USAJILI WA NAMBA ZA SIMU ZA MKONONI
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ilitoa agizo kuwa namba zote za simu za mkononi zisajiliwe Kati ya Julai 1 2009 hadi Desemba 31, 2009; na baadaye muda huo kuongezwa hadi tarehe 30 Juni 2010 ikitamkwa wazi kuwa muda huo wa ujasili hautaongezwa tena.
Sababu za kuanzisha utaratibu wa
kusajili namba za simu zimeelezwa mara kadhaa zikiwemo :
Kuwalinda watumiaji dhidi ya matumizi mabaya ya huduma za mawasiliano
Kuwezesha na kurahisisha utambuzi wa wateja watumiapo huduma mbalimbali kama M – Pesa, Z-pesa, ZAP na huduma nyingine za malipo ya Ankara kama za Umeme, Maji, Televisheni n.k.
Kuimarisha usalama wa nchi.
Kuyawezesha makampuni ya simu kuwafahamu wateja wao vizuri zaidi ili kurahisisha na kuboresha utoaji wa huduma kwao.
Wakati tukikaribia tarehe 30 Juni utaratibu umepangwa kupitia makampuni ya simu kuwa kuanzia tarehe 1 Juni 2010 laini yoyote itakayonunuliwa itatumika kwa kupiga au kupokea simu na kutuma au kupokea ujumbe ikiwa imesajiliwa tu na si vinginevyo.
Baada ya saa sita usiku tarehe 30 Juni yaani saa 00.00 kuanzia tarehe 1 Julai, 2010 namba yoyote ambayo itakuwa haijasajiliwa itafungiwa kupiga ,kupokea simu pamoja na ujumbe wa maandishi (SMS) kwa siku 90 hadi tarehe 30 Septemba 2010. Katika kipindi hiki cha siku 90 endapo utaisajili namba yako itafunguliwa . Kwa namba ambazo hazitakuwa zimesajiliwa ifikapo tarehe 30 Septemba zitafutwa na kuondolewa kwenye mitandao kabisa.
Mnakumbushwa pia kuwa hivi karibuni mswada wa sheria ya mawasiliano ya kielektroniki na posta ulipitishwa na Bunge kuwa sheria. Sheria hiyo inafanya usajili wa namba za simu za mkononi kuwa ni wa lazima kwa mujibu wa sheria kuanzia sasa na kutofanya hivyo ni kosa la jinai.
Mamlaka ya Mawasiliano inapenda kuyashukuru makampuni ya simu na watumiaji kwa ushirikiano ambao mumeuonesha mpaka sasa kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili.
USICHELEWE, SAJILI NAMBA YAKO YA SIMU MAPEMA!
Imetolewa na
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
moja katii ya sababu zilizotajwa ni Kuimarisha usalama wa nchi, hebu jamani nielimisheni hapa, hii ni kivipi? huku niliko mimi nina mobile phone ya pay as you go, sijaisajili popote pale na wala sijawahi ambiwa niisajili, sasa kama kuna hatari ya Kuimarisha usalama wa nchi kwa nini huku nje hilo hakuna?
ReplyDeleteHabari waungwana,
ReplyDeleteMimi sijafuraishwa na jinsi TCRA wanavyolishughulikia swala hili.
Kwanza walitakiwa wazuie sim cards kuuzwa kama njugu yaani watumiaji wapya wote wasajiliwe kisha ndio wawasajili wale wa zamani. Badala yake wameanza kusajili namba huku wakiruhusu sim card kuuzwa kama njugu. To me hii haina tofauti na kujaza maji kwenye ndoo iliyotoboka bila kuziba tundu kwanza.
Pili, ni hii sheria ya kumwadhibu mteja atakayetumia line isiyosajiliwa. Nafikiri ni busara kumwadhibu service provider yaani kampuni ya simu itakayoruhusu mteja asiyesajiliwa ku-access services zake. Kwa sheria hii inamaanisha Makampuni hayawajibiki coz at the end of the day haitakula kwao.
Huu ndio mtazamo wang kwa sasa. Asanteni.
hii haijakaa sawa, inamaana simu zote how about pay as you go, and i think most people haven't got contract. I may be there for short perion and need to communicate with people do i need to register my phone as well. Hii ni kubwa hakuna cha usalama wa nchi wala nini. they should register all sim card before selling them.
ReplyDeleteanon hapo juu:
ReplyDeleteNenda hata kwa majirani India mzee haijalishi unatumia sim card kwa muda gani lazima uregiste....lakini uzuri wao ni kwamba huuziwi sim card mpaka umepeleka documents za kuregister.
TCRA inabidi wazibane kampuni za simu ili zisiruhusu mtu kununua sim card mpaka awapatie documents ambazo watazitumia kuregister.
Ni kweli mambo yanakwenda kinyume. Inabidi wasajili sim cards mpya pale pale wanapouza, na huku wanaendelea kusajili za zamani. Kwa wale walalamikaji ambao wako nje ya nchi, mpango huu pia unatumia katika nchi nyingi za Ulaya ZENYE AMANI NA UTULIVU.Tofauti na UK na nchi nyengine ambazo watu wanafanyiziana kwa kutumia simu,anuani za nyumba n.k ili kumtia hatiani mwenzake kwa makosa makubwa.
ReplyDelete