Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini jioni ya leo, Mei 30, 2010, kwenda Kampala, Uganda, kuhudhuria Mkutano wa Kwanza wa Nchi Wanachama wa Mkataba Ulioanzisha Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC).
Rais Kikwete anahudhuria Mkutano huo kwa mwaliko wa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Mheshimiwa Ban Ki Moon.
Mkutano huo unaoanza kesho, Jumatatu, Mei 31, 2010, miongoni mwa mambo mengine utapitia na kufanya marekebisho katika Mkataba ulioanzisha ICC.
Mkutano huo unatarajiwa kumalizika Juni 11, 2010, lakini Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nyumbani keshokutwa, Juni Mosi, 2010.
Aidha, mkutano huo unatarajiwa kupitia orodha ya makosa manne yanayoorodheshwa chini ya Mamlaka ya ICC kwa lengo la kuongeza ama kuyatolea ufafanuzi zaidi makosa hayo.
ICC ina Mamlaka ya kuhukumu makosa manne ambayo ni Mauaji ya Kimbari (Genocide), Makosa Yafanyikayo Wakati wa Vita (War Crimes), Makosa Dhidi ya Binadamu (Crimes Against Humanity) na Uchokozi ama Ushari (Aggression), kosa ambalo halijapata tafsiri inayokubalika kimataifa katika Mkataba huo wa Roma
Mkutano pia utafanya tathmini ya shughuli za Mahakama hiyo tangu ilipoanzishwa Agosti, 1998, mjini Roma, Italia na kupendekeza namna ya kuboresha shughuli hizo.

Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi.
Ikulu-Dar Es Salaam
Mei 30, 2010
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi.
Ikulu-Dar Es Salaam
Mei 30, 2010
Uniform ya askari wao na jinsi walivyojipanga bila kubanana inaonesha kuwa jesi lao liko makini zaidi
ReplyDeleteInternational Criminal Court Review Conference. Are they (politicians) lawyers?
ReplyDeletethis is official engegment why our president is not wearing proper suit
ReplyDeleteA four years old.......sio right just to say a four years....a four years what relationship, colege, school, vision etc etc
ReplyDeleteAfrika mitindo ya wakubwa kuimbiwa nyimbo za kuwasifu haiishi? Kwa mtindo huo wangapi wanapoteza muda wa kazi zao na kuishia kusubiri wakubwa watue uwanja wa ndege masaa kadhaa na kujipanga barabarani kuwashabikia.
ReplyDeleteTufikiria mambo kiuchumi na hayo yanayotendeke yanaathiri vipi uchumi wa matiafa ya kiafrika.
Wangapi wanaacha kazi ofisini. viwandani, mama ntilie, machinga nk kwenda kuwalaki wakuu waliotoka kutumia mapato ya walipa kodi?