Zeituni Obama

Shangazi wa Rais wa Marekani Barack Obama amepewa ruhusa kubaki nchini humo baada ya kuomba hifadhi ya kisiasa kwa mara ya pili.

Zeituni Onyango, aliyezaliwa baba mmoja na Bw Obama, anaendelea kuishi katika nyumba za umma huko Boston baada ya kukataliwa alipoomba hifadhi hiyo mwaka 2004.

Aliomba tena baada ya kujulikana hadharani kuwa anakaa kinyume cha sheria wakati wa kampeni ya Bw Obama mwaka 2008.

Wakati huo Bw Obama alisema hakujua kwamba shangazi yake alikuwa Marekani kinyume cha sheria.

Watu wanaotafuta hifadhi Marekani lazima waonyeshe kuwa wanateswa nchini mwao kwa misingi ya dini,asili, utaifa, kwa kutoa maoni ya kisiasa, au kujihusisha na kundi la utetezi.
Habari kamili nenda BBC Swahili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 18, 2010

    duuh kweli maisha mihangaiko sana.sasa hao Marekani wamkumbuke Mwanakijiji wa jamii Forums.maana misiba na mambo mengi yanatokea nyumbani anashindwa kuja.

    hata kampeni za uchaguzi angekuja kuwapiga tafu Chadema.lakini ndio hivyo mambo bado hayajakubali.lakini dalili ya mvua ni mawingu kama Zeitun Obama kapata basi naye atapata.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 19, 2010

    Kidogo niseme JAMES BROWN.Kumbe ni shangazi yake mtu.Ebana eeeh kweli duniani kuna watu wamefanana.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 19, 2010

    sasa uyu shangazi kwa ukimbizi gani hasa alionao toka 2004 na sasa??

    aibu hii...kisa obama rais

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 19, 2010

    Du..Anafanana na Michael Jackson

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 19, 2010

    wewe uliyesema kama James Brown umeniwahi, mimi nilitaka kusema kama Michael Jackson.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...