Mzee Hassan Dalali (shoto) akimkabidhi kombe la ubingwa la
ligi kuu ya bara mwenyekiti mpya wa Simba sc Aden Rage
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba, Hassan Dalali (kushoto) akimkabidhi kombe la ubingwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage wakati wa makabidhiano wa ofisi pamoja na mali za klabu hiyo yaliyofanyika leo Makao Makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Msimbazi jijini Dar leo. Shoto ni Katibu Mkuu mstaafu Mwina Kaduguda




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Didi DrogbaMay 18, 2010

    DUU!PICHA ZOTE HATA KUTABASAMU HAKUNA?AU BADO MMELEWA KIPIGO CHA AIBU MLICHOKIPATA MISRI?HEBU CHEKENI KIDOGO BASI JAPO KWA AJILI YA KUPATA PICHA NZURI,KIDOOOOOGO KADU NAONA NDIO ANATABASAMU AT LEAST,LAKINI ADEN NA MZEE DALALI HAWATAKI HATA KUTIZAMANA

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 18, 2010

    kimsingi mi namkubali mzee wetu Dalali na nasema asante na hongera kwa mambo makubwa uliyotufanyia wana simba lakini
    1.katiba tuliyonayo ni ya wanasimba na wewe ni mmoja kati ya wanasimba na hatuna budi sote kuifuata
    2.cheo ni dhamana tulidhike pindi wenzetu wanapo omba dhamana hiyo pia kwani hii ni taasisi-KWA HILI HONGERA KWANI UMEKUBALI MATOKEO JAPO KTK PICHA UNAONYESHA KM VILE HUKUBALI.
    3.UMEONDOKA WAKATI TIMU IKIWA KWENYE MAFANIKIO MAKUBWA HIVYO NI RAHISI KWA WANACHAMA KUKUMBUKA KULIKO KUSUBIRI TIMU IWE PABAYA NDO UONDOKE HAPO KUMBUKUMBUKU ZA SISI ULIOTUONGOZA ZITATUELEKEZA KWENYE KUFELI TU LAKIN SASAHIVI ZINATUELEKEZA KWENYE MAFANIKIO.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 18, 2010

    Liko wapi hilo kombe?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 18, 2010

    Hivi ndivyo inavyotakiwa! Uwajibishwaji! Kama mtu, hasa aliyepewa dhamana fulani na umma, akiboronga ama akijihusisha na utovu wa nidhamu wa hadhara, ni shurti awajibishwe kwa maslahi ya umma.

    Hakika wana Simba leo hii tunalia machozi ya furaha, kwani Bwana Dalali alikuwa anaipeleka timu yetu pabaya. Alikuwa anatunadia mashabiki wetu wote kwa Yanga!

    Japo maamuzi hayo ya kumuwajibisha Bwana Dalali yalikuwa ya chini chini, na ilitumika busara ya kulificha hili jambo kwa kuitisha uchaguzi, lakini habari zinasambaa na zimetufikia wahusika.

    Bwana Rage, karibu sana kutuongoza na kuturudisha kwenye hadhi yetu wana Simba, maana tunatetereka. Bwana Dalali, na ukapumzike kwa amani, ndio ukubwa huo, cheo ni dhamana!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 19, 2010

    inaonesha liko kwake hili kombe mweeh

    ReplyDelete
  6. ObserverMay 19, 2010

    Katika kauli iliyonishangaza ya Mzee Dalali ni alivyosema wakati yeye anakabidhiwa uenyekiti hakukabidhiwa ofisi kama alivyomfanyia Rage, sana sana alikabidhiwa funguo za choo !!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 20, 2010

    LIPO TATIZO LA MSINGI. AMA NI KWA VIONGOZI AU MFUMO WA VILABU ULIOPO. KADUGUDA ALIPOINGIA MADARAKANI ALIKUWA NA NDOTO ZA KUIFANYA SIMBA IWE KLABU KUBWA BARANI AFRIKA. MWISHO WAKE AKAKATA TAMAA. RAGE AMEANZA KWA NGUVU.

    NAMUOMBEA MUNGU KAKANGU KUTOKA KULE RUFITA KWETU TABORA.
    LAKINI.... AKAE NAO AJIFUNZE KWANINI WALIOKUWA NA NDOTO KAMA ZAKE HAWAKUFANIKIWA? RAGE SIO MGENI SIMBA LAKINI ZAMANI SI SASA.
    MDAU- MNYAMWEZI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...