bro michu vipi?
Nimeshtuka leo kukuta hii mada hapa kwako ikiwa na jina langu: isaac mwamgogwa. Kiukweli ni kwamba mimi niliibiwa password ya email yangu kisha jamaa wakachukua contact zote ndani halafu wakaanza kuwatumia mail kama hizi watu wote humo kwa jina langu.
Kiukweli sio mimi ninayeomba msaada wa pesa ila ni hao jamaa walioniibia hiyo password ndio wanatumia.toka kipindi hicho mpaka sasa nimepata usumbufu mkubwa kwani kuna watu wametuma pesa kwa hao jamaa wakizani ni kweli ni mimi nina shida.
Licha ya hiyo pia kuna mambo mengi ambayo jamaa wanaendelea kusumbua watu kutoka kwenye hio mail address.isaac mwamgogwa ni mimi na sina shida yoyote mahali popote na ninakanusha kwamba sijamtumia mtu yeyote mail ya kuomba msaada.
ahsante.
mdau isaac mwamgogwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 23, 2010

    POLE SANA MDAU KWA YALIYOKUKUTA.KWA KIFUPI NI KWAMBA HAYA MAMBO YASINGETOKEA KAMA UNGABADILISHA PASSWORD YAKO MAPEMA.PILI MDAU UWE NA TABIA YA KUBADILI PASSWORD MARA KWA MARA.HATA MWIZI AWE MTAALAMU NAMNA GANI HAKUPATI NG'O.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 24, 2010

    Aise kaka pole sana. Hata mimi ilishanipata hii vile vile na moja kati ya marafiki zangu akawatumia kiasi kikubwa tu cha pesa akidhani ni mimi. Sasa nilichofanya nilijaribu tena kuingia kwenye hiyo hiyo email address yangu iliyokuwa hacked lakini kwenye password nikabadilisha. Na kwa mshangao ikafunguka na nikaona upuuzi hao jamaa waliokuwa wanaufanya kutuma emergency emails eti nimekwama London na nimeibiwa bag langu na documents za kusafiria na sina hata pesa za kulipia hoteli nilioshukia. Halafu inaonekana walisoma email zangu za zamani jinsi ninavyoandika kuanzia kusalimia hadi kumalizia na wakakopi hiyo format....kwa hivyo ilikuwa vigumu kwa contacts zangu kusita kuwa ilikuwa sio mimi. Yaani niliudhika sana. Basi hebu jaribu jinsi nilivyokushauri ili uweze kuwablock kutoendelea kuiabuse.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 24, 2010

    Sina hakika kama issue ni kubadili password mara kwa mara. (Mi natumia password yangu tangu 2003 hadi leo hiyo hiyo, ingawa naweza kuwa sijalengwa vile vile)

    Nadhani iko hivi:
    - Unatumiwa email, kuwa kuna mabadiliko ya kiufundi (yahoo, msn, etc) na inakuja fomu kuwa ili kudhibitisha wewe ndio mwenye akaunti, weka jina (username) na password. Ukiweka tu, zinaenda kwao.
    - Wakipata., jambo wanalofanya wao ni kubadili password, hivyo huwezi tena kuingia.
    - halafu ndio wanatumia watu kwenye address list.

    Tatizo
    Hii huwa inawapata zaidi watu ambao (nadhani) sio wazoefu sana kwenye kutumia mtandao/emails za jumuia., hivyo wanaamini sehemu kubwa ya email wanazotumiwa.

    Suluhisho.
    Soma kwa makini kila email inayokuja.

    Angalia domain name.. mfano ni yahoo.. basi uwe kwenye domain ya yahoo

    Mara nyingi kudhibitisha password huwa inafanyika ukiwa ume log in kwenye akaunti yako

    Ukipokea email ya matatizo..sijui nimeibiwa pesa.. nk.. angalia uhusiano wako na muhusika, halafu subiri akutafute kwa njia kama ya simu. (Mi nilipokea email ya mtu kaibiwa pesa London wakati najua yuko Njombe kikazi)

    Na mwisho, Internet inatumiwa Dunia nzima, hivyo kuna watu wa kila aina na kila lengo

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 24, 2010

    Tamaa ndo zinawaponza ninyi.
    Mtu anakutumia email eti umeshinda bahatinasibu ambayo hujawahi kucheza halafu wanakwambia tuma taarifa zako email na password wewe unawatumia kwa uroho wako. Matokeo ndo hayo sasa, mnatusababishia tunaibiwa siye sasa.

    Au mnapokea email toka kwa wanigeria, eti yahoo inataka ku-update system yake kwa hiyo lete taarifa zako email na password yako, wewe bila kukaa ukafikiri unawatumia. Watanzania jamani tutaamka lini? Kabla ya kujibu email, soma kwanza, elewa, tafakari, ukishindwa omba msaada kwa wataalamu. Email kutoka kwa watu usiowajua, usijibu hasa kama wanataka detail zako

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 24, 2010

    Wewe unayesema mtu awe anabadilisha password mara kwa mara sio kweli. Kwa taarifa yako hata uwe unabadili 24 7. Hackers wakipata password wanaitumia within 2 to 3 hours.

    Study shows that frequent password changes are useless.

    Cha muhimu create a unique password that is hard to crack.

    Mix upper and lower case..

    Mix numbers and letters...

    Usitumie maneno ya dictionary.

    The longer the password the better.

    Usitumie password iliyofanana kwenye social sites na ya email yako. Ingawaje kama umeitengeneza password nzuri utasalimika kidogo lakini kwenye public au wireless internet ni risk sana..

    Na pia ni kutojibu email za watu usiowajua. Kwasababu mimi nikijua email yako nikataka kuhack give me good 6 hours. Sasa imagine huko nigeria na india wasomi walivyo wengi na hawana kazi. Wanachotaka ni email ya mtu tu na muda wanao mwingi tu wakufanya maasi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 24, 2010

    cha muhimu tuelezane wanaibaje hizi password ni kutoka kwenye server au computer au wapi?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 24, 2010

    Mdau Mwamgongwa Pole ka kadhia hii na wengi imewakuta
    Labda kumbuka siku za nyuma uliwahi kupokea email ikkutaka ku-update data zako ikiwa pamoja na password yako?Huwa jamaa wanatumia mbinu hii wakijifanya wao ni yahoo au mtandao mwingine wowote
    Kuna nyakati jamaa hawa huwa wanakutumia email kusema kuna mihela kadhaa wa kadhaa inakusubiri, hujui hata chanzo cha hzio hela watu wengi wamejikuta wakitoa data zao kwa hawa jamaa ambao huzitumia kuiba na kuwaibia wenye emauil hizi na akaunti zao za benki
    Kuweni makini

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 24, 2010

    UTAPELEKAJE PESA BAADA YA KUPATA EMAIL TU, SI UTATAKA KUHAKIKISHA KWANZA HATA KWA KUMPIGIA SIMU. KITU HAPA NI UGENI KATIKA MASWALA YA UTNDAWAZI HAYO MAMBO NI YA KAWAIDA SANA HUKU MAJUU NA WATU WAMESHAYAZOWEA, USITUMI PESA KWA OMBI TOKA KWENYE EMAIL NA USIFUNGUWE EMAIL YA WATU USIWAJUWA HATA KAMA WANAKUHAIDI PESA AU KAZI USIYOOMBA.

    ReplyDelete
  9. mdau hapo juu wa saa01:33:00,ni kweli kuna jamaa ambao wameliwa pesa wakidhani ni kweli ni mimi nina shida,hiyo mail ambayo ililetwa hapa ikaandikwa KANYABOYA jamaaa waliitranslate kwa kiswahili then ndio wakamtumia huyo mdau aliyeleta hapa,na siyeye tu ni wengi wamenilalamikia,mie nilikuja kushtuka kuna rafiki yangu mmoja nilikua naye siku nzima jana yake mpaka linakuchwa then amerudi kwake kakuta email ikimwambia mimi niko scotland nina shida anitumie pesa,ndio akanipigia kunitaarifu kwamba kapata hiyo mail vipi nimemtumia nataka pesa niko scotland wakati tulikua wote mda wote ndio namimi nikastuka kama jamaa wanafanya mchezo huo.hata hivyo sikujua kama ilifika huku ni jana tu nimeona hiyo mada hapa ililetwa mwaka jana oktoba ikaandikwa KANYABOYA.
    ISAAC MWAMGOGWA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...