Hapa Iphone ikitwa na namba ya ankal
Ankal samahani, nimerudi tena. Ila awali ya yote naomba nikupongeze wewe na skwadi nzima ya Globu ya Jamii. Its unique and quite contaigious. yaani ukiionja tu huachi. Na yote hii ni kwa sababu tofauti na wengine wewe umejikita katika jamii haswa. Jambo ambalo vyombo kibao hapa nyumbani wametindikiwa. Wao kazi ni habari za viongozi, warsha, kongamano, semina na sijui nini... Lakini Globu ya Jamii aaaaahh.... Lolote lile twende. Na hii ndio raha ya mtandao. Yaani humu ni raha na saa ingine karaha kwa kwenda mbele.
Sasa bwana, kwanza nikushukuru kwa kuposti hiki kimeo changu cha iPhone yangu hii (naam, ni ya 3GS gamba jeupe) ambayo imebuma, na haitaki kufunguka, hivyo siwezi kufanya lolote. Cha ajabu hii leo nimekuta kwamba nikipigiwa simu naweza kupokea kama kawaida na kuongea uzuri tu. Pamoja na maelezo mazuri ya wadau kibao katika mtundiko wa kwanza, naomba niwasumbue tena kwa kuomba msaada kwenye hili jituta.
Hiki kimeo changu kama kime-lock mbona napata simu nikipigiwa? Ushahidi ni huo ankal ambapo umenipigia kwa namba niliyokupa na hiyo hapo inaita. Si unaona mwenyewe?? Sasa wadau kulikoni???? Naomba msaada jamani. Humo ndani kuna namba kadhaa ambazo ni muhimu kweli. Moja ni ya shemeji/wifi yenu ambaye yuko ughaibuni masomoni, nami siikumbuki kwa kichwa. Naomba muendelee kunielewesha wadau namna ya kutanzua kitendawili hichi.
Naomba ankal na wadau msinichoke
Mdau wa iPhone
Hapa kwikwi..
Mtundiko wa awali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2010

    ulisha jaribu kwenda kuflash hiyo sim.kama bado jaribu njia hiyo labla itafunguka.

    mdau
    usa

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 24, 2010

    yaani mi ningekuwa dio huyo mwanamke nimeshakupa talaka, yaani inakuaje namba ya mtu wako muhimu hiyo hauikumbuki kwa kichwa? au ndio unamchuna mwenzako, anabeba mabox ili akuletee wewe iphone lakini hata namba yake hauijui.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 24, 2010

    mchinz huo!! vitu vya kupew pewa bure navyo si poa~~

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 24, 2010

    Iko disabled unaweza kureceive na kupiga emergency
    Hiyo iphone sijui ya Italy? Spain?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 24, 2010

    mjomba alikuwa likizo sasa anarudi urahiani kula bata zaidi

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 24, 2010

    na wewe una bore na kasimu chako cha kupewa !! sasa unataka sisi tufanye nini!! ebu kaka michuzi tuwekee habari za maana

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 24, 2010

    ndugu yangu pole, hayo mambo ya ni ya kawaida hata magari sometime yanasumbua,sasa ndugu yangu unaweza kunisaidia iyo serial no. hapo nyuma then nijue maker ni nani maana hapa japan huwa zina agrement! kwa miaka 2, hivyo you are innocent! kosa ni lao. ukinpatia mie nitaenda kuuliza hata kama ni nje ya mkataba! nitapata ufumbuzi maana hata mie ni shughuli zangu kiasi flan eletron. lakin namba ya shemej usifanye hivyo next time utamvunja moyo tunaonekana hatujali! wao ni wepesi mno kwa kushika namba zetu.
    asante, mdau japn.

    ReplyDelete
  8. Ankal nashukuru kwa kupata namba yako ya simu nilikua naona aibu kukuuliza waosha vinywa wangenizodoa.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 24, 2010

    Simu yako ipo "carrier unlocked" ndiyo maana unaweza pata network inatakiwa kuwa unlocked " jailbroken" kuweza kutumia vitu vingine

    Kuna tools nyingi za kui unlock ila kuwa makini unaweza lock simu yako kabisa kama uki upgrade baseband ya simu yako. Usi update simu yako for now kwenye itunes

    Kwa maelezo zaidi wasiliana nami

    josh17tz@yahoo.com

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 24, 2010

    Hiyo simu imeibiwa huko USA na ndo maana imepigwa lock

    ReplyDelete
  11. Ndugu yangu hiyo itakuwa iphone ya kichina. ama kweli mchina nuksi, eti iphone inaingia laini tatu na inauzwa laki moja!!!????Pole kaka

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 24, 2010

    ndo faida ya vitu vya kuiba,kwani huyo aliyokupa hakukupa na kitabu,navvyojua kitabu cha Laptop au simu za maana lazima kiwe na lugha zote za kimataifa,sasa Google tatizo lako kwenye internet nautapata ufafanuzi.
    Michuzi hii habari inaboa sasa, namimi chupi yangu haitakati wadau nisaidieni jamani

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 24, 2010

    Huna haja ya kusumbuka kakaangu,hiyo simu sio original iphone,nik=likuwa nayo hiyo ni kutoka china kaka,iphone ya ukweli haifanyi hivyo kabisa!kama hiyo mtu alikuletea zawadi mrudishie ili aende aliponunulia wataitengeneza au kumpa nyingine akiwa na risiti aliyonunulia,oher than that unapoteza muda kuuliza hakuna atakayekusaidia.Asante sana.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 24, 2010

    Kaka the problem with iPhone is hutajua lini itafunction well na lini italeta matatizo, anyway im a great user of iPhone and i have unlocked and jailbreak many of them, the problem is with the version, it seems you upgraded to 3.1.3 which has alot of bugs and it needs alot of bug fixes,one of them is screen display and lapse of time on application,Blackr1an they haven't come with cracked one yet for you to fix the bugs or should i say errors and if it is version 3.1.2 also there some issues where by blackr1an cant fix. I am in Tanzania Arusha to be specific,if you wish we can downgrade the version and then later upgrade to its original firmware. Pole najua jinsi iPhone zinazingua wa Tz wengi but the technology is far advanced compared to any Mobile phone you have to be very extra careful to what you download and its operation or else this is what usually happens for misuse.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 24, 2010

    Muheshimiwa simu yako iko JAIL BROKEN, that simply means UNLOCKED IPHONE,

    The only way out, ni kuirestore to factory settings, and that MEANS itakuwalocked again, you will have to unlock it again by JAIL BROKE IT)..

    This is what you have to do..
    You need to download itune from apple website.

    open itune on the computer while connected to internet,

    Connect the iphone using cable provided onto the computer.
    and follow through instructions on how to restore it, to factory settings,
    1. Hold Power button on TOP, and HOME button at the same time, until it shut down and the APPLE LOGO APPEAR, LET GO OF POWER BUTTON and still holding HOME BUTTON, and until the plug IN ITUNE logo appear. NOW YOU HAVE THE CLEAN IPHONE..

    Continue with the onscreen instruction on ITUNE in your PC

    Once you have done that, i will provide you with further info on how to jail broke it again, but YOU WILL LOOSE ALL THE APPS AND PHONE BOOKS.

    or alternatively there are alot of info on how to JAIL BROKE your phone(2G/3G) to use on other NETWORKS. you just need to do your home work.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 24, 2010

    Hallow Halloow!

    Tunatumai itafunguka.

    Wadauz 1 & 2 oyee!

    Changamsha Baraza! Lol!

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 24, 2010

    Hallow Halloow!

    Tunatumai itafunguka.

    Wadauz 1 & 2 oyee!

    Changamsha Baraza! Lol!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 24, 2010

    ni wasiwasi mwenye simu hii ni ankal mwenyewe anataka msaada wa kuitoa lock ila kaona noma msimwambie anayo simu ya wizi , ANKAL usione noma we sema tu kama ni yako ,usjali

    mdau
    kkoo

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 24, 2010

    Hapo Approximately ni kama miaka 80 ya kusubiria ha ha ha ha haaaaaaa

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 24, 2010

    HIZO DAKIKA ZA KUSUBIRI NI ZAIDI YA MIAKA 15000 JE UTASUBIRI MIAKA HIYO ILI IFANYE KAZI TENA? UNAPOKEA SIMU NA UNAWEZA KUPIGA EMERGENCY KWA SABABU WENZETU WANAKAUTU KIDOGO, KWA EMERGENCY KAMA MOTO AU KUUMWA UNATAKIWA KUITA AMBULANCE AU FIRE ENGINE KUOKOA MAISHA YAKO SASA WANAKURUHUSU KUPIGA ILI WAO WAONDOWE LIABILTY KWANI WAKIKUFUNGIA SIMU MOJA KWA MOJA NYUMBA IKAWAKA MOTO NA UKAFA WEWE AU NDUGU KWA AJALI HIYO BADO UTAKUWA NA HAKI YA KUWASHITAKI HATA KAMA HULIPI MBILI KUWA WALIKUFUNGIA SIMU HUKUWEZA KUITA FIRE ENGINE, HII SHERIA NINAYOIZUNGUMZIA NI YA MAJUU SI TANZANIA, KWANI WAO BADO HIYO SIMU INAHESABIKA IKO KWAO THE SAME KWA KUPOKEA SIMU HAWAWEZI KUKUFUNGIA KWA SABABU WANAPOKUPOIGIA KWA MANTIKI YAO KAMA WANAVYOFIKIRIA KUWA SIMU BADO IKO NCHINI MWAO THEN WANAPATA PERCENTAGE FULANI KUTOKANA NA WEWE KUPIGIWA KWANI SYSTEM YAO INTAMBUWA KUWA BADO UKO NDANI YA JURISDICTION YAO

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 24, 2010

    bwana michuzi asante kwa ushirikiano(polisi jamii)mwizi wangu nimempata leo,simu hiyo nilitumia mwezi tuu!

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 24, 2010

    Hi,
    I am technical support agent and when you get iPhone is disabled,try again in....,....,mins" it is usually cause of inserting the wrong passcode more than once.
    What you can do is force restore the iPhone thru iTunes(a program u download thru www.apple.com/itunes/download).Be prepared to loose all your data unfortunately....Weka email yako ili nikutumie the article you need to follow in force restoring your iPhone or if you can get into www.apple.com/support and search for article HT1808
    Hope it works,
    All the best...

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 24, 2010

    Hivi kuwa na iphone ni deal sana bongo nini? Apart from making and receiving calls what else can one do with iphone in Tanzania?

    Hiyo simu kama iliibiwa kuwa makini. Interpol may track you down. Are also sure that the phone is not linked with terrorist activities?

    Utakuja kufa hivi hivi kwa vitu vya dezo.

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 25, 2010

    iphone inatakiwa izimwe once a week since hiyo ni kama computer so u nid to refresh it.hii ni info kwa wote wenye iphone...nwy on your case inaonakena umeichezea mno hiyo cm..mpka na language imejirudisha kwenye ts original sertings..nwy shikilia button ya kuzimia na hiyo button ya chini..press and hold 4 few secondz itatokea screen inasema slide to power off..na chini cancel..slide hiyo ya slide to turn off..leave it for few hrz..even ucku mpka asubuhi..thn iwashe tena..maybe this will help..ila inaonekana kama thats not ur 4ne..na umejaribu sana kuiweka wrong passcode..ndio imereact..na kuiflush ma dear uwe na atleast laki moja..so yeah..gud luck..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...