimtaka awe balozi wa kulitangaza soka la Tanzania na pale patakapokuwa na uwezekano ajitahidi kuwatafutia timu vijana wengine wa kitanzania ili nao wapate nafasi ya kucheza soka nchini Sweden kama yeye.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2010

    Mkuu Yussuph Mndolwa mdau wetu usiye na makuu unajichanganya na kila mtu bila jali ana nini na ni nani,Mungu akuzidishie mkuu uzidi kupata.wadau wako kula pweza na usakata twanga pepeta na kata ya kinondoni.wakilisha mkuu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2010

    Hongera Haruna,kaza buti songa mbele,soka la TZ ni Simba/Yanga na siasa nyingiiiiiiii wala hakuna future plans for young players.all the best kaka.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 28, 2010

    Kama Boban amekuwa na mawazo ya kutembelea ubalozi bila shaka amebadilika, hongera Boban. Sasa ni zamu ya chuji kuiga mfano wa rafiki yake na kutafuta timu ya kucheza nje maana uzee unakaribia tusingependa kuona "star" kama hawa wakihangaika mitaani wakati wa uzee wao na mifano ni mingi!!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2010

    longtime boban,big up man
    cm

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 28, 2010

    Hongera Yusuph Mndolwa.
    mafanikio yako ndio yetu.
    Haruna Mbeyu.

    ReplyDelete
  6. kazana mdogo wangu nakutakia kila la heri

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 28, 2010

    Wakuu wa Ubalozi kuweka milango wazi kwa mapokezi ya watanzania wawakilishi katika fani za ngoma za utamaduni,wanamuziki na michezo kama mchezaji Haruna Boban ni hatua kubwa saana kimaendeleo kwa vijana wa Taifa letu Tanzania.
    Mickey Jones

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 28, 2010

    Balozi zetu zimebadilika, siku hizi ziko mstari wa mbele kwa national interest. Haruna Moshi mpe salamu MAXIMO tunataka aondoke zake Brazil hana mpango wowote wa anabania mastar na kuweka vibonde katika time ya taifa, subiri Rwanda watatutoa nduki kwao.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 28, 2010

    sawa michu kwa kubania comments zangu, nilichosema ni kweli, ungeliweka hapa comments zangu na ukawacha watu either wakubaliana nami au wakatae kuliko kuweka kapuni.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 28, 2010

    Kaimu Balozi Mwakasege Oyeeee

    Wadau Oyeeeee

    Boban Oyeeee

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 28, 2010

    kama anavyosema director mbeyu, tunakuombea kila la kheri mzee mndolwa, nimekumbuka enzi za ununio! seha

    ReplyDelete
  12. Mdau K.VMay 28, 2010

    All the best Boban............
    Kaza buti......

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 29, 2010

    All the best Boban...

    Mimi ninaswali nataka kujua kazi za kufanya kwenye ubalozi zinapatikanaje? Mimi nataka kufanya huko kwenye ubalozi wowote tu.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 29, 2010

    Kaka yangu Msekwa hongera umenenepa sana. Mambo yako super, nawe Mndolwa endelea kutuwakilisha vizuri huko.

    Ze Mdauzi.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 29, 2010

    MIMI NAMPONGEZA BOBAN KWANI NI ANGALAU TUMEANZA KUWA NA WACHEZAJI KTK LIGI KUU ZA ULAYA NI MAENDELEO NA KAMA WATANZANI TUKIWAPA SURPORT BASI HARUNA,HENRY JOSEPH,MACHUPPA,CREDO MWAIPOPO,NIZAR KHALFAN PAMOJA NA WENGINE AMBAO WANACHEZA KTK LIGI MBALIMBALI ZA ULAYA WATAKUWA WAMETUFUNGULIA NJIA. MIMI NAISHI DANMARK SASA HIVI NAWEZA NIKAJIVUNA KUWA TANZANIA TUNAPIGA HATUA. KILA KITU KINA MWANZO. TUSHIKAMANE TUSIONEANI WIVU JELOUS SIYO MZUKA. HONGERA HARUNA MOSHI BOBAN NA WACHEZAJI WENGINE WOTE KWA KUITANGAZA TANZANIA. MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...