Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemaliza hotuba yake sasa hivi wakati akiongea na wazee wa jiji la Dar es salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee hall. Katika hotuba hiyo iliyodumu saa moja nzima alizungumzia mambo kadhaa, na kubwa lililochukua nafasi kubwa ni kuhsu mgomo uliotishwa na TUCTA uliopangwa ufanyike Mei 5, 2010 ambapo wafanyakazi wamehimizwa kugoma. Kwa kifupi kasema
*Mgomo ni batili kwani haukuangalia maslahi ya wengi
*Ameshangaa unaitishwa mgomo Mei 5, 2010 wakati kuna mazungumzo yanaendelea kati ya serikali na TUCTA, ambapo pande hizo mbili zina mihadi ya kuwa na mkutano Mei 8, 2010
* Amesema pendekezo la TUCTA kwamba kima cha chini kiwe laki 315 amesema halitekelezeki kwani serikali sio tu haina uwezo wa kulipa wafanyakazi kiwango hicho, bali pia itakuwa inanufaisha watu wachache wakati mamiliioni wengine wakisota. Hapo akimaanisha pato lote la Taifa haliwezi kutumiwa na sehemu tu ya wananchi (wafanyakazi wasiozidi laki 5) ambapo zaidi ya milioni 35 wangeathirika kwani pesa hiyo haipo labda ikopwe.
*Amesema viongozi wa TUCTA ni wanafiki kwani wanahudhuria vikao vyote vya maamuzi ambapo sio tu husaini fomu za posho bali pia hata makubaliano yanayofikiwa na chama hicho na serikali katika vikao mbalimbali vya tume na baraza.
* Amewaasa wafanyakazi watumie hekima na busara katika maamuzi yao dhidi ya kauli za viongozi wa TUCTA ambao amesema hawawaambii ukweli wananchi kwa maslahi yao.
*Amesema ukweli ni mwisho wa matatizo, hivyo hawezi kuwa mnafiki wa kuwaongopea wafanyakazi kuwa atawalipa kiasi wakitakacho ili "kujipatia kura" wakati wa uchaguzi mkuu, akasisitiza kwamba serikali ina nia ya kulipa wafanyakazi wake vyema, lakini kwa kadri ya uwezo wake ilionao.
Juhudi zinafanywa kupata hotuba kamili..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2010

    kama amekosa cha kusema akae kimya, mawaziri na maofisa wa serikali wanasaini posho ngapi? mbona hizo hajaziongelea? halafu kuwaita TUCTA kwenye mazungumzo na kusaini posho ni nani aliyeaandaa hizo posho? kama mngewaita kwenye mazungumzo bila ya kuwapa posho kulikuwa na shida gani?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 03, 2010

    Na wao TUCTA walikuwa wapi siku zote mpaka wasubiri uchaguzi ndio wajitie kugoma? Nani asiyejua kuwa uchumi umeyumba dunia nzima, sasa mwaka huu tu peke yake ndio utatosha kumaliza matatizo ya wafanyakazi ya miaka na miaka? Kama hao viongozi wa TUCTA wanatumia na watumike vizuri lakini mgomo sijui mgumu hauna maslahi yoyote kwa wafanyakazi wala taifa kwa ujumla. Hebu niambie hao wafanyakazi wakigoma wiki nzima, nani atakayewapa posho za kujikimu na familia zao? Kawaida mgomo inabidi watu wajiandae hasa wajue wataishije pale ambapo mwajiri atasema basi umetoka wewe ataingia mwingine, kumbukeni kuwa soko limejaa watu waliomaliza shule na hawana kazi na wanahitaji hizo nafasi za kazi.

    Mfano mdogo ni mgomo wa BA jinsi watu walivyochangamkia nafasi za waliogoma tena kwa kujitolea na kulipwa posho. Wallahi ningekuwa mimi JK ningesema, wagome kisha naamuru waajiriwe wengine ambao wako mabarabarani wanasaga soli kutafuta ajira!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 03, 2010

    Presidaa hapo kachemka, hapa hajatutetea wafanyakazi bali kaleta ubabe tu.Si tulitegemea angezungumzia ukubwa wa makato ya mmwezi kwenye mishahara yetu yamezidi kua makubwa mno yaani unasurrender hadi 1/3 ya mshahara kwenda kwenye makato huu ni uonevu. Bora basi mifuko ya hifadhi za jamii ingekua inawapatia makazi bora wanachama wake zenye thamani kulingana na makato ya mwezi ya mwanachama lakini wapi serikali yenyewe ndio imekua mstari wa mbele kujichotea hela za mifuko hii kufanyia mambo yake huku mfanyakazi akibaki masikini. Anoni wa Mon May 03, 09:18:00 PM hujui shida za wafanyakazi maana najua wafanya biashara kodi hulipa mara moja tu kwa mwaka zilizobaki wateja wao huwachangia kupitia VAT so hawezi kujua ndani ya pay slip kuna majonzi gani

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 03, 2010

    Rais hapa mi huwa simuelewagi, Unaongea na wazee wa Darisalaam kuhusu wafanyakazi na hawa wazee wamelipwa kajiposho kuja kukusikiliza unatarajia hawata piga kelele za shangwe kila ukisisitiza jambo? Kwa nini usingeomba uwahutubie wafanyakazi wenyewe halafu uwaambie tunaongeza kakodi ka PAYE kidogo uone kama watakushangilia kishabiki kama hao wazee uliowahutubia pale Diamond. Hongeleni TUCTA angalau mmeweza kupaza sauti zenu mbele ya majukwaa japo serikali yetu haitujali lakini huduma zetu inazithamini na inajua madhala yake pindi zikikosekana Wasioelewa wachache kama anoni wa Mon May 03, 09:18:00 PM ndio watakao sema wafanyakazi wafukuzwe ati kwa kugoma. We unajua gharama za kuajiri mfanyakazi mpya kazini au unaropoka tu. Leo hii timu ya madaktari mhimbili, Mwananyamala, Temeke, Ilala, KCMC Bugando n.k, Wafanyakazi wote kwenye wizara,na idara za serikali viwanya vya ndege bandarini, uhamiaji mipakani n.k uwafukuze kazi kwa kugoma unaweza kupata wengine kwa mara moja utawapata wapi? Na kwa muda gani au unafikiri ni rahisi? Kama unadhani ni rahisi subiri (kama ni mwanaume)mkeo ajifungue then fukuza mfanyakazi wako wa nyumbani wakazi mkeo kamaliza maternity leave uajili mwingine asiyejua kufua, kupika, wala kumshika, kumlisha na kumwogesha mtoto uone kazi ya kumfundisha ilivyokua ngumu huku wote mkiondoka kabla jua halijatoka, mkirudi saa mbili usiku. Usiropoke mambo kirahisi tu.Fikiria kidogo

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 03, 2010

    Ankal naomba usibane comments za watu,inakuwa haina maana unaweka maada/habari halafu watu wanapochangia unakuwa bias bila kujali huyo mtu ametumia muda wake wa kuandika na kuwasilisha maoni yake. Tanzania haiwezi kujengwa kama tukiwa waoga ankal. Baada ya kusema hayo maoni yangu ni kama ifuatavyo;

    Izingatiwe kuwa wakati wabunge wanalipwa mamilioni ya fedha kwa mwezi, wafanyakazi wengine hususani watumishi wa umma kama walimu, wauguzi, maaskari nk wengi wao wanalipwa kima cha chini ambacho ni chini hata ya fedha anazolipwa mbunge kwa siku moja. Inasikitisha sana kuona kiongozi wa nchi anatangaza kwamba suala la wafanyakazi kuongezewa mishahara yao halitatekelezwa kikamilifu kutokana na visingizio mbalimbali. Hii ni ishara ya matabaka katika taifa, kwani wakati wabunge wanajiongezea wenyewe kipato na kupata mapato ya kiwango cha kufuru ukilinganisha na hali ya taifa; wabunge hao hao wanashindwa kuibana serikali kutekeleza ahadi zake. Baadhi ya wabunge wamegeuka kama wenye shibe wanaosahau wenye njaa.
    Nachukua fursa hii kuhamasisha wananchi kuitaka serikali kuweka rasmi wazi kwa umma, kiwango cha mishahara na posho wanacholipwa watumishi wakuu wa serikali wakiwemo viongozi wa kisiasa. Kadhalika, tunaitaka serikali iweke wazi ripoti ya Tume ya Ntukamazima ambayo iliteuliwa mwaka 2006 na kukamilisha kazi yake mwaka 2007 ya kupendekeza nyongeza ya viwango na maslahi ya wafanyakazi. Hii itawezesha watanzania kuwianisha vizuri mapato ya kada zote za wafanyakazi na kuunganisha nguvu katika kuhakikisha mapendekezo ya ripoti hiyo na matakwa ya umma kuhusu uboreshaji wa maslahi ya wafanyakazi nchini yanatekelezwa.

    Mdau Ughaibuni

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 03, 2010

    Mon May 03, 10:33:00 PM unasema ankal asibane comment angalia kwanza kichwa cha habari yenyewe kabla hujakurupuka kupoteza nguvu kuandika comment yako

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 03, 2010

    Mbona maoni yetu hatuyaoni? Acheni kubania tuliyesema kutokana na uzembe huu unaofanywa. Natarajia nitasoma maoni yangu kama nilivyoandika.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 04, 2010

    Nimechangia maoni yangu tangu saa 3 za usiku na sijayaona. Sasa kaka michuzi unaweka mada za nini kama kunakuwa na ubaguzi kiasi hiki? Bila shaka umefaidika na kutouweka mchango wangu hapo!

    ReplyDelete
  9. msemma kwelliMay 04, 2010

    Naomba mungu maoni yangu yatatolewa, maana mpaka tunahisi hii blog inakaupendeleo kwa walio madarakani kuliko wakaretwa!

    Rais akisema serikali haina hela ya kuwalipa wafanyakazi ana maana gani?

    Mbona hatujasikia hata siku moja amekwama kwenda safari za nchi za nje sababu hakuna hela BOT?

    Hela za kuwalipa wabunge, 12m/- kwa mwezi zinatoka wapi, na hizi za juzi tu kuboresha majimbo (kama vile!) je nazo zimetoka wapi?

    Tunajua hela zipo maana idadi ya wafanyakazi ni ndogo kuliko pato la nchi kwa mwezi.

    Kuweza kuwalipa hawa wafanyakazi ni rahisi.

    -Tupunguze misamaha ya kodi, kuimarisha tathmini na ukusanyaji wa kodi.
    -Kupunguza matumizi yasiyo na maana wizarani, kwenye mashirika na posho za mikutano, ambazo hazina kichwa wala miguu, kama wafanyakazi hawatokei mikutanoni, sheria zipo.
    -Tusiamini kuwa wawezekaji mi miungu, wao wanakuja watengeneze pesa, kwaio watafanya kila hila wafanikishe hilo, jamani tuwe na uchungu na rasilimali za nchi.
    -Magari ya kifahari na anasa zingine serikalini kama zingeondolewa kabisa, basi kusingekua na ulipaji mdogo wa mishahara.
    -Makampuni binafsi kama hayawezi kulipa kima cha chini kilicho "realistic" na maisha bongo, basi wafunge biashara zao, mie mfanyabiashara, najua wafanyabiashara wenzangu, kwetu ni faida tu bila hata kujali binadamu wenzetu.
    -Nchi yetu itumie na kufaidaka na rasilimali, ama sivyo, lazima walalahoi watakuja juu, maana inaonekana, nchi hii viongozi wamesahau binadamu wengine kabisa!

    ReplyDelete
  10. ADILI NA NDUGUZEMay 04, 2010

    Nyie wote wachangiaji hamna utaalamu. Mishahara inatakiwa iwe endelevu. Siyo leo unalipa mwezi unaofuata hulipi. Halafu inasimamiwa kisheria. Serikali ikishindwa kuwalipa wafanyakazi serikali itashtakiwa. Wakati suala la posho za safari hizo unaweza ukafuta safari au ukapunguza idadi ya watu wa kwenda safari na hubanwi kisheria.

    Haya masuala ni ya kibajeti. Kwa hiyo kuhusisha safari za kikazi za Rais na viongozi wengine ni masuala ya kibajeti ambapo hali isiporuhusu safari inafutwa wala haileti mgogoro.

    Hizo allocations nyingine kama mishahara ya wabunge siyo ya kudumu. Ndiyo maana wanalipwa gratuities. Akishindwa ubunge basi.Tunazungumzia wabunge 232. Ilhali wafanyakazi wako 350,000. Sasa hapo ni suala la mahesabu. Nilitegemea TUCTA nao wangekuja na maelezo ya kisomi kumchallenge Rais. Mimi binafsi naona maelezo ya Rais yana hoja. Nyie wenzangu mmeamua kumcharaza tu wala hamjachallenge alichosema.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 04, 2010

    Taarifa ya mkaguzi mkuu inaonyesha kuwa shilingi trilion 1.7 zilitumika kulipa wafanyakazi hewa. Serikali ilipendekeza wafanyabiashara mabepari wafidiwe hasara iliyotokana na kuvurugika kwa uchumi wa dunia na shillingi trillioni 1.7 zilitengwa kwa kazi hiyo (pengine ni EPA nyingine ya pesa za uchaguzi). Kuna upotevu mwingine kibao wa mabilioni kwenye taarifa ya CAG kila mwaka wa fedha ukiacha matumizi ya anasa ya viongozi wetu. Uwezo wa kulipa upo ila utu sasa haupo kwani watu wanajijali wao tu na kuacha wengine wateseke.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 04, 2010

    we adili na nduguze umechallenge nini sasa hapo. watu wengine bana. natamani nikuone!! nadhani hujui unasema nini. afu wewe michuzi comment za maana huweki na badala yake unaweka malalamiko

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 04, 2010

    laanakhum...

    JK una chuki binafsi/bifu na MGAYA?

    mbona umemuaddress kwa jina lake kiivo?

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 04, 2010

    unaweza ukawa na pointi JK,ila jinsi ya ku-present mada yako umechemka BIG TIME

    ovyo kabisa!!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 04, 2010

    Jamani kwa upande wangu mimi naona Rais ana hasira ya kutoalikwa kwenye sikukuu ya Mei mosi, Na inawezekana TUCTA nao kuna baadhi ya process waliskip lakini hatuwezi kuwalaumu TUCTA kwa sababu kwanza wanapigia kelele haki y amfanyakazi wa Tanzania sio ya Mgaya kama Raisi alivyokuwa anasema,

    Lakini pia toka mwanzo serikali haikwenda sambamba na TUCTA kuketi kwenye meza kwa majadiliano mpaka pale walipoona kwamba kweli TUCTA walikuwa serious na ule mgomo, Serikali kwa Busara zake walitakiwa wapange tarehe ya majadiliano siku 1 au 2 kabla ya mgomo ule kama kweli walitaka suluhu ya matatizo

    Kwanini Ang'anganie tu mshahara wa 315,000/= tu, mbona kuna madai mengine hakuyasema kama kodi kwenye mshahara, tunaumia jamani wale wazee ni wanafiki wanapiga makofi wakati mwisho wa mwezi wanatuomba pocket money usipotuma hela maneno

    Watanzania tuungane tutetee haki yetu, hata kama sio 315,000 basi angalau watufikirie, Maisha bora mshahar awa laki 1 yanatoka wapi???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...