Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi tawi jipya la benki ya CRDB huko Marangu, moshi vijijini Jana mchana.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Dr.Charles Kimei na kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Benki hiyo Martin Mmari.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua tawi jipya la Benki ya CRDB muda mfupi baada ya kulifungua huko Marangu,moshi vijijini jana mchana.Watatu kushoto pembeni ya Rais ni mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Dr.Charles KimeiRais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dr.Charles Kimei muda mfupi baada ya kulifungua tawi jipya la Benki hiyo katika kijiji cha Marangu,wilaya ya moshi vijini jana mchana.Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo Bwana Martin Mmari.
Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Vunjo Aloyce Kimaro muda mfupi baada ya Rais Kikwete kufungua tawi jipya la benki ya CRDB katika kijiji cha Marangu,wilaya ya moshi vijijini.Kijiji cha Marangu ni sehemu ya jimbo la Vunjo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia baadhi ya wananchi wa kijiji cha Marangu walihudhuria sherehe za ufunguzi wa tawi jipya la CRDB kijijini hapo jana mchana.
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro Lucas Ng'oboko akimuonesha Rais Jakaya kikwete chumba cha Mahabusu katika kituo kipya cha Polisi katika kijijicha Okaoni,Kobosho wilaya ya moshi vijijini jana muda mfupia baada ya Rais Kikwete kukifungua kituo hicho kilichojengwa kwa nguvu ya wananchi kwa kushirikiana na jeshi la polisi nchini.Rais kikwete pia alifungua nyumba mbili mpya za maofisa wa polisi watakaotoa huduma katika kituo hicho.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia baadhi ya wananchi wa kijiji cha Marangu walihudhuria sherehe za ufunguzi wa tawi jipya la CRDB kijijini hapo jana mchana.
(picha na Freddy Maro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 27, 2010

    Hakuna jipya.... tunataka kima cha chini 315,000.00 japo hutaki kura zetuu...

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 27, 2010

    wewe Anon wa may 27,05:06:PM
    vipi? unauliza makalio ya mbwa wakati mkia unauona!huyo mwenye kofia nyekundu ndie yeye ras makunja sema tu leo gitaa lake lipo kwa fundi,lakini ndie mwenyewe kiongozi wa watoto wa mbwa ffu

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 27, 2010

    Wee acha wafungue kwanza hapo Marangu. Ungejua wateja wako wengi sana hapo na mama yangu ni mmoja wao na alikua mpaka aende Moshi mjini. bank hii matawi ya juu wana foreign account hapo ukiweka hela kabdla ya saa 9 mchana mama anaipata siku hiyo hiyo. Lakini kwenda Moshi mjini ndio inakua matatizo tena.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 27, 2010

    kuna watu wana macho makali !unajua uyu kamanda amenipa kisogo sikujua kama ndie yeye ras makunja.
    naona yupo kistaraabu leo,bila kifaa cha kazi

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 27, 2010

    hivi, usalama wa rais upo hapo kweli?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 28, 2010

    Napenda kutoa maoni kuhusu kampala International University.Kama mdau alivyolonga hapo juu ni kweli usiopingika kua hawa waheshimiwa wanatoza ada kwa dola za Kimarekani wakati mishahara na gharama zote wanalipa kwa fedha za kitanzania na hazibadiliki (Fixed). Ni wakati wa watanzania kurudi nyuma na kuangalia kama ni lazma kusoma kwao ama wana elimu nzuri ambayo tunakimbilia moja, ama wanajua mapungufu ya elimu yetu hivyo wanaleta tiba mbadala hivyo kutulazimu kwenda hapo. kama wangekosa wanafunzi nadhani wangejiuliza kuna nini.

    tuna TCU hapa je sio moja ya kazi zao kuangalia utaratibu wa kuendesha vyuo. Prof Mayunga nadhani hapa unaweza kutusaidia.

    embu tuweke taratibu za kuwekeza Tanzania na tuzifuate vinginevyo tutahukumiwa na vizazi vijavyo. Mdau na mwanafunzi muathirika wa utaratibu wa KIU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...