Mshindi wa Miss Dar Intercollege ,Rose John kutoka chuo cha Ustawi wa Jamii (kati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili,Cassiana Milinga kutoka chuo cha biashara CBE (kulia) na mshindi wa tatu Marylidya Boneface nae kutoka chuo cha Ustawi wa Jamii.
Miss Dar Intercollege 2010,Rose John akiwa pamoja na wenzake alioingia nao katika tano bora,toka kulia ni Joyce Baluhi ambaye ameshika nafasi ya nne,Cassiana Milinga ameshika nafasi ya pili,Marylidya Boneface nafasi ya tatu na Agather Killala nafasi ya tatu.
Mratibu wa Miss Dar Intercollege,Vicky Kimario (kushoto) akiwa pamoja na mama wa mitindo Tanzania,Mama Asiah Idarous ambaye ndie aliefanya kazi kubwa ya kuwapendezesha warembo hao siku ya leo wakiwa katika picha ya pamoja na warembo watatu bora.
tano bora.
washiriki wote wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchujo kufanyika.
Barnaba na Lina wakiwaburudisha wadau waliofika katika klabu ya kimataifa ya Bilicanas kushuhudia kupatikana kwa mrembo wa Dar Intercollege usiku huu.
warembo wacheza shoo yao kwa style ya kipekee kabisa.
Barnaba na Amin wakifanya vitu vyao usiku huu ndani ya klabu bilicanas.
majaji wakifuatilia kwa makini mtanage huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2010

    Kuna Miss ....Tanzania and so and so a lot in Tanzania especially Dar. What is going on down there? Hivi ni uzuri au imekuwa biashara? Unashindwa kujua Mrembo hasa wa Tanzania ni yupi? Maana kila kona kuna Miss something. Naona kuna Miss Kata, Miss Tarafa, Miss Wilaya, Miss Mkoa, Miss Mji, Mis Capital Dodoma etc...Please paraents Just wondering I think it is too much hata maana ya urembo inapungua. Anyway they are all beautifull!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2010

    ".....nawaangazia warembo kama uncle Hashim Lundenga...."

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 28, 2010

    sijui ni vipi huyu alishinda, walimuangalia tabasamu lake lakini?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2010

    Hii imekuwa bishara nzuri sana tanzania, mimi naona soon kutakuwepo mashnidano ya miss porn star hapa nyumbani. mind my words, sio mbali, ni karibu tu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 28, 2010

    hawa wanamuziki vipi mbona pichani wanaonekana afya mgogoro?au ndiyo style za vumbi maana hapa hatu zungumzii unene bali muonekano wa lishe ktk ngozi!! jipendeni jamani hata kuvaa vizuri pia nimuhimu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 28, 2010

    hii inanitahadharisha sasa kwamba inabidi kurudi tz kidogo angalau nizoee sura za wabantu wenzangu,maana vinginevyo mtasema najifanya,kusema kweli hapo mimi sijaona mrembo,ila wote ni wazuri .
    hii ndiyo taabu ya kukaa uzunguni muda mrefu,ukizoea sura za kizungu za kikwetu zinakupa butwaa kiasi kuchambua mrembo nani kati yao.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 28, 2010

    Naungana na Anon. wa Fri May 28, 05:48:00 AM, it's just too much kwa kweli. Punde si punde tutaongezewa list kwenye menu i.e. "Miss Kula Kidogo", "Miss Movies", "Miss Nyagi/Nguvu", "Miss Chips Kuku", "Miss Kudesa", "Miss Roho Nzuri", "Miss Kusali", "Miss Miss/Single", "Miss Mkemwenza", "Miss Mke wa Celebrity", "Miss Wawaaa" etc.

    By the way, hivi yule dada muigizaji aliyekuwa akiitwa Nina yuko wapi siku hizi????

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 29, 2010

    SWALI: Kuhusu huyo dada jaji wa pili kushoto, amevaa kitu kingine kweli mwilini mwake mbali na hiyo hereni moja na hicho kidude mkono mmoja? Hiyo picha imechomekewa (graphics) au ni kweli alikuwepo hivyo hivyo?

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 29, 2010

    anko michu,ningependa kuuliza wadau,hivi huyo dada wa 2 kutoka kulia picha ya mwisho kabisa amevaa nguo?ameleta gumzo kubwa sana hapa kitaa...

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 29, 2010

    na pia tunaomba warembo watumie majina yao ya asili sio catherine john,christina joseph tafadhali kutokuweka jina asili si ushamba wala haikupunguzi
    pointi katika ushindani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...